UBINAFSISHAJI ULIOFANYIKA ULAYA BAADA YA VITA KUU YA PILI (WW-2)
Ndg.wana JF, kwa ufupi tu, ule ubinafshaji uliofanyika kwa wazungu baada ya WW-2 ni tofauti sana na huu unaofanyika hapa kwetu TZ.
Wazungu wao waliwachukuwa WANANCHI wao/watu wao/makampuni Yao, aidha yakiwa ndani ya nchi ama nje, i e Europe ama USA, n.k. Wakapa na ruzuku kupitia mabanki yao. Hii iliwafanya waendelee kwa haraka kwani wote ni wamoja! Lakini sisi tunamchukuwa Mwaarabu aliyetufanya watumwa, ama Mzungu aliyetutwala)Mkoloni, eti atuendeshee biashara, viwanda, mashamba, bandari, viwanja vya NDEGE, machimbo ya madini mbali mbali, je ni kweli atatuendeleza?
Mie sielewi hii akili Watanganyika tumeipata wapi? Aidha, itoshe kusema tu kuwa sisi Watanganyika/Watanzania sote tumelaaniwa, tuna laana ama tumerogwa. Nani katuroga? Huenda hata aliyeturoga kafa labda! Shame on us! Hivi hata Waafrika wenzetu, majirani zetu hatuzomei na kutuonea huruma sisi? Mbona ktk mataifa ya Wazungu mmoja/nchi ikifanya vibaya wengine wanaingilia kati? Yaani kama EU/US, je kwetu mboa AU ipo kimya?
Hebu wana JF hapa tusaidiane kwa mjadala wa kina ili vizazi vijavyo vifahamu kuwa karne fulani sii wote walikuwa vilaza kama kina Chief MANGUNGA wa MSOWERO KILOSA MOROGORO. Huyo hakusoma, naye ni "CHIEF" Je hawa wetu ""CCM""si wamesoma? Tena na historia ya akina MANGUNGA, imrkuwaje?
Jadili, paza sauti na tuwashauri.