Naungana na Shigongo Mawaziri na Watumishi wote wa serikali watoto wao wasome shule za serikali

Naungana na Shigongo Mawaziri na Watumishi wote wa serikali watoto wao wasome shule za serikali

Haya mawazo tulikuwa tunasema muda mrefu, iwapo kutokuwa na sheria ya kuhakikisha ukiwa kiongozi wa serikali, mtoto wako lazima asome shule za serikali, tungeona huduma bora kwenye shule hizo.
Naunga mkono hoja. Umeongea kitu bora kaka.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Kwanini lazima iwe hivyo? Kila mtu ampeleke mtoto wake anapoweza/anapotaka. Kufanya kazi serikalini sio kosa la kuchaguliana namna ya kutumia hela zako
Hoja kubwa ya mtoa mada mi naiona kuwa siyo kumpangia mtu matumizi ya fedha bali ni kwamba;

1. Kuwaeleza viongozi kwa vitendo namna wanavyo tuhadaa Wananchi kwa kusifia bungeni kuwa elimu inayotolewa na shule za serikali ni nzuri huku watoto wao wakisoma shule tofauti.

2. Watoto wa viongozi wao wanasoma kwa lugha ya kiingereza ambayo Ndiyo serikali huitumia kuwanyima/ kuwaondoa vijana ktk ajira nzuri za serikali/ ninafsi hata uongozi maana taarifa zote muhimu za serikali ikiwa ni pamoja na usaili wa kazi huendeshwa kwa kiingereza huku Wananchi wa kahadaiwa kwa kuambiwa kuwa kiswahili ni lugha tamu, kiuahalisia haitumiki ktk mambo muhimu ya ajira, ofisi na hata soko la ajira kimataifa.

3. Ubaguzi unaendelea kushamiri ktk taifa tena ubaguzi hatari unaogusa nyanja muhimu kijamii, kiuchumi na kisiasa, na hii baadae tutaijutia ingawa tutakuja tumechelewa.

4. Bado hoja inasimama kwa nguvu kuwa kea nini viongozi wote hawataki kuwapeleka watoto wao ktk shule ambazo kila siku majukwaani wanatwambia zimeboreshwa na nzuri?

Kama siyo hadaa kwa Wananchi nini?.

Kwa nini viongozi hawataki lugha ya kiingereza itumike ktk shule za serikali lakini wao wanaotunga sera hawazitumii sera hizo? Kama mpishi anayepika kile asichoweza kila.

Mtoa mada anawarejesha viongozi kwenye ukweli kuliko kuendelea na hadaa kubwa yenye madhara makubwa baadae yanayo tokana na hizi hadaa za viongozi wetu.
 
Iwe kikatiba si kuunga mkono hoja,
Ila tuanze na yeye wakwake wanasoma wap!
 
Miaka ya 2000 mwanzoni ,nadhani sisi ndo tulikuwa wa mwisho kusoma na watoto wa mawaziri
 
Shigongo ana hoja ya msingi. Haiwezekani serikali inawapumbaza wananchi kwa kujifanya inatoa elimu bure, huku elimu yenyewe ikigubikwa na changamoto lukuki, na ambazo serikali imeendelea kuzipotezea!

Wahamasishaji wa hiyo elimu bure yenyewe, wanawakimbizia watoto wao kwenye mashule yenye gharama kubwa! Kama siyo kuchezeana akili huku ni nini!!

Na wao waanze kuwapeleka watoto wao kwenye shule za kata kote nchini kama wana huo ubavu, ili kuonesha mshikamano na pia mfano kwa raia wa kawaida
 
Back
Top Bottom