Nawakubali sana Waislamu kwenye kuzika, nawaza niweke kwenye wosia wangu nikifa nizikwe isizidi masaa 24

Mi wananikera sana mtu kafa leo na leoleo wanazika, tena wanaikimbiza maiti kwenda makaburini. Kule tu kukimbia na maiti kuwahi kuzika naona kama ni imani tu ya kishenzi, unakimbizaje maiti vile?
Kijesh jesh mkuu ndo ujanja.. hahahah
 
Hizo ni sheria za mwenyezimungu alizo muelekeza mtume wake muhammad kwamba kunavitu vitatu ambavyo havitakowo kucheleweshwa 1.mtu akitaka kuongia kwenye uislam 2. Ndoa 3. Mtu anapokua amefariki
Asante kwa elimu, tunajifunza
 
Mtu akifa hakuna haja ya kumzika harakaharaka bila sababu za msingi ndio maana kuna dawa za kuzuwia maiti kuoza na mochwari zipo ili kusubiri matayarisho ya kuzika yakamilike
Kuna siasa nyingi sana kwenye hicho kinachoitwa matayarisho ya kuzika. Ndo maana mimi sitachelewesha hili tukio, nahisi huko mbeleni nitagombana sana na watu kwenye hili
 
Walau masaa 24 tu na isizidi siku mbili
 
Uanruhusiwa mkuu Tena andika usizikwe na jeneza wakuingize kule PEMBEN mwamba ili BAADA yukihitaji kuongeza mwingine HAPO tusiteseke tunachimba PEMBEN tu
Hahahaha au sio mkuu wangu, hamna wanizike tu kwa jeneza ila iwe chap chap kijeshi
 
Sema hii inabidi uwe na imani fulani kabla, kwamba mwili ni kama boksi tu la mbao
 
Hilo hata kwenye ukiristo linawezekana tu. Andaa mazingira, weka wosia.

Na sio waislam wote wanazikwa siku hiyo hiyo.
 
Kabisa aisee, sioni ufahari kwenye kumuweka maiti mda mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…