Naungana na Dkt. Lwaitama kuhusu Katiba Mpya

yaelezee basi kwenye hiyo katika mpya unayoitaka ili iwe mpya, sio kuzungumzia urasi tu kitu ambacho kipo taya kwenye katiba ya sasa, huo upya uko wapi sasa?

sasa huo upya uko wapi 🐒
Mkuu, katika members naowaona wana ufahamu mzuri wa haya mambo ya siasa na hasa Katiba ya Nchi, mmoja wapo ni wewe; kumbe ndivyo sivyo. Ahsante
 
Hii tuliyonayo inatumika ipasavyo??

Nadhani tuelimishane kwanza kwa hii iliyopo wengi waielewe

Ili ikija hiyo mpya iwe ni kwa uhitaji wa wengi na kugusa maslahi ya wengi.

Kwa hali jinsi ilivyo sasa naona kama wanaolilia katiba mpya ni wanasiasa tu kwa interest zao binafsi.

Yaani wapate wepesi kufikia lengo la kushika dola.
Hii ya sasa siyo explicit
 
Tatizo si Katiba Mpya... Mkitaka Mpya watakuja nayo alafu muaminishwe kwamba ni Mpya!
Nionavyo tatizo kubwa ni wananchi pamoja na uelewa & mwamko mdogo!

Kwao chochote kitakacholetwa na ccm sawa tu!
Katiba nzuri inatakiwa iwe kama moto.

Ukiichezea tu inakuchoma.
 
Mkuu, katika members naowaona wana ufahamu mzuri wa haya mambo ya siasa na hasa Katiba ya Nchi, mmoja wapo ni wewe; kumbe ndivyo sivyo. Ahsante
muhimu zaidi ni haki na uhuru wa maoni na mtazamo wa kila mwananchi kuskizwa bila makasiriko na kuhehimiwa bila chuki na mihemko 🐒
 
Kwanza niwashukuru wale wate waliotoa mada na waliotoa maoni kwenye Kongamano lililopangwa na TLS. Ahsanteni sana.

Kipekee naungana na wazo la Dr. Lwaitama kuwa ni muda muafaka suala la Katiba mpya lianze na wakati wa kuandika katiba hiyo wasijumuishwe Vyama vya Siasa na jukumu hili waachiwe Wanasheria ili tupate Katiba Mpya.

Ameendelea kusema kuwa tayari tunayo draft ya Warioba ambayo itawaongoza Wataalam hao kuja na Katiba mpya na nzuri na iliyoboreshwa. Binafsi ninaafiki mawazo yake.
MAJIZI CCM HAYATAKI KATIBA MPYA ITAWAFUNGA JELA
 
Uzoefu kutoka duniani kote kabisa unaonyesha kwamba Katiba Mpya zilizo nzuri KAMWE hazijawahi kupatikana hivi hivi tu bure bure kwa njia za amani bila ya kuingia gharama kubwa zaidi ya Machozi, Jasho na Damu. Nchi zote kabisa ambazo Leo hii zina Katiba nzuri hapa duniani zimewahi kuingia gharama za namna hiyo, hakuna hata nchi Moja ambayo Wananchi wake wamepata Katiba yao nzuri bila ya kupitia hatua hiyo ngumu, mbaya na ya hatari.

Mifano ya uthibitisho juu ya suala hili ipo mingi Sana karibia kwenye nchi zote kabisa hapa duniani. Mathalani, majirani zetu wa Kenya walipata Katiba yao waliyonayo hivi Sasa (ambayo kwa kiasi kikubwa Sana ina sifa za kuwa Katiba nzuri), waliipata Katiba hiyo baada ya kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2007/2008 baada ya Uchaguzi Mkuu kwenye nchi hiyo. Vita hiyo ndio kiini cha kulazimisha kupatikana kwa Katiba yao waliyonayo hivi Sasa.
Unaweza kusema hiyo ndio njia pekee ambayo CCM inatengeneza, lakini njia nyingine ni CCM kupasuka na hii itatokea sooner or later. Maana wanatumia majeshi ya ulinzi na usalama kwa kuendelea kukaa madarakani kwa gharama yeyote ile, sioni kwa Tanzania hii kutokea
 
Makamba Snr alisema Katiba Mpya haitaleta ugali mezani.
Huyu ni mtoto wa mmoja wa wazee wa hovyo nchini Makamba, hawa ni wapotoshaji na wanatetea matumbo yao tu. Wanaogopa katiba mpya kama rasimu ya tume ya Warioba ilivyopendekeza itawatoa kwenye ufalme waliojitengenezea
 
muhimu zaidi ni haki na uhuru wa maoni na mtazamo wa kila mwananchi kuskizwa bila makasiriko na kuhehimiwa bila chuki na mihemko 🐒
Wewe mzee Makamba kama kuna hukumu huko wewe kuni na uzao wako, unajua kweli ya mapungufu ya hii katiba. Na mwenzako Wassira kazi yenu ni kupotosha kweli kwa maslahi yenu, hamna uzalendo kama Mwalimu Nyerere kukemea uovu, mlaaniwe na vizazi vyenu tena tutawaona mnavyodhalilika
 
ni jambo la maana sana kurelax unapozunguzia jambo hili muhimu sana kwa mustakabali mwema wa mama Tanzania..

kujihesabia haki na kuhukumu wengine ni kujaribu kunyang'anya majukumu ya Mwenyezi Mungu, na hicho ni kiwango kibaya zaidi cha tamaa ya binadamu kwa mambo asiyoyaweza na yasiyo muhusu...

hata hivyo bado haina maana yoyote eti, unachokiona wewe ni upungufu na mwingine akaona ni sio upungufu unamkasirikia 🤣

huo ni uking"ang"anizi useless na nonsense kabisaa..

katiba ya kuzungumzia vyeo na madaraka ya kisiasa si muhimu sanaa kwa sasa Tanzania, unless iwe imezingatia vipaumbele na maslahi mapana ya wananchi kama vile maji, elimu,afya, kilimo, miundombinu, biashara, uvuvi haki, uhuru na mahitaji mengine ya msingi , na sio muhemko, chuki na hizo ghadhabu na hasira za mkizi 🐒
 
Kwanza niwashukuru wale wate waliotoa mada na waliotoa maoni kwenye Kongamano lililopangwa na TLS. Ahsanteni sana.

Kipekee naungana na wazo la Dr. Lwaitama kuwa ni muda muafaka suala la Katiba mpya lianze na wakati wa kuandika katiba hiyo wasijumuishwe Vyama vya Siasa na jukumu hili waachiwe Wanasheria ili tupate Katiba Mpya.

Ameendelea kusema kuwa tayari tunayo draft ya Warioba ambayo itawaongoza Wataalam hao kuja na Katiba mpya na nzuri na iliyoboreshwa. Binafsi ninaafiki mawazo yake.
Lile bunge la katiba lilisheheni wanasiasa watupu matokeo yake tuliyaona....hawa wataalamu nao...
Pascal Mayalla
 
Sisi mchakato wa katiba tulishafunga mjadala tunayo rasimu ya kitiba ya warioba
 
ni jambo la maana sana kurelax unapozunguzia jambo hili muhimu sana kwa mustakabali mwema wa mama Tanzania..

kujihesabia haki na kuhukumu wengine ni kujaribu kunyang'anya majukumu ya Mwenyezi Mungu, na hicho ni kiwango kibaya zaidi cha tamaa ya binadamu kwa mambo asiyoyaweza na yasiyo muhusu...

hata hivyo bado haina maana yoyote eti, unachokiona wewe ni upungufu na mwingine akaona ni sio upungufu unamkasirikia 🤣

huo ni uking"ang"anizi useless na nonsense kabisaa..

katiba ya kuzungumzia vyeo na madaraka ya kisiasa si muhimu sanaa kwa sasa Tanzania, unless iwe imezingatia vipaumbele na maslahi mapana ya wananchi kama vile maji, elimu,afya, kilimo, miundombinu, biashara, uvuvi haki, uhuru na mahitaji mengine ya msingi , na sio muhemko, chuki na hizo ghadhabu na hasira za mkizi 🐒
Unafiki utabaki kuwa ni unafiki tu, hakuna jinsi nyie corrupted CCM mnaweza kujificha kwa hili. Hamtaki na mko tayari kupotosha kweli lazima mkemewe kwa ukali, unaweza kuniambia sababu gani ilikwamisha rasimu ya Warioba?

Ni kuogopa kutoka madarakani kwa mijizi ya CCM, mwanao January alinukuliwa akisema katiba itakuletea ugali? Je siyo ulevi wa madaraka kuwakejeli watanzania huko?

Nyie wahuni tu mlaaniwe kwa kutaka kuiingiza nchi yetu kwenye shida sababu ya uroho wenu wa madaraka
 
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi :pulpTRAVOLTA:
Hayo mahitaji muhimu ni life time, watu wanazaliana kila siku. Hilo la katiba ni one time.
 
Lazima katiba hiyo mpya,
kabla ya mambo mengine yote, itengeneze na kuandaa mazingira ya uhakika ya mahitaji hayo muhimu ya lazima ya kibinadamu maji, afya, elimu kunafaisha wanadamu wa idadi yoyote hata kwa miaka mia5 ijayo,

hiyo ya vyeo na madaraka, halafu eti ndio iwe katiba mpya, ni upotoshaji. Hayo yatakua marekebisho tu kwa manufaa ya wanasiasa 🐒
 
Hii iliyopo ndiyo ipo kwa manufaa ya wanasiasa zaidi.
 
Unafiki utabaki kuwa ni unafiki tu, hakuna jinsi nyie corrupted CCM mnaweza kujificha kwa hili. Hamtaki na mko tayari kupotosha kweli lazima mkemewe kwa ukali, unaweza kuniambia sababu gani ilikwamisha rasimu ya Warioba?

Ni kuogopa kutoka madarakani kwa mijizi ya CCM, mwanao January alinukuliwa akisema katiba itakuletea ugali? Je siyo ulevi wa madaraka kuwakejeli watanzania huko?

Nyie wahuni tu mlaaniwe kwa kutaka kuiingiza nchi yetu kwenye shida sababu ya uroho wenu wa madaraka
ni muhimu kufahamu bayana kwamba hakuna mahali mihemko, ghadhabu na kujihesabia haki kuliko mwingine inaweza kusaidia kuleta matokeo chanya hata siku moja...

Infact,
kuna mambo ambayo watu wenye dhamana muhimu na majukumu mazito ya umma, kitaifa na kimataifa hawawezi kubabaika na watu waliokosa hekima, busara na uelekeo wa kisiasa tena katika mambo serious ya waTanzania..
Hao ni wakupuuzwa tu..

Zaidi sana,
yapo mambo nchini, ambayo hayana dalili, na kamwe hayawezi kufanyika wala kutokea Tanzania, unless umedanganywa na mganga wako ..

eti kuitoa ccm madarakani 🤣
 
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi :pulpTRAVOLTA:
Wewe ni mmoja kati ya wasiojua katiba ni nini, katiba ndiyo inayosimamia maisha yako ya kila kitu kuanzia asubuhi mpaka asubuhi, yaani haki yako ya kuishi na kupata mahitaji yako yote muhimu ya kila siku. Ndani ya katiba serikali inalazimika kuhakikisha unapata uongozi bora, maji safi na salama, chakula, elimu, huduma za afya, malazi bora na huduma za mawasiliano yanayokuwezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, vyote hivi vinatekelezwa kutokana na kodi unayolipa serikalini.
HAYA NDIYO MATAKWA YA KATIBA.
 
Back
Top Bottom