The Republican
Senior Member
- Dec 5, 2021
- 174
- 307
Hii imekaaje ndugu? Naomba maarifa kidogo kama hutojali.Sipendi ubinafsishaji wa Bandari ya Dar sababu itaondoa uwezo wa Clearing Agents ku clear mizigo kwa kodi ya chini kwa faida ya mteja haswa magari yaliyoyochakaa ambayo ni over taxed. Kwa mfumo uliopo, Clearing Agents wana nafasi kubwa ku clear mizigo kwa kodi ya chini kuliko ile ambayo TRA wangedai. Hii ni win-lose situation. Hakuna mtu mwenye akili nzuri anayetaka kulipa kodi ya TRA ambayo inaenda kununua Land Cruiser LC300 na kujenga mahekalu ya MaCCM.
Lisha kuwa halali, andamana sasaWewe ukiunga mkono haimaanishi jambo hilo ni halali.
Mashairika yote yauzweHuu ni ukoloni wa kidigitali/ Digital era colonialism ndio hizi hadithi wanakuja na mifumo yao ya kisasa. Huu ni ukoloni ule ule kwa mbinu za kisasa. Mifumo gani ambayo mswahili wa leo hawezi kuweka? Kuna wakati tuliaminishwa miamala ni Maximalipo tu mbona kuliwekwa mifumo mengine ya kiserikali na mambo yanaenda. Kinachotakiwa ni utashi na mitazamo ya waliopewa jukumu la kuongoza wenzao.
Binafsisheni na majeshi nayo kama mmeaamua kujitoa ufahamu kiasi hiki.
Wauze mashirika yote ya umma yanayo fanya biasharaCcm mnauza bandari yetu miaka 100? Mkataba gani wa miaka 100? Kwa malengo Yapi? Miaka 100 mabadiliko yatakua makubwa sana hapa Duniani, Kwanini tunahukumu vizazi vyetu vitatu au vinne kwa tamaa za sasa?
Baada ya hapo atakuja mwingine ajifanye Mzalendo wakati alishiriki uchafu!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mashairika yote yauzwe
Acha mvua inyeshe tuone panapo vuja Hawa viumbe wamezidi tamaaHakuna nchi ambayo imebinafsisha kila kitu mzee bandari ni sehemu nyeti sana huwezi kumpa mtu binafsi aendeshe kuna mambo mengi ya kiusalama kwetu na nchi jirani ni sawa na kuzi privatelize airports haiwezekani zitakuwa ni highways za kupitishia magendo na silaha haramu .
YAANI TUMPE MCHINA NDIO ASIMAMIE BANDARI YETU LOL!!
God forbid![emoji419][emoji375]Kama Alhaji Mwinyi Alivyifanya Loliondo Kuitoa Miaka 100 Kwa Mwarabu
Yanakwenda Kukamilishwa Tena Na Mama Anawapa Tena Waarabu Bandari Miaka 100
PUMBAUBINAFSISHAJI ULIOFANYIKA ULAYA BAADA YA VITA KUU YA PILI (WW-2)
Ndg.wana JF, kwa ufupi tu, ule ubinafshaji uliofanyika kwa wazungu baada ya WW-2 ni tofauti sana na huu unaofanyika hapa kwetu TZ.
Wazungu wao waliwachukuwa WANANCHI wao/watu wao/makampuni Yao, aidha yakiwa ndani ya nchi ama nje, i e Europe ama USA, n.k. Wakapa na ruzuku kupitia mabanki yao. Hii iliwafanya waendelee kwa haraka kwani wote ni wamoja! Lakini sisi tunamchukuwa Mwaarabu aliyetufanya watumwa, ama Mzungu aliyetutwala)Mkoloni, eti atuendeshee biashara, viwanda, mashamba, bandari, viwanja vya NDEGE, machimbo ya madini mbali mbali, je ni kweli atatuendeleza?
Mie sielewi hii akili Watanganyika tumeipata wapi? Aidha, itoshe kusema tu kuwa sisi Watanganyika/Watanzania sote tumelaaniwa, tuna laana ama tumerogwa. Nani katuroga? Huenda hata aliyeturoga kafa labda! Shame on us! Hivi hata Waafrika wenzetu, majirani zetu hatuzomei na kutuonea huruma sisi? Mbona ktk mataifa ya Wazungu mmoja/nchi ikifanya vibaya wengine wanaingilia kati? Yaani kama EU/US, je kwetu mboa AU ipo kimya?
Hebu wana JF hapa tusaidiane kwa mjadala wa kina ili vizazi vijavyo vifahamu kuwa karne fulani sii wote walikuwa vilaza kama kina Chief MANGUNGA wa MSOWERO KILOSA MOROGORO. Huyo hakusoma, naye ni "CHIEF" Je hawa wetu ""CCM""si wamesoma? Tena na historia ya akina MANGUNGA, imrkuwaje?
Jadili, paza sauti na tuwashauri.
Kama mnataka kubinafsisha kwa nini msiwambie watanzania wenyewe waunde makampuni waiendesha, au ndo ule jenerali Ulimwengu aliuita ugenishaji.
UBINAFSISHAJI ULIOFANYIKA ULAYA BAADA YA VITA KUU YA PILI (WW-2)
Safi Sana mama shikilia hapo hapo ukimaliza uje taNesco. Wabongo ni watu wapumbavu wanacho jali ni wizi halafu utendaji sifui
Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app