Ishu kubwa bandari iendeshwe kisasa cargo ziingie na zitoke kwa wakati maswala ya usenge wa wabongo wanao fanya hapo kushirikiana na tra yaishe.Kukabiliana na wabongo wezi imeshindikana kwa hiyo suluhisho ni kuwapa waarabu ambao sio wezi, kweliii!!!! Kwa nini wabongo wanakuwa wezi? Kuna mwenye hili jibu? Kama haliko kwa nini lisijulikane na kupatiwa ufumbuzi.
Hii ishu mimi naiona ni kama mzazi nyumbani kwake kuna chakula kingi. Ila anao watoto ambao watukutu na si waaminifu wanadokoa hicho chakula.
Kudhibiti huo udokozi anaona karaha. Hivyo anaamua jambo la kufanya ni bora mimi niwe na uhakika wa kupata chakula njaa niisikie tu huko. Baada ya kupata huo uhakika anasema sasa hiki chakula kilichopo kwa vile watoto hawa sio waaminifu basi ngoja nifungulie na mbwa nao waje kugombania na kugawana hicho chakula na watoto. Uzuri wenyewe hawa mbwa ni wale waliopata mafunzo hawawezi kuwadhuru watoto zaidi ya kula hicho chakula na watoto.
Serikali ilinunua ndege za biashara mnashangilia, ikikodisha bandari ili isifanye biashara mnasifia! Tanzania nchi yangu TanzaniaIfike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.
Kwa taarifa zaidi soma hapa >> Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.
Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.
Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?
Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.
Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.
It
Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
Unataka tulie? Haya nalia sasaSerikali ilinunua ndege za biashara mnashangilia, ikikodisha bandari ili isifanye biashara mnasifia! Tanzania nchi yangu Tanzania
Wakibinafsishiwa wabongo ndio utaona shoo lake. Wabongo unawajua unawasikia??UBINAFSISHAJI ULIOFANYIKA ULAYA BAADA YA VITA KUU YA PILI (WW-2)
Ndg.wana JF, kwa ufupi tu, ule ubinafshaji uliofanyika kwa wazungu baada ya WW-2 ni tofauti sana na huu unaofanyika hapa kwetu TZ.
Wazungu wao waliwachukuwa WANANCHI wao/watu wao/makampuni Yao, aidha yakiwa ndani ya nchi ama nje, i e Europe ama USA, n.k. Wakapa na ruzuku kupitia mabanki yao. Hii iliwafanya waendelee kwa haraka kwani wote ni wamoja! Lakini sisi tunamchukuwa Mwaarabu aliyetufanya watumwa, ama Mzungu aliyetutwala)Mkoloni, eti atuendeshee biashara, viwanda, mashamba, bandari, viwanja vya NDEGE, machimbo ya madini mbali mbali, je ni kweli atatuendeleza?
Mie sielewi hii akili Watanganyika tumeipata wapi? Aidha, itoshe kusema tu kuwa sisi Watanganyika/Watanzania sote tumelaaniwa, tuna laana ama tumerogwa. Nani katuroga? Huenda hata aliyeturoga kafa labda! Shame on us! Hivi hata Waafrika wenzetu, majirani zetu hatuzomei na kutuonea huruma sisi? Mbona ktk mataifa ya Wazungu mmoja/nchi ikifanya vibaya wengine wanaingilia kati? Yaani kama EU/US, je kwetu mboa AU ipo kimya?
Hebu wana JF hapa tusaidiane kwa mjadala wa kina ili vizazi vijavyo vifahamu kuwa karne fulani sii wote walikuwa vilaza kama kina Chief MANGUNGA wa MSOWERO KILOSA MOROGORO. Huyo hakusoma, naye ni "CHIEF" Je hawa wetu ""CCM""si wamesoma? Tena na historia ya akina MANGUNGA, imrkuwaje?
Jadili, paza sauti na tuwashauri.
Nitakuelewa sana Tena sana kama Ndugu yangu Chige na wadau wengine wa masuala ya maendeleo watakubali kujumuika kuchangia uzinwako huu. Tumsubiri.Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.
Hii naiwekaSerikali ilinunua ndege za biashara mnashangilia, ikikodisha bandari ili isifanye biashara mnasifia! Tanzania nchi yangu Tanzania
Wachache sana ndio watakaokuelewa,mfano mdogo mwendokasi tu wameshindwa kuuendesha kiufanisi na kila siku wanalalamika hasara ndio itakua bandari waliyoishindwa miaka yote,uendeshwaji wa ile bandari yetu ni kituko cha dunia kwa wakati tuliokua naoIfike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.
Kwa taarifa zaidi soma hapa >> Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.
Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.
Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?
Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.
Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.
Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
Mkuu unaweza kuweka ushahidi kama ni uwekezaji wa miaka 100?Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-
19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.
b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.
d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.
e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.
g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge
Sent using Jamii Forums mobile app
Umemsahau Binamu wa Mjombashangazi ?Hivi amekosekana Mzungu hadi aje Mwarabu?
Lakini bado naamini Watanzania wapo waneoweza .
Tatizo ni kutaka kuteua Kwa kujuana badala ya kutangaza hizo nafasi watu waombe Na kufanyiwa usaili.
Hata iyo kodi tutayolipwa italiwa na wachache labda tubinafsishe na Serikali ya CcmNaungana na wewe serikali kufanya biashara ni kunufaisha watu wachache tu maana wizi ni asili ya watanzania ziwekwe terms nzuri kimkataba ambazo zitaipa pesa za uhakika serikali wawaachie wawekezaji.hata ufanisi utakuwepo sana na malalamiko yatapungua sana
Kwa hoja hii basi hakuna kitu serikali itatakiwa kubaki nachoIshu kubwa bandari iendeshwe kisasa cargo ziingie na zitoke kwa wakati maswala ya usenge wa wabongo wanao fanya hapo kushirikiana na tra yaishe.
Bandari + tra imekuwa kichaka cha upigaji na kufirisi watu ,mjomba angu amefanya kazi hapo miaka ya 60 hadi Leo mifumo ni Ile Ile hakuna kilicho badilika. Contena zinajazana hapo muda unapotea kodi inapotea bado rushwa na ukiritimba umetawala .Bora serikali ikae bambeni ijipigie percent yake tu, huku mifumo ikiboreshwa.
Imebaki taNesco .
Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app