Nawadharau sana Waingereza kwa kuendeleza utawala wa Kifalme

Umalile Nkamu🤣
 
nchi Nyingi zenye Demokrasia ya kweli maendeleo watu ni madogo

1. Nchi za Scandnavia ambazo maendeleo watu ni makubwa wana wafalme, kina Norway, Denmark etc
2. Nchi za Gulf zina wafalme na Masultan
3. mashariki ya Mbali Japan utamkuta Emperor Naruhito

hata nchi ambazo unakuta wananchi wanachagua demokrasia inakuwa kama changa la macho Mfano Democrat na Republican una choice ya wawili tu, chagua left wing ama right wing huna choice ya kufikiria nje ya box.

njoo huku kwetu sasa, fujo pro max.
 
Hapo Chadema hamna Mfalme?
 
jipige kifua mara 3 sema mimi ni MJINGA
 
Eti kamtu Kako nchi ya dunia ya tatu, nchi ambayo hata maji ya bomba shida,bajeti karibu yote ni hela ya msaada kanaita nchi ambayo inawapa sehemu kubwa ya bajeti Yao primitive! Hio nchi primitive iko mbali yenu miaka 1000
 
Uingereza ina kitu kinaitwa Mixed Government (Monarchy, Aristocracy and Democracy). Huu mfumo hauishii kwenye familia ya kifalme peke yake, bali unaenda hata kwenye Bunge lao. Nchini Uingereza mpaka leo hii lina nafasi tisini (90) za wabunge ambao huzirithi kutoka kwa familia zao. Yaani mtu unazaliwa tu tayari una nafasi ya ubinge inakusubiri......

Tena siku hizi wamebadilika, zamani The House Lords (Upper House) ambako wanakaa mabwanyenye walikuwa na uwezo wa kupinga (Power to Veto) miswada na sheria mbalimbali inayotungwa na wabunge ambao wanachaguliwa na raia wa Uingereza (The Commons). Ndiyo maana huwa nawashangaa sana mnavyotamani kuiga hii mifumo ya watu......

NB: Hili la Uingereza halina tofauti sana na kinachoendela kule CHADEMA baina ya Mbowe na Mtei......
 
Madhara ya kunywa maji ya kisima yaliyochanganyika na kinyesi lazima utaongea utumbo
 
Shughulika na ufalme ccm iliyojisimikia Tanzania, ya Uingereza waachie wenyewe hutayaelewa.
 
Mimi nadhani ni mfumo mzuri kwa kuwa wananchi wa uingereza wenyewe wameuridhia na unawapa kile ambacho wanakitaka.....
Wanafalsafa wakubwa duniani kama Socrates, Plato na Marcus Aurelius walikuwa wanaamini kwamba huu mfumo wa Mixed Government (Monarchy, Aristocracy and Democracy) ndiyo njia sahihi kabisa ya kuongoza nchi. Hii ya kuruhusu kila mtu tu anayejua kuongea kuwa kiongozi kwasababu tu watu wengi wanamtaka huleta sana shida kwenye mataifa mengi.

Unakuta hata wale wajinga na maarufu (Demagogues) wanateuliwa na kushika nyadhifa za nchi, ilhali tunafahamu fika kwamba hawana uwezo wala maadili ya kuwa viongozi wa ummah. Hata Marekani kwenyewe hawaruhusu Demokrasia ambayo wanaharakati wetu wanaihubiri.....
 
Kwamba fujo pro max, Wazungu walituharibia utawala wetu wa kitemi huo ndio ulikuwa sahihi sana lkn hii Demokrasia ya vyama vingi ni uongo tu na fujo
 
Unashauri ili sisi tuwe vizuri tufuate mfumo upi mzee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…