Nauza bajaj niliyoichukua kwa mkopo, atakayeitaka atatakiwa kurudisha rejesho

Ni kweli.

Kwa sisi tunaofanya mikataba mitaani huwa hesabu inakuja kila siku kumi akiongeza hapo zake mbili ila hizo za kampun huwa wanataka instantly kama wiki wiki siku kumi ni siku kumi hawataki maelezo hapa ndipo mkataba unapomuwia ugumu.

Angepewa fursa ya kusogea siku mbili mbele angeweza akatoboa.
 
Hii si bei ya noah mpya kabisa kwenye karatasi ..!?
 
Ukimaliza miaka 2 bajaji itakuwa umeilipia 14,497,600 (milioni kumi na nne laki nne, elfu tisiini na saba na mia sita)

139,400 kwa wiki zidisha wiki 52 kwa mwaka zidisha miaka 2.

Nadhani sasa umeshagundua kuwa jamaa wamekuingiza cha kike kiasi fulani.
 
Mkuu umempunguzia deni, kwa wile analipa kwa wiki, kwenye mwaka mmoja kuna wiki 52x139400x2 = 14,497,600/=
 
Muache wizi hiyo kazi naifahamu atakama dereva anafanya kazi za kusomba mizigo ya wamama sokoni hiyo pesa ni ngumu kupata
 
Aise pole sana ndio madereva walivyo wengi sio waaminifu wengine wanachinja vifaa wanauza na kama ndio mgeni kwenye biashara ndio wanakuchezea michezo michafu. Wengine wanaweka bond kisa makamari hasa vijana usumbufu unakua ni mwingi.
 
Muache wizi hiyo kazi naifahamu atakama dereva anafanya kazi za kusomba mizigo ya wamama sokoni hiyo pesa ni ngumu kupata
Hahah mkuu mbona umefika mbali kiasi hiki?

Hakuna wizi hiyo kazi ni kazi kama zilivyo kazi nyengine unaajiriwa unamuingizia mwenye kampuni mill 30 kwa mwezi ikifika mwisho wa mwezi anakupa chako 1 mill kama mshahara unabaki unakenua meno na hakuna siku atakurithisha kampuni tofauti na huku unaumia ndani ya muda fulani baada ya hapo unapata maisha,wapo wasomi wameweka vyeti makabatini wanaifanya wanajutia kwanini walikuwa wanajidhalilisha kuzunguka na bahasha za khaki kutafuta kazi za ”ndiyo boss ndiyo boss".

Kila kazi ina principle na codes zake muhimu kuzizingatia hawa Bajaj&bodaboda drives wanapata sana hela tatizo lao sketi haziwapiti mbali.
 
Hapo bado hujaweka 2M (1M aliyoanza nayo Kama cash, 1M nyingine ni ile aliyoifanyia rejesho) Kama nimemuelewa sawa. Jumla ni Kama 14M+ hivi.
Hawa jamaa ni zaidi ya wanyonyaji isee.

Sent from my Nokia 1.4 using JamiiForums mobile app
 
Waswahili wanaita kausha damu.
 
Umekosea kidogo, mwaka una wiki 52 (365/7) kwa wiki 104 jumla inakuja kama 14.5m hivi, mwezi wa wiki 4 kamili ni february tu. Mingine inazidi wiki 4....
 
Hapo bado hujaweka 2M (1M aliyoanza nayo Kama cash, 1M nyingine ni ile aliyoifanyia rejesho) Kama nimemuelewa sawa. Jumla ni Kama 14M+ hivi.
Hawa jamaa ni zaidi ya wanyonyaji isee.

Sent from my Nokia 1.4 using JamiiForums mobile app
Hatari sana... lakini kuna dereva bajaji hapo katoa experience yake mbona kama mambo ni possible kabisa mkuu sema tu utakuwa umenyonywaa parefu na kesho haitabirikii kabisa.
 
Hatari sana... lakini kuna dereva bajaji hapo katoa experience yake mbona kama mambo ni possible kabisa mkuu sema tu utakuwa umenyonywaa parefu na kesho haitabirikii kabisa.
Ila Bajaj zimekuwa nyingi Sana hasa kwenye miji mikubwa kiasi kwamba wameanza kukataa kutoa usajili. Mfano mzuri ni Mbeya.
Japo anaweza kutoboa Ila ni kwa jasho na damu.

Sent from my Nokia 1.4 using JamiiForums mobile app
 
Mikopo yote ya bajaji Ni hivi..Tena wengine unarudisha Hadi milioni 14
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…