Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Mnao miaka kadhaa nikiwa darasa la sita...nilipigwa kipigo cha Mbwa koko baada ya Mwalimu kunichanganya na mchelewaji maarufu wa shule.

Alipokuja kugundua sio mimi ilikuwa imeshapita..fimbo na mateke yaliniweka chini.Wanafunzi wenzangu walipiga kelele.

Toka hiyo siku shule nikawa nachelewa na kuja nilovyojisikia mpaka nilipo maliza.

Ilikuwaje,nilimfuata Mwalimu kwa wakati tofauti ambao yeye hakutegemea wakiwa ofisini na wenzake.
Nikamweleza mbele ya wenzake kuwa ulichofanya ni kitu kibaya sana na familia yangu ita deal na wewe taratibu.
Aisee ni kisa kirefu sana....alikuja kuwa rafiki yangu sana.
 
View attachment 3266333

Hii picha sio ya kuigiza. Ni picha halisi ilipigwa na camera ya simu ambayo haikuwa na spidi sana ndio maana unaona kuna sehemu za picha ziko out of focus, kuonyesha zilikuwa zina movement ya kasi zaidi spidi ya camera ya simu.

Na picha inajieleza. Hasira za mwalimu, maumivu ya mwanafunzi na shock usoni mwa wanafunzi wanaotazama tukio hili.

Sasa niambieni. Nipate picha au video clip kama hii na huyo hapo anaesulubiwa awe ni mwanangu, mnafikiri nitamfanya nini huyo mwalimu, kumpeleka kwa polisi wetu hawa ambao wengi ni wala rushwa? Ni kosa gani ambalo huyu mwanafunzi anaweza kuwa amefanya kiasi mwalimu amwadhibu kwa ghadhabu na ukatili namna hii - amembaka mama yake?

Walimu wenye tabia hii chukueni tahadhali. Mtaja kutana na watu ambao akili zao zitakuwa kama zenu, na hamtashinda.

Haya mambo ya kuchapana tulijifundisha kutoka kwa wazungu.
Inasikitisha sana

48C9605800000578-5339177-image-a-2_1517481064812.jpg
 
Hata vitu vidogo kama miongozo mbalimbali ya elimu unataka mwanasheria aje akusomee ndiyo uelewe?

Hata Mkuu wa shule/Mwalimu mkuu hana mamlaka ya kumuadhibu mtoto hovyo kama inavyoonekana hapo isipokuwa kwa utaratibu mgumu hasa.

Binafsi kama mtetezi wa haki za watoto na binadamu kwa ujumla nimesababisha walimu kadhaa kufutwa kazi, kuandikishwa barua rasmi za onyo na wengine kesi zao zipo mahakamani kutokana na ukatili dhidi ya watoto.

Wewe zungumza tu hivyo kwakuwa zamu yako bado haijakufikia lakini siku likikufika hutopata muda wa kuongea mashudu kama haya.

Sijawahi kuwa kucheka na walimu wapumbavu kama wewe badala yake kila shule ninayopita hakuna mwalimu anayeleta ujinga dhidi ya watoto.
Wewe ni famba yaan mwalimu afutwe kazi akimuonya mtoto mpumbavu ..? Mtoto asie na maadili wala asiefundishika. Kuna watoto hata wakipigwa na kupewa ng'eu ni kidgo ukilinganisha na matendo yao..
 
Nimesoma pahala hapa JF kuna Mwalimu wa shule ya muhimbili miaka ya nyuma aliyekuwa akichapa fimbo kwa spidi ya cherehani. Sikuamini, ila nina anko wangu aliyesomea nyakati hizo shule ya Tambaza iliyokuwa jirani pia aliwahi kunihadithia.
Chakushangaza, ndipo wazazi walikuwa wakipenda kuwasomesha watoto zao hapo, na baadhi ya watoto hao ni viongozi katika nafasi mbalimbali serikalini na taasisi kubwa tu nchini.

Cjui shida ni nini? Watoto wamekuwa na viburi na wakorofi ama walimu ndo hivo
 
View attachment 3266333

Hii picha sio ya kuigiza. Ni picha halisi ilipigwa na camera ya simu ambayo haikuwa na spidi sana ndio maana unaona kuna sehemu za picha ziko out of focus, kuonyesha zilikuwa zina movement ya kasi zaidi spidi ya camera ya simu.

Na picha inajieleza. Hasira za mwalimu, maumivu ya mwanafunzi na shock usoni mwa wanafunzi wanaotazama tukio hili.

Sasa niambieni. Nipate picha au video clip kama hii na huyo hapo anaesulubiwa awe ni mwanangu, mnafikiri nitamfanya nini huyo mwalimu, kumpeleka kwa polisi wetu hawa ambao wengi ni wala rushwa? Ni kosa gani ambalo huyu mwanafunzi anaweza kuwa amefanya kiasi mwalimu amwadhibu kwa ghadhabu na ukatili namna hii - amembaka mama yake?

Walimu wenye tabia hii chukueni tahadhali. Mtaja kutana na watu ambao akili zao zitakuwa kama zenu, na hamtashinda.
Ndo umetuliza akili ukaja na post kama hii!!!!! ......... Hawaishi duniani.
 
Jamani, uchapaji gani huu? 😭😭
Utafikiri sio binadamu.

Hii sijui ni shule gani?
 
Huyo mwalimu ana msongo tu wa mawazo,Walimu saizi hawana mda na mambo ya bakora yalishapitwa na wakati,
Walimu saizi wanachapa mkia binti za shule siyo bakora,kama sivyo bas wapo busy kutafuta pesa mtaani muda wa vipindi
 
Mnao miaka kadhaa nikiwa darasa la sita...nilipigwa kipigo cha Mbwa koko baada ya Mwalimu kunichanganya na mchelewaji maarufu wa shule.

Alipokuja kugundua sio mimi ilikuwa imeshapita..fimbo na mateke yaliniweka chini.Wanafunzi wenzangu walipiga kelele.

Toka hiyo siku shule nikawa nachelewa na kuja nilovyojisikia mpaka nilipo maliza.

Ilikuwaje,nilimfuata Mwalimu kwa wakati tofauti ambao yeye hakutegemea wakiwa ofisini na wenzake.
Nikamweleza mbele ya wenzake kuwa ulichofanya ni kitu kibaya sana na familia yangu ita deal na wewe taratibu.
Aisee ni kisa kirefu sana....alikuja kuwa rafiki yangu sana.
Ulimtishia watamloga? Ukiwa unatoka Sumbawanga that works! Mwambie tutakuweka mbususu kwenye paji la uso hakugusi tena hata ufanye nini!
 
Mimi kama mwalimu ukiniletea ushenzi wako tunamalizana kama unavyotaka. Huwa nawataka sana wazazi wapuuzi kama wewe waje shuleni tumalizane. Kama vipi chukua toto lako kalifundishe mwenye nyumbani kwako, sipendagi ujinga
Hawa wajinga ndio wanasababisha watoto wao kuwa machoko....mwalimu hawezi kuwa mpuuzi ampige mwanafunzi kiasi hicho halafu hizo adhabu ni zakawaida tu,,,niliwahi kuzingua nyumbani mama akanikata kisu mkononi na mpaka leo nina hilo kovu ila yote kwa yote lengo lilikuwa ni kurejesha nidhamu
 
Unataka kusema nini yaani? Kwa kipindi chake ulitarajia asome kozi gani nyepesi zaidi ya ualimu?

Hiyo ndiyo kozi pekee ambayo binadamu yeyote anaweza kusoma na usipate Supplementary wala discontinuation hadi unahitimu.
Nini maana ya mwalimu? Namaanisha mwalimu ni nani?
 
Kuchapwa ndiyo njia pekee ya mtoto kuelewa?

Hakika watumwa ni wengi barani Afrika.

Mimi sijawahi kumchapa mtoto wangu lakini nikimuelekeza jambo analifanya kwa haraka kwasababu nimemlea kama rafiki nazungumza naye namna nzuri ya kuishi na wazazi pamoja na jamii kwa ujumla.

Lakini hali ni tofauti kwa watoto wa majirani maana wazazi wao ni aina yako wanaoamini kwenye kuchapa. Wamekuwa wakiwachapa lakini ndiyo kwanza watoto wamekuwa sugu.

Kilichomsababisha achapwe jana anakirudia leo kitu kile kile.

Kama wewe ni mwalimu mfanye mwanafunzi awe rafiki atakusikiliza kwa umakini na kwa upendo mkubwa na hata kuelewa darasani anakuelewa vizuri zaidi kuliko mwalimu chapa chapa ambaye anachukiwa na watoto.

Halikadhalika ukiwa mzazi mfanye mtoto awe rafiki uta enjoy maisha maana hatokuficha kitu chochote kiwe kibaya ama kizuri.
Wewe dogo hauna familia ila unaleta stor za kusadikika...kwasababu sisi tulio na familia hatuwi na mawazo kuku kama yako
 
Basi inawezekana kufanya hivyo kwa watoto pia. Shuleni tukifanya kosa kubwa tulikuwa tunakuwa suspended mwezi mmoja
ndio nilichoandika hapo juu aina hiyo ya adhabu ni kumtoa mtoto darasani aende kwao akamlete mzazi wake kuliko kumbamiza akafa bure
 
Mkuu, ndio maana basi alikuwa anawapa kichapo sana watoto wake wasipofanya vizuri darasani. Sasa walimu kama Magufuli hawatakiwi kabisa, wana mental issues. Si unaona mentality ya "kuchapa watu bila huruma" aliileta hadi kwenye uraisi? Akamchapa na Ben Saanane. Anaweza kuwa alifanya vizuri katika baadhi ya sehemu,lakini kwenye hili la kuchapa alikuwa na tatizo la afya ya akili
Eti nawewe ni platinum member
 
Uliwahi kuona wapi mtu aliyekuwa kipanga wa darasa akawa mwalimu?

Walimu ni watu waliokosa alama za kutosha kwenda kusoma kozi za maana na zenye uzito ndiyo wakaangukia ualimu.

Mkuu hujawahi kusikia mtaani watu wakisema mtoto fulani amefeli hivyo hawezi kusoma kozi zingine labda aende ualimu?

Ualimu ndiyo kazi ambayo hata mtu awe kilaz,a anasoma maana ni kozi ya watu wasio na mwelekeo wa kimaisha hata watoto wanajua hivyo.

Yaani unakuta mwalimu kawapa mtihani watoto lakini hata majibu ya mtihani wenyewe mwalimu na mwanafunzi wote hawajui hadi mtoto akikuletea karatasi zake za mtihani ndiyo unagundua mwalimu kamkosesha mtoto ama kampa tiki sehemu ambayo sio jibu sahihi.
Duh mimi ni mwalimu , naomba screenshot Salio lako bank na mimi ukifanya hivyo nascreen Salio langu bank halafu tutasoma nani Hana mwelekeo wa maisha kati yetu , ntataja namba zangu za olevel, na advance na wewe utaje tuone nani alikuwa kilaza
 
Back
Top Bottom