Naungana na Dkt. Lwaitama kuhusu Katiba Mpya

Ila la CCM kwenda maporini wakati wa kupiga kura kuwezesha ushindi limeleta sintofahamu kuhusu uchaguzi huru
 
Ila la CCM kwenda maporini wakati wa kupiga kura kuwezesha ushindi limeleta sintofahamu kuhusu uchaguzi huru
mambo ya kushangaza ndio kama haya sasa kwenye siasa za Tanzania,

badala ya kuzingatia mambo muhimu na ya maana, unasifu na kushabikia mambo ya hovyo hovyo, kwamba huo ndio uzalendo, khaaaa...

huo si ni sawa na ushirikina sasa?🐒
 
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi
Mmepewa kazi ya uchawa hata umuhimu wa katiba hamjui ndio maana huwa nawaita mazezeta ya Samia.
 
Naunga mkono, wanasiasa wa CCM wavivu kufikiri. Hivi kazi hawaiwezi
 
CCM hawatakaa wakubali, hawa Jamaa huwa hawapendi Amani
Ccm na katiba mpya ni sawa na nyoka na panya
Si kwamba hawapendi amani, katiba inayoenda kutishia madaraka yao ni dangerous zaid
Hapa wakiona maslahi yao yanaguswa wataipiga vita
Labda CCM ife kwanza, adui wa amani na haki Tanzania na wasiotaka asilani katiba mpya ni CCM.

Umeishawahi kumsikiliza mzee wao wa hovyo wanayependa kumtumia kupotosha kweli kuhusu umuhimu wa katiba Wassira?
CCM kamwe haitakubali
Uzoefu kutoka duniani kote kabisa unaonyesha kwamba Katiba Mpya zilizo nzuri KAMWE hazijawahi kupatikana hivi hivi tu bure bure kwa njia za amani bila ya kuingia gharama kubwa zaidi ya Machozi, Jasho na Damu. Nchi zote kabisa ambazo Leo hii zina Katiba nzuri hapa duniani zimewahi kuingia gharama za namna hiyo, hakuna hata nchi Moja ambayo Wananchi wake wamepata Katiba yao nzuri bila ya kupitia hatua hiyo ngumu, mbaya na ya hatari.

Mifano ya uthibitisho juu ya suala hili ipo mingi Sana karibia kwenye nchi zote kabisa hapa duniani. Mathalani, majirani zetu wa Kenya walipata Katiba yao waliyonayo hivi Sasa (ambayo kwa kiasi kikubwa Sana ina sifa za kuwa Katiba nzuri), waliipata Katiba hiyo baada ya kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2007/2008 baada ya Uchaguzi Mkuu kwenye nchi hiyo. Vita hiyo ndio kiini cha kulazimisha kupatikana kwa Katiba yao waliyonayo hivi Sasa.
 
Mmepewa kazi ya uchawa hata umuhimu wa katiba hamjui ndio maana huwa nawaita mazezeta ya Samia.
katiba iliyoko bado ni nzuri sana Tanzania na ni mfano wa kuigwa Africa, na kama yapo maeneo ya kubadilishwa basi yataboreshwa kadiri itavyoonekana inafaa, lakini sio eti kwasababu ya mihemko na tamaa za vyeo na madaraka ya watu waliofilisika kisiasa na waliokosa dira na uelekeo wa vyama vyao wamesema au wanataka katiba nyingine 🐒
 
Sasa ww unaona wapinzani wa Tanzania wapo serious? Hivi ni kweli kuwa, wao wanaonewa tu? Hakuna mazuri ya CCM? Hata tukileta katiba mpya pia, wapinzani watapata effect. Mfano, vyama vyao ni vya watu binafsi. Pia vina viongoz wa kudumu.

Katiba mpya inaweza kututaka tuwe na vyama vya public kama CCM ingawa, nayo imekuwa ya Kikwete. Aidha, mm nafikiri upinzani bado hawajajipanga kabisa. Mfano mwaka 2015 Mbowe kwenda kuchukua mgombea kutoka CCM ambaye pia walishasema ni fisadi. Hakika CDM sio chama cha ukweli.
 
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi
Kua na katiba bora kunaathiri vip hayo mambo kufanyika?.Hizi ni sababu za waliofilisika kifikra.
 
CCM itapandikiza mamluki
 
Kua na katiba bora kunaathiri vip hayo mambo kufanyika?.Hizi ni sababu za waliofilisika kifikra.
Yes,
serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan ipo kazi kushughulika na mahitaji muhimu ya lazima kwa wananchi ya maji, afya, elimu, miundombinu, kilimo, biashara, ufugaji, uvuvi, ulinzi, usalama n.k

hayo mengine si kipaumbele hata kidogo kwa sasa na pengine hata wakati ujao.

Ni muhimu sana kuwapa nafasi wenye dhamana ya uongozi wa nchi wakafanya kazi kwa nafasi wananchi wapate maendeleo 🐒
 
Acha kuleta mifano ambayo haina uhalisia ili tu uteteee ujinga.katiba bora nikwamanufaa ya nchi kwa ujumla.Tena kwa vizazi na vizazi.mambo ya vyama vya siasa ni manufaa kidogo sana ukikinganisha na manufaa mengine.Nchi inahitaji katiba itakayolinda rasilimali na kuweka uwajibikaji. sana.
 
Miaka 60 ya uhuru kuzungumzia hayo kana kwamba ndo tumezaliwa ni aibu.
 
CCM hawatakaa wakubali, hawa Jamaa huwa hawapendi Amani
Tanzania ni kisiwa cha amani Africa

Ni kwasababu tuna uongozi thabiti na serikali imara

We are not peaceful because of upinzani uchwara
 
Miaka 60 ya uhuru kuzungumzia hayo kana kwamba ndo tumezaliwa ni aibu.
sio Uhuru tu, na Muungano pia ambao umeimarika na kushamiri zaidi..

aibu na fedheha iandamane na wale tu, waliokosa kuungwa mkono na wananchi, waliokosa hoja, waliokosa ushawishi, waliokosa mipango mikakati, dira na uelekeo ..

Lakini serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, haiwezi kubabaika nao bali kuongeza juhudi na maarifa ya kuwaletea wanainchi maendeleo endelevu ya kisiasa, kijamii na kiuchmi kwenye maeneo yao kulingana na vipaumbele vya mahitaji yao 🐒
 
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi
SH
 
Kama anayeamuwa uwepo wa katiba mpya ni rais, hilo halitaweza kutokea. İli iweje?

Watu wanaogelea kwenye asali we eti unasemaje?
Mkuu ni kweli wenye asilimia 100 (100%) kwamba haitawezekana kabisa kupata KATIBA MPYA kama mtu wa mwisho kutoa idhini ya kupata katiba hiyo ni Mwenyekiti wa Chama kinacho isimamia Serikali iliyopo madarakani.
 
kwa maoni yangu nadhani suala la katiba sio muhimu kabisa kwa sasa ukilinganisha na yale mahitaj muhimu sana ya wananchi kama vile maji, afya, elimu, kilimo n.k ambayo ni muhimu zaidi
Mkuu, hayo mambo unayoyaona muhimu ndio hasa, kwa sasa yanahitaji KATIBA MPYA ili yaende vizuri kwa wakati tulionao. Aidha, fahamu kuwa siasa ni kila kitu katika maisha ya kawaida na maendeleo ya binadamu.
 
yaelezee basi kwenye hiyo katika mpya unayoitaka ili iwe mpya, sio kuzungumzia urasi tu kitu ambacho kipo taya kwenye katiba ya sasa, huo upya uko wapi sasa?

sasa huo upya uko wapi 🐒
 
Mkuu, umeandika mengi sana para kwa mapara, lakini hakuna cha maana na chenye uhalisia . JITAFAKARI
 
Labda CCM ife kwanza, adui wa amani na haki Tanzania na wasiotaka asilani katiba mpya ni CCM.

Umeishawahi kumsikiliza mzee wao wa hovyo wanayependa kumtumia kupotosha kweli kuhusu umuhimu wa katiba Wassira?
Makamba Snr alisema Katiba Mpya haitaleta ugali mezani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…