Naungana na Dkt. Lwaitama kuhusu Katiba Mpya

Naungana na Dkt. Lwaitama kuhusu Katiba Mpya

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Kwanza niwashukuru wale wate waliotoa mada na waliotoa maoni kwenye Kongamano lililopangwa na TLS. Ahsanteni sana.

Kipekee naungana na wazo la Dr. Lwaitama kuwa ni muda muafaka suala la Katiba mpya lianze na wakati wa kuandika katiba hiyo wasijumuishwe Vyama vya Siasa na jukumu hili waachiwe Wanasheria ili tupate Katiba Mpya.

Ameendelea kusema kuwa tayari tunayo draft ya Warioba ambayo itawaongoza Wataalam hao kuja na Katiba mpya na nzuri na iliyoboreshwa. Binafsi ninaafiki mawazo yake.
 
Tunataka Katiba Mpya bila masharti yeyote.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Kwanza niwashukuru wale wate waliotoa mada na waliotoa maoni kwenye Kongamano lililopangwa na TLS. Ahsanteni sana. Kipekee naungana na wazo la Dr. Lwaitama kuwa ni muda...
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi :pulpTRAVOLTA:
 
Iwe jua, iwe mvua wananchi wanataka Katiba Mpya.
 
Sababu za kutaka katiba mpya ni kubadili mfumo mzima wa utawala ambao ndio unasababisha kukosekana huduma bora ambazo wewe unaona ni muhimu.

Kupitia katiba mpya madaraka ya rais yatapunguzwa ili awajibishwe. Rais akiweza kuwajibishwa na wateule wake watawajibika. Hakutakuwa na ufisadi holela kwenye miradi ya maji, afya na elimu. Shughuli za chama zitatenganishwa na za serikali na kila mmoja atawajibika kivyake.

Bila katiba mpya hakuna huduma bora za afya, elimu wala maji. Hata ccm wanajua hilo lakini wanaogopa mabadiliko yatawafyekelea mbali.
 
Ccm na katiba mpya ni sawa na nyoka na panya
 
Kwanza niwashukuru wale wate waliotoa mada na waliotoa maoni kwenye Kongamano lililopangwa na TLS. Ahsanteni sana. Kipekee naungana na wazo la Dr. Lwaitama kuwa ni muda muafaka suala la Katiba mpya lianze na wakati wa kuandika katiba hiyo wasijumishw Vyama vya Siasa na jukumu hili waachiwe Wanasheria ili tupate Katiba Mpya. Ameendelea kusema kuwa tayari tunayo draft ya Mhe. Warioba ambayo itawaongoza Wataalam hao kuja na Katiba mpya na nzuri na iliyoboreshwa. Binafsi ninaafiki mawazo yake.
naunga mkono hoja
p
 
Tunataka Katiba Mpya bila masharti yeyote

naunga mkono hoja
p
Ccm na katiba mpya ni sawa na nyoka na panya
CCM kamwe haitakubali
Iwe jua, iwe mvua wananchi wanataka Katiba Mpya.
Tatizo si Katiba Mpya... Mkitaka Mpya watakuja nayo alafu muaminishwe kwamba ni Mpya!
Nionavyo tatizo kubwa ni wananchi pamoja na uelewa & mwamko mdogo!

Kwao chochote kitakacholetwa na ccm sawa tu!
 
Hii tuliyonayo inatumika ipasavyo??

Nadhani tuelimishane kwanza kwa hii iliyopo wengi waielewe

Ili ikija hiyo mpya iwe ni kwa uhitaji wa wengi na kugusa maslahi ya wengi.

Kwa hali jinsi ilivyo sasa naona kama wanaolilia katiba mpya ni wanasiasa tu kwa interest zao binafsi.

Yaani wapate wepesi kufikia lengo la kushika dola.
 
Kwani Katiba ni mali ya wanasheria? Je,hiyo Katiba inatumika kwa wanasheria tu? Tunawezaje kuwapa wanasheria kutunga Katiba wakati awana mandate kutoka kwa kwa wananchi. Lakini pia mbona tumeisha fika pazuri kwenye swala la Katiba,tunayo Katiba Pendekezwa sasa ni wajibu wa serikali kuileta kwa wananchi ili tupige kura ya ndiyo au hapana.
 
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi :pulpTRAVOLTA:
Huoni aibu hadi leo bado nchi inayoongozwa na chama chako haina uhakika katika huduma kama maji na elimu?
 
Sababu za kutaka katiba mpya ni kubadili mfumo mzima wa utawala ambao ndio unasababisha kukosekana huduma bora ambazo wewe unaona ni muhimu.

Kupitia katiba mpya madaraka ya rais yatapunguzwa ili awajibishwe. Rais akiweza kuwajibishwa na wateule wake watawajibika. Hakutakuwa na ufisadi holela kwenye miradi ya maji, afya na elimu. Shughuli za chama zitatenganishwa na za serikali na kila mmoja atawajibika kivyake.

Bila katiba mpya hakuna huduma bora za afya, elimu wala maji. Hata ccm wanajua hilo lakini wanaogopa mabadiliko yatawafyekelea mbali.
naona tu tatizo binafsi kwenye utawala na madaraka ya Rais ambayo kimsingi hayana tatizo kabisa as we are engaging. Nadhani umesahau uchaguzi🤣

kama hiyo katiba ingeeleza jinsi wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyibiashara, lakini pia huduma za kijamii kama vile afya, elimu, maji, miundombinu n.k vinavyopaswa kua haki ya waTanzania ningekuelewa..

Otherwise hiyo katiba ya kutaget vyeo na madaraka ni useless tu kama ya Kenya inavyowavuruga wenyewe 🤣

wameshindwa hata kutofautisha public participation na makelele 🤣
 
Tangu tupate uhuru ssa ni miaka 60 ila mpka leo maji tatzo hata kwenye mikoa yenye maziwa mf mwanza ssa unataka kuja kutatua tatzo wakati tatzo kubwa kwanza halijatatuliwa ambalo ni ccm
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi :pulpTRAVOLTA:
 
Back
Top Bottom