Nawakubali sana Waislamu kwenye kuzika, nawaza niweke kwenye wosia wangu nikifa nizikwe isizidi masaa 24

Hahahaha au sio mkuu wangu, hamna wanizike tu kwa jeneza ila iwe chap chap kijeshi
Jeneza anachukua SEHEMU za watu mkuu
Unajua huku mbezi beach kunanmakaburi ya luventri mkuu huko asixikwe nduguyakoooo YAAN ukiona kazikiwa UJUE kampandia mwingine

Sasa Hawa WA dini yetu nawapenda hawachukui SEHEMU KUBWA YAAN ikitokea tunaenda kuxika waislam huwa pale KATIKATI yakaburi ndio tinachimba tunaweka mwingine

Huko HATA serikali za mitaa wamewashindwa
 
Umeogopa kuwekwa kwenye friji kama ice cream za bakhresa
 
Kukamuliwa mavi akukwepeki mkuuu eakikosa masela

Wale jamaa zetu funxa chini ya ardhi lazima wayakamuee so n SWALA LA uamuzi tu
 
Mi wananikera sana mtu kafa leo na leoleo wanazika, tena wanaikimbiza maiti kwenda makaburini. Kule tu kukimbia na maiti kuwahi kuzika naona kama ni imani tu ya kishenzi, unakimbizaje maiti vile?
Hao ambao hawakimbizwi huwa wanarudi tena duniani?
 
Hivi mnaoongeaga vitu kama hichi mnakuwaga wazima au??!!indio dalili za kichaa wewe kama unaona hupendi tokaa nenda huko kwenye uislam kwani kuna mtu kakushika??!!ukristo upo tangu miaka alfu iweje wewe uje ulopoke utumbo now🙄🙄🙄🙄 hebu tokaa hapa kaa kimya ukiona tofauti sepa kimya huwa siwaelewagi watu kama nyie
 
Mtu akifa hakuna haja ya kumzika harakaharaka bila sababu za msingi ndio maana kuna dawa za kuzuwia maiti kuoza na mochwari zipo ili kusubiri matayarisho ya kuzika yakamilike
Matayarisho ni nini?! Yaani mnachotayarisha ni nini?! Na hayo matayarisho yanahitaji nini na nini?! Ninachokiona kwa wasio waislamu ni kufanya msiba ni kama sharehe!,
Watu kula , kunywa na kucheza muziki!.
Kwetu sisi akifa muislamu kinachotakiwa ni mambo manne tu ya msingi na ya lazima!.
1️⃣Kumuosha maiti.
2️⃣ Kumvika sanda.
3️⃣ Kumswalia.
4️⃣ Kumzika na mambo yote manne hayamalizi hata masaa matano kila kitu tumemaliza.
 
Sisi huwa hatuziki hadi daktari athibitishe kuwa mtu kafa baada ya hapo tunaenda kuchimba kaburi.
Sasa utakuta mtu kafia hospitali na daktari kathibitisha kuwa mtu kafariki halafu mnamuweka wiki nzima mkingoja afufuke !.
 
Uanruhusiwa mkuu Tena andika usizikwe na jeneza wakuingize kule PEMBEN mwamba ili BAADA yukihitaji kuongeza mwingine HAPO tusiteseke tunachimba PEMBEN tu
Mtu ambaye siyo mwislamu hawezi zikwa kiislamu!.
Na maanisha hawezi oshwa na waislamu, kuvikwa sanda na waislamu, kuswaliwa na waislamu na kuzikwa na waislamu.
Labda akiusia watu wa dini yake wamfanyie kama waislamu wanavyowafanyia maiti wao wakikubali hapo sawa.
Mambo ya mazishi yanaingia kwenye kauli ya Allaah aliposema:
"{ لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ }
[Surah Al-Kāfirūn: 6]

Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu."
 
Huyu atazikwa na WAZAZI wake atakamuliwa na NDUGU zake lakn sio waislam
 
Msinichoshe na mambo mengi

Kuzikwa siku hiyo uwongo ndugu zangu wa ujerumani, Nairobi na dasilamu mpka wafike,
 

Katika uislamu ni dhambi kubwa kumchoma maiti hata angekuwa maiti huyo siyo mwislamu.
Katika hadithi mtume anasema kuvunja mfupa wa maiti ni sawa na kuvunja mfupa wa mtu ambaye hajafa.
Na kuhusu kuzika Allaah amesema kuhusu ardhi.
"{ ۞مِنۡهَا خَلَقۡنَٰكُمۡ وَفِيهَا نُعِيدُكُمۡ وَمِنۡهَا نُخۡرِجُكُمۡ تَارَةً أُخۡرَىٰ }
[Surah Ṭā-Hā: 55]

Kutokana nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo tunakurudisheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine
( tutakufufueni siku ya qiyaama)"

Na nasikia wachungaji wakati wa mazishi huwa wanamwambia maiti.
" Ulitoka kwenye mavumbi na sasa unarudi katika mavumbi................."
Imani za kuchoma maiti ni Imani za kipagani japo nasikia kuna askofu huko Afrika kusini aliusia akifa achomwe moto na kweli alivyokufa wakamchoma! Hata hapo Kenya kuna mwanasiasa mkongwe alikuwa ni jaji wakati wa serikali ya mkoloni akausia akifa achomwe na alipokufa alichomwa kama miaka miwili au mmoja na nusu iliyopita.
Japo wahindi mabaniani Bado wanachomana kwa moto wa kuni siku hizi kuna mashine maalumu za kuchoma maiti kwa moto wa umeme na kuacha majivu matupu!.
 
Usiwekeane ahadi na kifo kuwa uzikwaje

Mv Bukoba ilipozama kuna watu hadi leo hawajawahi.patikana

Ndege ya Malyasia ilipotelea angani na abiria wote hadi leo maiti zao hazikupatikana

Hujui utakapofia na utakufaje
 
Nyinyi wakristo mnaamini yesu alikufa na kuzikwa ! Swali ni je , Yesu alivyokufa kulingana na imani yenu
( sisi waislamu hatiamini kuwa Nabii Isa mwana wa Maryamu alikufa bali tunaamini alipaishwa kwenda mbingu bila kuonja mauti na atarudi duniani kabla ya Kiyama na atamuua dajjaali) YESU ALIZIKWA BAADA YA SIKU NGAPI ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…