comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amesema huko tunapoenda tuweke utaratibu kuwa mtu akichaguliwa kuwa waziri, mtoto wake asome shule za serikali. Amesema hii itasaidia kufanya mawaziri wasimame mitaala na kuunda sera zenye maslahi mapana kwa taifa
Amesema hayo akijadili bajeti ya elimu iliyowasilishwa bungeni na waziri wa Elimu, prof Adolf Mkenda, ambapo ameshauri mitaala isisitize elimu kwa vitendo na sio nadharia pekee, pia lugha ya kufundishia isiwe na mkanganyiko ambapo ameshauri kama ni kiswahili kifundishwe kuanzia la kwanza hadi la tatu. Kuanzia la tano mtoto atumie kiingereza ili asipate shida anapoingia sekondari kama ilivyo hivi sasa kwa wanafunzi waliosoma shule za serikali na waliosoma shule binafsi.