VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Sitaki niwachoshe kwa maneno mengi. Nawaambieni tu kwa kifupi na kwa uhakika. Bakuli la michango analolitembeza mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu si la kubezwa au kumezwa. Yaweza kuwa ni kwa kujua au kutokujua, Lissu anaruka kikwazo kikuu kilichosukwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu: ukata kwa vyama vya upinzani. Ukata tata ungewakata na kuwavuta wapinzani nyuma na kuwafanya washindwe kufanya kampeni.
Mipango kabambe ilishasukwa kitambo kuvifanya vyama vya upinzani mwaka huu kuandamwa na ukata wa kifedha. CCM yetu yenyewe, kwakuwa ina rasilimali za kutosha na kutisha na kwakuwa imejibanza kwenye koti la Serikali, ilijiandaa kujidai itakavyo kwenye kampeni hizi huku wapinzani wakishindwa kufanya kampeni. Mipango ilisukwa vyema. Kampeni zina gharama nyingi: usafiri, malazi,mavazi, chakula, vifaa vya sauti, majukwaa na kadhalika.
Mipango ya kuufanya ukata umee kwenye vyama vya upinzani ilianza miaka kadhaa iliyopita. Karibu kila chama kikubwa cha upinzani hapa nchini vikiwemo CHADEMA, ACT na NCCR-Mageuzi kina chama au vyama rafiki nje ya Tanzania. Marafiki hao wa nje husaidia vyama hivyo kifedha hasa kwenye harakati kama hizi za kiuchaguzi. Na hakukuwa na ubaya kuhusu kusaidiana huko. Lakini, mwaka huu misaada hiyo imepigwa pini. Imezibwa. Hakuna misaada tena. Ukata!
Lissu ajaziwe bakuli lake. Achangiwe. Hata mimi, kama mfuasi ninayejinafasi wa demokrasia ya vyama vingi, nimeshamchangia Lissu. Lazima tuwe na mgombea strong wa upinzani ili kutufanya tuchague vyema. Lazima mwaka huu mchuano mkali uwe kati ya Dkt. Magufuli na Lissu. Lazima tusikie sera za kila mmoja wao na tuamue. Bakuli la Lissu, hata kama litakejeliwa na kudhihakiwa, lina maana kubwa: linaruka mipango ya kidhalimu ya kutengeneza ukata kwa wapinzani.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma, Tanzania)