Nauza Bata Bukini wenye miezi 8 wakiwa wamepatiwa chanjo zote

Nauza Bata Bukini wenye miezi 8 wakiwa wamepatiwa chanjo zote

Status
Not open for further replies.
Habari
Nauza bata bukini 6 kwa bei ya shillingi million moja (1,000,000). Bata wana umri wa miezi 8 na wana chanjo zote. .

Hawa bata nawajali sana nahakikisha wanakula kabichi na spinach kila siku. Nawanunulia chakula top quality ni wenye afya nzuri sana. Nauza wote sita siuzi mmoja mmoja kama unahitaji nicheki 0714829688. .

NIKO MANZESE SWEETCORNER
Picha huleta ushawishi zaidi kuliko maneno
 
Picha huleta ushawishi zaidi kuliko maneno
Nimeweka mpaka video
Biashara yeyote kuona ni bure hakuna atakayelazimishwa kununua
Anayehitaji anawaona picha hapa au anakuja kuwaona home
 
Bora masikini wa roho kuliko masikini wa akili wa kuuziwa Bata kwa sh 120K wakati Bata dume huku anauzwa sh 15K, hiyo 120K unapata mbuzi watatu na chenji inabaki
Mkuu kama kitu hukifahamu ni bora ukauliza ili upate uelewa utakuja kukusaidia siku ingine huko uendako, kuliko kuendelea kuongea Mambo usiyoyajua kwenye biashara za watu

Kuna Mifugo aina nyingi sana duniani, wengine wanafugwaa Kwa lengo la ufahari tu na sio Kwa ajili ya kuchinja na Kula kama wafanyavyo wengine au ufanyavyo wewe

Hao bata anaouza mleta Uzi ndio bei zake hizo na hapo yeye anauza bei ndogo, maana hao wanauzwa 150-180K na Kwa wanaoujua wala hawashangai, hao sio bata maji unaosema wewe wanauzwa 15-20k

Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua, wakati wewe unataka ukananunue mbuzi mwenzako anaenda kununua bata bukini 150K na hamchinji kumla bali anamfuga kama pambo

wakati wewe unaendelea kummbembeleza Mzee kimaro akuuzie IST yake Kwa 7M kuna mwenzio anaenda kununua Farasi mkubwa Kwa 12M na sio kusema atamchinja au ataingia road trip bali ni fahari ya macho

Wakati wewe unataka uende mnadani ukanunue Ng'ombe kwa 200k ili ukanenepeshe ikifika Christmas umuuze 800k mwenzio anaenda kununua Nyati maji Kwa 3M na hamchinji bali kwake ni furaha tu kuwaona

Wakati wewe unataka kununua kuku wa kienyeji kwa 15k ili ukaongezee vitoweo nyumbani kuna mwenzio ananunua kasuku 800k na hamchinji kumla bali ufahari

Wakati wewe unanunua njiwa local kwa 5k mwingine ananunua njiwa wa kisasa Kwa 2M na hamchinji kumla bali anamtumia kama pambo au ufahari

Wakati wewe unanunua punda 300k ili akusaidie kazi za hapo nyumbani mwingine ananunua Ngamia 4M ili amsaidie kazi lakini pia anaona Raha tu kumiliki

Kwahiyo kwenye haya maisha kuna levels kwenye kila kitu na ukilijua hili huwezi kupata tabu na maisha ya watu maana nawewe unaweza kufika hizo levels siku moja na ukabadiri fikra zako za leo

Kwenye maisha kuna matabaka mengi sana hapa Duniani labda huko mbinguni ndio hatujui, ila Kwa Dunia hii matabaka ni kuanzia kwenye vyakula,mavazi,makazi, matibabu,starehe na vingine vingi

Ukiona wewe kwako hakina maana basi ujue hakipo Kwa ajili yako, punguza ujuaji kwenye vitu usivovijua ili uendelee kujifunza maana dunia imejaa mambo mengi tusiyoyajua

Kwahiyo Kwa sie ambao tunawajua hao bata tunaweza kusema jamaa anauza bei ya kutupa maana 1M Kwa bata bukini 8 hiyo ni zaidi ya bei nzuri kusema ukweli
 
Kwahiyo Kwa sie ambao tunawajua hao bata tunaweza kusema jamaa anauza bei ya kutupa maana 1M Kwa bata bukini 6 hiyo ni zaidi ya bei nzuri kusema ukweli
Mkuu kwa lecture hii sirudii! [emoji120][emoji120]
 
Wana nini cha ziada kuliko hawa bata wetu wengine tunaouziana 15k?
 
Acheni roho za ajabu.

Hakuna aliyelazimishwa kununua. Kama hujawahi kufuga chochote acheni kelele.

Bata nawanunulia chakula na nawagharamia sana, kwani kuna mfugo unaojifuga wenyewe?

Acheni roho mbaya sio jambo la kiungwana hata kidogo
Mtu ameuliza wana kipi cha ziada tofauti na hawa wetu tunaonunua 20k?, badala ya kujibu hoja unaishia kusema unawalisha, kwani hao wengine hawawalishi?
 
Sijaona bata wa 120k hapo. Huu ujinga wa kufuga bata bukini na kuambiwa sijui anauzwa Hadi laki 3, ni uongo mkubwa
Ni kama forever living tu, kila aliyepigwa anatafuta nae wa kumpiga. Utauziwa lakj 2, baada ya muda utagundua ulipigwa na wewe utatafuta wa kumpiga kwa kuwasifia hao bata
Eti ana nyama zaidi ya mbuzi. Acheni ujinga, kwa udogo huo hizo nyama zinakaa wapi? Mnafanya watu kama mazezeta
 
Hawa Bata ni WA urembo, kwenye Bustani za nyumbani. Hakuna aliyesema kuwa ni wakubwa kushinda mbuzi. Na hakuna aliyekulazimisha kufuga. .
Ndugu yangu una chuki na roho mbaya Sana acha hayo mambo. .

Kuna watu wanafuga njiwa, na anauzwa mpaka elfu 15? Je njiwa ana nyama nyingi?

Kuna watu wanafuga mbwa, aisee anakula dona na nyama Kila week. German shepherd wa miezi miwili anauzwa mpaka laki 3. Je analiwa?

Watu wanafuga paka unajua paka anakunywa maziwa na dagaa na bado haliwi. Watu wanafuga kasuku na gharama za kuwalisha ni kubwa, unajua ni shilling ngap just gharama za dawa na kumfuga kasuku?

Nilienda kwa mtoto wa bhakresa kufanya kazi masaki nilikuta ana fish tank Lina samaki ukuta mzima. Na samaki wa mapambo ambao hawakui na hawaliwi. Gharama tu za kuwaoa fish pellets unajua mfuko ni shilling ngap per month?

Kuna watu wanafuga sungura. Sungura anakula mboga Sana na majani. Piga hesabu za kumlisha karoti mpaka awe na umri wa kuliwa. Bei yake elfu 35, je watu wasile sungura?

Hawa Bata ni mifugo Kama mifugo mingine. Ni Bata ambao anatoa vifaranga vitano tu kwa mwaka. Upatikanaji wake ni adimu Sana. Pia ni mifugo ya urembo. Wazuri Sana ukiwa unawafuga kwenye Bustani yako nyumbani. Pia wanaliwa. Pia wanakula Sana majani kushinda vyakula vya kuku vya kawaida. Gharama zake ni kubwa kuwafuga. Hizi ndio sababu ambazo zinapelekea wawe wa gharama. .

Ila kikubwa hujalazimishwa kuwafuga. Sioni sababu ya kupinga jambo ambalo hujalazimishwa. Watu wanapata mishahara wanapenda kula na Malaya bar, au wanakunywa bia na hizi ni starehe zao. Usilazimishe watu waishi Kama wewe. .

Acha roho hiyo ndugu yangu Kila jambo unataka ushindani na Kila jambo unaleta ujuaji. Hawa Bata wanafugwa na wale tu wanafuga Bata Bukini sio kwa ajili yako. Ukishajua Hilo basi sio fani yako. .

Kama nimekukwaza au nimesema jambo likakukera samahani Sana. Ila huu Uzi haukuwa kwa ajili yako huna sababu ya kupost kwenye Kila Uzi Kaa kwenye majukwaa yanayokuhusu. .

Mimi binafsi napenda kufuga samaki, nafuga kuku, Brahma, Bata bukini. Nyumba yangu haina nafasi Ila ingekuwa na nafasi ningefuga hata mifugo mingi tu. Binafsi starehe yangu. Hawa Bata Sijapenda kuwauza nawauza kwa sababu tu, mahali napowafugia nataka nijenge nipangishe. Ningekuwa na sehemu ya kuwaweka nisingeuza. Mungu ni mwema siku zote. .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom