Nawadharau sana Waingereza kwa kuendeleza utawala wa Kifalme

Nawadharau sana Waingereza kwa kuendeleza utawala wa Kifalme

Eti kamtu Kako nchi ya dunia ya tatu, nchi ambayo hata maji ya bomba shida,bajeti karibu yote ni hela ya msaada kanaita nchi ambayo inawapa sehemu kubwa ya bajeti Yao primitive! Hio nchi primitive iko mbali yenu miaka 1000
jikiteni kwenye hoja yake
 
Wanafalsafa wakubwa duniani kama Socrates, Plato na Marcus Aurelius walikuwa wanaamini kwamba huu mfumo wa Mixed Government (Monarchy, Aristocracy and Democracy) ndiyo njia sahihi kabisa ya kuongoza nchi. Hii ya kuruhusu kila mtu tu anayejua kuongea kuwa kiongozi kwasababu tu watu wengi wanamtaka huleta sana shida kwenye mataifa mengi.

Unakuta hata wale wajinga na maarufu (Demagogues) wanateuliwa na kushika nyadhifa za nchi, ilhali tunafahamu fika kwamba hawana uwezo wala maadili ya kuwa viongozi wa ummah. Hata Marekani kwenyewe hawaruhusu Demokrasia ambayo wanaharakati wetu wanaihubiri.....
Kweli kabisa ndugu.....kwa kifupi akiachwa sana huru baada ya kustawi anaangamia....waliolijua hilo mapema ndio hawa wanapandikiza demokrasia kwenye mataifa masikini huku wao wenyewe demokrasia yao ikiwa mdomono tu.......
 
Unashauri ili sisi tuwe vizuri tufuate mfumo upi mzee?
Kiuhalisia nchi yetu bado ni changa sana kufuata demokrasia kamilifu na haiwezi kustawi......ukifuatilia historia ya Dunia unagundua kuwa mataifa mengi makubwa wakati yanapigania ustawi wa mataifa yao hawakuwa na demokrasia kwa kuwa wakati mwingine kufuata maoni ya wengi ni kuelekea kwenye kuangamia......

Changamoto yetu sisi huku nchi za Africa wale tuliowaamini tukawapa uongozi wamefunikwa na shuka la ubinafsi na wamevaa miwano ya roho mbaya........
 
Unashauri ili sisi tuwe vizuri tufuate mfumo upi mzee?
Mfumo wowote uimara wa kiutawala ni lazima uzingatie taasisi asilia (Local & Social Institutions) ambazo zimejengeka kwa muda mrefu ndani ya taifa husika. Hili la kuchukua na kuiga kila kitu kutoka mataifa ya nje ndilo linayagharimu mataifa mengi sana duniani. Jambo linaweza likawa zuri na likafanya kazi nchini Uingereza lakini lisiwe zuri nchini Tanzania. Ndiyo maana tunategemea wasomi wetu wa Tanzania wawe "Empiricists" huku wakiuliza swali hili kabla ya kufanya chochote kile "Will it work ??" and "And Why should it work ??"

Ukisoma historia ya katiba ya Marekani (Constitutional History of the United States) utafahamu kwamba waliiga mambo mengi sana kutoka nchini Uingereza. Kuanzia mgawanyo wa madaraka (Separation of Powers), mfumo wa sheria na utoaji haki (Legal System/The Common Law System) na mfumo wa haki za binadamu (Bill of Rights) lakini kuna mambo mengi hawakuiga. Wao badala ya kuweka Mfalme kama baadhi walivyotaka wenyewe wakaweka Raisi anayeteuliwa. Badala ya kuwa na dini ya taifa kama Uingereza (State Religion) wakina Thomas Jefferson wakaingia maktaba na kutafuta mfumo ambao ungelifaa taifa la Marekani.

Thomas Jefferson ndiyo aliyewashauri Wamarekani waachane na kuiga mifumo ya Ulaya na kuanza kusema Marekani ni taifa la kikristo. Hili alilifanyia majaribio alivyokuwa anaandika katika ya jimboni kwake Virginia. Kama wangeiga, hili la dini lingewavuruga kabisa. Jefferson akaamua kuiga mfumo wa Sheria wa Mongolia (The Ikh Yasa) uliotungwa na Tamujin a.k.a Ghengis Khan miaka zaidi ya 700 iliyopita. Ndiyo ukaona Marekani likawa ndiyo taifa la kwanza kabisa la Magharibi kuruhusu uhuru wa kuabudu (Freedom of Religion), kitu ambacho kiliwahi kufanywa na taifa la Mongolia peke yake.

Jefferson akaenda mbali zaidi na kuanzisha THE ELECTORAL COLLEGE ili kuhakikisha serikali haishikiliwi na wajinga wajinga tu (Demagogues). Eti kila mtu ambaye ni maarufu basi tumpe nchi kisa kapata kura nyingi. Hili limesaidia sana nchini Marekani kuwafunga spidi gavana baadhi ya watu. Sasa huku Tanzania utasikia mara, tuige Uingereza, tuige Marekani, tuige Singapore, na tuige hadi Kenya (Yaani Kenya ni ya kuigwa kweli ???), bila kujiuliza swali la msingi kabisa "Will it work here ???"

Sasa mlianza na Ujamaa, mkalimbikiza nguvu zote za dola kwa mtu moja (Raisi Mfalme/Imperial Presidency). Hili likawashinda vibaya na mpaka leo hii mnaisoma namba na mnataka Raisi apunguziwe madaraka. Lakini, kule Marekani Raisi Mfalme (Imperial Presidency) imefanikiwa vizuri sana kwasababu wana BUNGE na MAHAKAMA Imara, pia raia wengi wa Marekani ni watu wenye uelewa mpana wa mambo tofauti na Tanzania ambako vyama vinawaamulia raia kitu.

Mambo, kama haya ndiyo mnatakiwa wasomi myaangalie. Mimi sitawaambia ni mfumo upi unafaa kwa Tanzania, nilichofanya ni kutoa mwongozo tu. CHADEMA wanataka sera ya majimbo, tena wanataka na serikali tatu na wameigeuza hii kama ndiyo ajenda ya watanzania wote (Well and good. But will it work ??). Kule Marekani majimbo yalifanikiwa kwasababu zile zilikuwa ni nchi huru, huku mnataka majimbo yawe kimikoa na kikanda ambako bahati mbaya sana kila mkoa hukaliwa na kabila fulani.

CCM wanataka Chama kushika hatamu (Party Supremacy) na kulimbikiza madaraka (Centralization) kama kule Uchina, lakini bahati mbaya sana hawana mfumo imara wa Serikali za Mitaa ( Local Government) ambao ndiyo chombo muhimu kinachofanya kazi kuhakikisha wananchi wa kawaida na viongozi wa huku chini wanafanya kazi moja kwa moja na Serikali Kuu (Central Government). Serikali za mitaa za Uchina zina nguvu kubwa mnoo na ziko huru (Autonomous) , ndiyo maana mfumo wao unafanikiwa. Sisi Tanzania kuna kipindi Mzee Nyerere aliamka amevurugwa tu akaamua kufuta serikali za mitaa. Baada ya muda yakamshinda akaamua kuzirudisha.

Raisi Magufuli naye akaamua kuzinyang'anya serikaliza mtaa mapato yake na kuyapeleka serikali kuu. Hapa unadhani serikali zitajiendeshaje ilhali mapato yake yote yanaenda hazina ???

Lakini, mbaya zaidi taasisi asilia (Local Chieftainship) ambazo ndiyo ziko jirani na watu zilufutwa na Mzee Nyerere ili kujenga Ujamaa. Nadhani hili halikuangaliwa kwa undani na mapana yake zaidi. Nasema hivi kwasababu Kama taasisi za kikabila ni kitu kibaya kwanini basi ubakize sheria za kikabila (Customary Laws) ambazo zinafanya kazi na kutumika mpaka leo hii ??? Kingine ni kwamba wanaotatua kesi za kikabila ni wasomi (Judges/Magistrates) wasio na ujuzi wowote ule kuhusu watu wa jamii husika, mbali na kusaidiwa na wazee wa baraza ambao hawana nguvu yoyote ile......

NB 1: Tukikata kutoka hapa ni lazima kwanza tuifahamu Tanzania hii vizuri na jamii yake, siyo kuiga-iga kila kitu tunachosoma darasani au kuoana kwenye televisheni, halafu tunataka kutengeneza A CARBON COPY OF FOREIGN MODELS. Mimi nawakubali sana wapinzani, lakini kuna wakati ukiwasikiliza wanaharakati wao unabaki tu mdomo wazi. Haya angalia kali ya leo aliyotuletea ndugu Salary Slip....

NB 2: Hivi unafahamu kwanini IRAN mbali na matatizo yao wanafanikiwa kuliko nchi nyingi za kiislamu ??? Ni kwasababu, tofauti na falme nyingine na mataifa mengine ya kiislamu, waajemi wametengeneza serikali mchanganyiko (A Mixed Government) ambayo inazingatia tamaduni za waajemi ambazo zimedumu kwa miaka zaidi ya 6000. Wamechanganya (Theocracy, Democracy and Aristocracy ). Tofauti na Saudi Arabia, Qatar au U.A.E ambako ni aidha utii SHARIA LAW au upigwe JAMBIA, Iran wameweza kuweka uwaiano mzuri biana ya sheria za dini na zile za kiraia.

Nchi kama hii ambayo kila mtu ana sehemu yake ni ngumu kuifanyia uzandiki (Subversion) na hujuma (Sabotage) za kisiasa. Khomeini kafa lakini nchi inadunda tu......Sisemi kwamba huu ndiyo mfumo sahihi (Ideal Model), lakini walau umeonyesha kufanya kazi kuliko mataifa mengine kama yetu ambapo Raisi akifa tu, anakuja mwingine na mambo yake. Mwishowe nchi inajaa vurugu na hakuna kinachoendelea. Hebu angalia kinachoendelea saa hizi hapa nchini.....​
 
Very poor timing ya hiki ulichoandika hapa, expect the backlash hata kama una hoja.
 
Naunga mkono hoja. Yaani eti kuna familia haifanyi kaI yoyote inaabudiwa na kulindwa na waingereza wote. Bure kabisa hwa watu
Kuna kitu hukijui, siyo kosa lako, hao hiyo familia siyo binadamu wa kawaida, ukitaka kuelewa utawaelewa, wazungu si wajinga kama unavyodhani kila siku wanabadirisha vyama vya kuwaongoza lakini hiyo familia haiguswi, jiulize mwenyewe swali hili kwanza ndio utajuwa wewe ni bure kabisa.

Vatican imewashindwa hawa Kwa hiyo kaa kitako kwa kutulia, huna unalolijuwa.
 
Bajeti ya kutunza hiyo familia miak nenda miaka rudi inabebwa na nani kama sio walipa kodi wa Uingereza?
Wananchi wenyewe wanapenda hivyo na ikitokea mwanasiasa kuanza kuziaki huo ufalme atashambuliwa na wananchi wenzake kuliko unavyofikiria, haina tofauti sana kama tz spika achane hotuba ya rais mbele yake nafikiri panaweza kuchimbika lkn kwa Marekani hilo ni jambo dogo sana.
 
Uko sahihi
Utawala wa kifalme uingereza hauna athari yoyote as long as democrasia yao ipo imara. Kiongozi wa kifalme ni ceremonial leader, hana mamlaka yoyote ya kiutendaji.
 
Huelewei hata demokrasia ni nini ndio maana unaamini Uingereza, Scandinavian na US hakuna demokrasia ila bongo ndio kuna demokrasia ya kweli.
Poor.
nchi Nyingi zenye Demokrasia ya kweli maendeleo watu ni madogo

1. Nchi za Scandnavia ambazo maendeleo watu ni makubwa wana wafalme, kina Norway, Denmark etc
2. Nchi za Gulf zina wafalme na Masultan
3. mashariki ya Mbali Japan utamkuta Emperor Naruhito

hata nchi ambazo unakuta wananchi wanachagua demokrasia inakuwa kama changa la macho Mfano Democrat na Republican una choice ya wawili tu, chagua left wing ama right wing huna choice ya kufikiria nje ya box.

njoo huku kwetu sasa, fujo pro max.
 
Poor Malcom
House of Lords imebaki kama pambo tu, hata mishahara hawalipwi katika hilo bunge.
Uingereza ina kitu kinaitwa Mixed Government (Monarchy, Aristocracy and Democracy). Huu mfumo hauishii kwenye familia ya kifalme peke yake, bali unaenda hata kwenye Bunge lao. Nchini Uingereza mpaka leo hii lina nafasi tisini (90) za wabunge ambao huzirithi kutoka kwa familia zao. Yaani mtu unazaliwa tu tayari una nafasi ya ubinge inakusubiri......

Tena siku hizi wamebadilika, zamani The House Lords (Upper House) ambako wanakaa mabwanyenye walikuwa na uwezo wa kupinga (Power to Veto) miswada na sheria mbalimbali inayotungwa na wabunge ambao wanachaguliwa na raia wa Uingereza (The Commons). Ndiyo maana huwa nawashangaa sana mnavyotamani kuiga hii mifumo ya watu......

NB: Hili la Uingereza halina tofauti sana na kinachoendela kule CHADEMA baina ya Mbowe na Mtei......
 
Wanafalsafa wakubwa duniani kama Socrates, Plato na Marcus Aurelius walikuwa wanaamini kwamba huu mfumo wa Mixed Government (Monarchy, Aristocracy and Democracy) ndiyo njia sahihi kabisa ya kuongoza nchi. Hii ya kuruhusu kila mtu tu anayejua kuongea kuwa kiongozi kwasababu tu watu wengi wanamtaka huleta sana shida kwenye mataifa mengi.

Unakuta hata wale wajinga na maarufu (Demagogues) wanateuliwa na kushika nyadhifa za nchi, ilhali tunafahamu fika kwamba hawana uwezo wala maadili ya kuwa viongozi wa ummah. Hata Marekani kwenyewe hawaruhusu Demokrasia ambayo wanaharakati wetu wanaihubiri.....
Poor Malcom, US ni demokrasia ya kweli na mojawapo ya kale zaidi "katika modern world"
 
Kwa sababu ufalme ni sehemu ya historia iliyoifanya nchi yao kuwa mojwapo ya himaya kubwa zaidi duniani kwa kipindi kirefu cha historia ya dunia.
Maisha yao yanagharamiwa na serikali kwa sababu gani ?
 
Sasa mbona hatujawahi kufuata hata hiyo demokrasia kamilifu na bado tuko nyuma sana tu kimaendeleo??!
Kiuhalisia nchi yetu bado ni changa sana kufuata demokrasia kamilifu na haiwezi kustawi......ukifuatilia historia ya Dunia unagundua kuwa mataifa mengi makubwa wakati yanapigania ustawi wa mataifa yao hawakuwa na demokrasia kwa kuwa wakati mwingine kufuata maoni ya wengi ni kuelekea kwenye kuangamia......

Changamoto yetu sisi huku nchi za Africa wale tuliowaamini tukawapa uongozi wamefunikwa na shuka la ubinafsi na wamevaa miwano ya roho mbaya........
 
Back
Top Bottom