Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Uongo mkubwa ulioandika kwa unadhifu sana
1. Ufalme hakuwahi kuja au kuwepo sehemu kwa watu kuuchagua. Ufalme ulikuwa unaibuka na kujisimika kwa vita, nguvu na kumwaga damu. Hakuna mahali jamii ilichagua kuwa na wafalme dunia hii. Ni ujuha kusema Jafferson aliwaambia Wamarekani wasiige kuwa na ufalme kama Ulaya. Kwanza vita vya uhuru vya Marekani vyenyewe vilikuwa ni kuondokana na Ufalme.
1. Ufalme hakuwahi kuja au kuwepo sehemu kwa watu kuuchagua. Ufalme ulikuwa unaibuka na kujisimika kwa vita, nguvu na kumwaga damu. Hakuna mahali jamii ilichagua kuwa na wafalme dunia hii. Ni ujuha kusema Jafferson aliwaambia Wamarekani wasiige kuwa na ufalme kama Ulaya. Kwanza vita vya uhuru vya Marekani vyenyewe vilikuwa ni kuondokana na Ufalme.
Mfumo wowote uimara wa kiutawala ni lazima uzingatie taasisi asilia (Social Institutions) ambazo zimejengeka kwa muda mrefu ndani ya taifa husika. Hili la kuchukua na kuiga kila kitu kutoka mataifa ya nje ndilo linayagharimu mataifa mengi sana duniani. Jambo linaweza likawa zuri na likafanya kazi nchini Uingereza lakini lisiwe zuri nchini Tanzania. Ndiyo maana tunategemea wasomi wetu wa Tanzania wawe "Empiricists" huku wakiuliza swali hili kabla ya kufanya chochote kile "Will it work ??" and "And Why should it work ??"
Ukisoma historia ya katiba ya Marekani (Constitutional History of the United States) utafahamu kwamba waliiga mambo mengi sana kutoka nchini Uingereza. Kuanzia mgawanyo wa madaraka (Separation of Powers), mfumo wa sheria na utoaji haki (Legal System/The Common Law System) na mfumo wa haki za binadamu (Bill of Rights) lakini kuna mambo mengi hawakuiga. Wao badala ya kuweka Mfalme kama baadhi walivyotaka wenyewe wakaweka Raisi anayeteuliwa. Badala ya kuwa na dini ya taifa kama Uingereza (State Religion) wakina Thomas Jefferson wakaingia maktaba na kutafuta mfumo ambao ungelifaa taifa la Marekani.
Thomas Jefferson ndiyo aliyewashauri Wamarekani waachane na kuiga mifumo ya Ulaya na kuanza kusema Marekani ni taifa la kikristo. Hili alilifanyia majaribio alivyokuwa anaandika katika ya jimboni kwake Virginia. Kama wangeiga, hili lingewavuruga kabisa. Jefferson akaamua kuiga mfumo wa Sheria wa Mongolia (The Ikh Yasa) uliotungwa na Tamujin a.k.a Ghengis Khan miaka zaidi ya 700 iliyopita. Ndiyo ukaona Marekani likawa ndiyo taifa la kwanza kabisa la Magharibi kuruhusu uhuru wa kuabudu (Freedom of Religion), kitu ambacho kiliwahi kufanywa na taifa la Mongolia peke yake.
Jefferson akaenda mbali zaidi na kuanzisha THE ELECTORAL COLLEGE ili kuhakikisha serikali haishikiliwi na wajinga wajinga tu (Demagogues). Eti kila mtu ambaye ni maarufu basi tumpe nchi kisa kapata kura nyingi. Hili limesaidia sana nchini Marekani kuwafunga spidi gavana baadhi ya watu. Sasa huku Tanzania utasikia mara, tuige Uingereza, tuige Marekani, tuinge Singapore, na tuige hadi Kenya (Yaani Kenya ni ya kuigwa kweli ???), bila kujiuliza swali la msingi kabisa "Will it work here ???"
Sasa mlianza na Ujamaa, mkalimbikiza nguvu zote za dola kwa mtu moja (Raisi Mfalme/Imperial Presidency). Hili likawashinda vibaya na mpaka leo hii mnaisoma namba na mnataka Raisi apunguziwe madaraka. Lakini, kule Marekani Raisi Mfalme (Imperial Presidency) imefanikiwa vizuri sana kwasababu wana BUNGE na MAHAKAMA Imara, pia raia wengi wa Marekani ni watu wenye uelewa mpana wa mambo tofauti na Tanzania ambako vyama vinawaamulia raia kitu.
Sasa, hili ndilo mnatakiwa wasomi mliangalie. Mimi sitawaambia ni mfumo upi unafaa kwa Tanzania, nilichofanya ni kutoa mwongozo tu. CHADEMA wanataka sera ya majimbo, tena wanataka na serikali tatu na wameigeuza hii kama ndiyo ajenda ya watanzania wote (Well and good. But will it work ??). Kule Marekani majimbo yalifanikiwa kwasababu zile zilikuwa ni nchi huru, huku mnataka majimbo yawe kimikoa na kikanda ambako bahati mbaya sana kila mkoa hukaliwa na kabila fulani.
CCM wanataka Chama kushika hatamu (Party Supremacy) na kulimbikiza madaraka (Centralization) kama kule Uchina, lakini bahati mbaya sana hawana mfumo imara wa Serikali za Mitaa ( Local Government) ambao ndiyo chombo muhimu kinachofanya kazi kuhakikisha wananchi wa kawaida na viongozi wa huku chini wanafanya kazi moja kwa moja na Serikali Kuu (Central Government). Serikali za mitaa za Uchina zina nguvu kubwa mnoo na ziko huru (Autonomous) , ndiyo maana mfumo wao unafanikiwa. Sisi Tanzania kuna kipindi Mzee Nyerere aliamka amevurugwa tu akaamua kufuta serikali za mitaa. Baada ya muda yakamshinda akaamua kuzirudisha.
NB 1: Tukikata kutoka hapa ni lazima kwanza tuifahamu Tanzania hii vizuri na jamii yake, siyo kuiga-iga kila kitu tunachosoma darasani au kuoana kwenye televisheni, halafu tunataka kutengeneza A CARBON COPY OF FOREIGN MODELS. Mimi nawakubali sana wapinzani, lakini kuna wakati ukiwasikiliza wanaharakati wao unabaki tu mdomo wazi. Haya angalia kali ya leo aliyotuletea ndugu Salary Slip....
NB 2: Hivi unafahamu kwanini IRAN mbali na matatizo yao wanafanikiwa kuliko nchi nyingi za kiislamu ??? Ni kwasababu, tofauti na falme nyingine na mataifa mengine ya kiislamu, waajemi wametengeneza serikali mchanganyiko (A Mixed Government) ambayo inazingatia tamaduni za waajemi ambazo zimedumu kwa miaka zaidi ya 6000. Wamechanganya (Theocracy, Democracy and Aristocracy ). Tofauti na Saudi Arabia, Qatar au U.A.E ambako ni aidha utii SHARIA LAW au upigwe JAMBIA, Iran wameweza kuweka uwaiano mzuri biana ya sheria za dini na zile za kiraia.
Nchi kama hii ambayo kila mtu ana sehemu yake ni ngumu kuifanyia uzandiki (Subversion) na hujuma (Sabotage) za kisiasa. Khomeini kafa lakini nchi inadunda tu......Sisemi kwamba huu ndiyo mfumo sahihi (Ideal Model), lakini walau umeonyesha kufanya kazi kuliko mataifa mengine kama yetu ambapo Raisi akifa tu, anakuja mwingine na mambo yake. Mwishowe nchi inajaa vurugu na hakuna kinachoendelea. Hebu angalia kinachoendelea saa hizi hapa nchini.....