Nawapa siri nyingine; vitu vya bure vina laana. Ukitaka kupata sharti utoe kidogo

Nawapa siri nyingine; vitu vya bure vina laana. Ukitaka kupata sharti utoe kidogo

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
NAWAPA SIRI NYINGINE; VITU VYA BURE VINA LAANA. UKITAKA KUPATA SHARTI UTOE KIDOGO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Huwezi ukafanikiwa kwa kitu ulichopewa bure au ulichokipata bure bila kukitolea jasho au sadaka au kitu chochote. Hii ni siri ambayo wengi hawaijui lakini walifundishwa wakiwa watoto kwa namna nyingi.

Angalia watu wanaopewa vitu vya burebure karibu wote wanalaana. Wanamaisha magumu. Ni maskini, tegemezi na watumwa.

Angalia wanawake wengi. Ni maskini, wanalaana na ngumu kufanikiwa kwa sababu wanapenda vitu vya bure na siku zote mtu anayepokea vitu vya burebure bila kulipia gharama lazima alaanike. Hawezi fika popote.

Huwezi taka ulipiwe nauli tuu burebure utegemee utakuwa mtu wa maana. Umejilaani mwenyewe.

Wanaojua siri hizi hawataki kusema ukweli wote.

Katika mafundisho ya Dini Kuna kitu kinaitwa Dhabihu, zaka na Sadaka.

Kikanuni, Mungu nimuweza wa yote. Anakila kitu lakini aliweka mfumo wa ukitaka kupokea sharti utoe kidogo. Unaitwa uwekezaji.

Ukipata kitu, unatoa sehemu ya kile kitu unamrudishia aliyekupatia. Hata kama sio siku hiyohiyo.

Ukienda ugenini. Inasemwa usiende mikono mitupu. Usikae burebure. Na mgeni akiondoka kwako asitoke mikono mitupu. Hizo ni kanuni za kustawi, kuneemeka na kufanikiwa. Najua haya mambo wengi hawajafundishwa na waliofundishwa wanapuuza.

Uliwahi kufika sehemu ukaona watu wanatunza?
Yaani umeenda labda kwenye tamasha fulani, kuna waimbaji au wasanii. Wanafanya burudani alafu ukaona baadhi ya watu wakitoka kuwatunza pesa. Wale sio wajinga.

Mtu akikufurahisha sana. Asikufurahishe bure. Kama una hata buku tano mpe. Utakuja kunishukuru.

Unaenda Kanisa au msikitini. Sheikhe au Mchungaji kaongea mambo ambayo umejifunza sana au yamekubariki. Usikubali kujifunza bure au kubarikiwa burebure. Hazitafanya kazi. Hutozifanyia chochote.

Hakunaga kitu cha bure ambacho utakifanyia jambo la maana. Zaidi kitakuletea matatizo.

Hapo ndipo umuhimu wa kushukuru unapojitokeza. Unashukuru kwa jambo la baraka na lililokufurahisha.

Pili, unatoa kidogo sehemu ya jasho(mali yako) kulipia kile kilichokubariki au kufurahisha. Hiyo ni kufanya baraka hizo ziwe na kibali bila vizuizi.

Nimemaliza. Hiyo ni kwa wenye ufahamu.

TaikonMaster
Kwa sasa Masaki, Dar es salaam
 
Binafsi naita Sadaka

Sadaka ni lango la mafanikio

Hata waabudu shetani wanatoa Sadaka

Mungu aliagiza aletewe Sadaka ya Isaka, mtoto pekee wa Ibrahimu ili kuzidi kumfunulia mafanikio Ibrahimu

NB: Hela usiyoitolea jasho hautaona mafanikio yake, easy come easy go
 
Hili wengi hawalijui au wanalijua lakini wanapuuza
 
Hili wengi hawalijui au wanalijua lakini wanapuuza
Ni kweli, japo ni vyema kutoa Sadaka sehemu sahihi

Sadaka huambatana na nia(kunuiza), kwamba unatoa Sadaka fulani ili kuomba jambo fulani

Mfano naomba kwa mizimu, mke wangu abebe mimba baada ya kusubiria miaka 10 ya ndoa, ombi langu linaambata na Sadaka ya Kondoo kwa mizimu

Baada ya miezi 3, mke anabeba mimba 🙏🙏
 
Vijana hizi mambo hawazielewi.

Ngoja niwaite wadogo zangu
Lamomy ledada min -me Bushmamy
 
Haya uliyoyasema hayana udhibitisho kwa asilimia 100

Ila kuna kutoa sadaka huku hakuna shaka,inasemwa kadri unavyotoa ndio kadri unavyozidishiwa, hiyo imedhibiti kwenye vitabu vya dini, na matajiri wanajua vizur sana hii siri,ndio maana huwa wanatoa na kuzidishiwa zaidi

Sadaka pia ni sehemu ya kufanyiwa wepesi mambo yako,na ubakhiri ni sehemu ya kufanyiwa mambo yako yasiwe mepesi

Sadaka pia ni sehemu ya kutibu maradhi yetu,toa sadaka kwa nia ya kupata nafuu kwa maradhi yako

Sadaka pia hufuta madhambi yetu,imedhibiti kwenye vitabu vya dini

Lakini sikubaliana na wewe kwamba eti asiye toa kuwa amelaaniwa au analaaniwa!

Hapana! Hapa haupo sahihi hata kidogo,unless hujui maana ya laana.

Asante
 
Soma vizuri tena.
Title iko wazi kabisa.
Kama hutaki kutoa usipokee. Hiyo ni kanuni.

Ukipokea tafsiri yake kuna sehemu unatakiwa utoe. Nature yenyewe iko wazi. Inaeleza kila kitu.
 
Soma vizuri tena.
Title iko wazi kabisa.
Kama hutaki kutoa usipokee. Hiyo ni kanuni.

Ukipokea tafsiri yake kuna sehemu unatakiwa utoe. Nature yenyewe iko wazi. Inaeleza kila kitu.
Hakuna kitu kama hicho mkuu,sikulazimishi uniamini,baki na msimamo wako nami na msimamo wangu, simple!
 
Back
Top Bottom