Desemba 31, mwaka jana Rais John Magufuli akiwa mapumzikoni katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo mkoani Geita aliwapa siku tano viongozi hao kupatana, vinginevyo angetengua uteuzi wao. Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa chanzo cha ugomvi huo ni matumizi mabaya ya fedha...