Nawapa siri nyingine; vitu vya bure vina laana. Ukitaka kupata sharti utoe kidogo

NAWAPA SIRI NYINGINE; VITU VYA BURE VINA LAANA. UKITAKA KUPATA SHARTI UTOE KIDOGO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Huwezi ukafanikiwa kwa kitu ulichopewa bure au ulichokipata bure bila kukitolea jasho au sadaka au kitu chochote. Hii ni siri ambayo wengi hawaijui lakini walifundishwa wakiwa watoto kwa namna nyingi.

Angalia watu wanaopewa vitu vya burebure karibu wote wanalaana. Wanamaisha magumu. Ni maskini, tegemezi na watumwa.

Angalia wanawake wengi. Ni maskini, wanalaana na ngumu kufanikiwa kwa sababu wanapenda vitu vya bure na siku zote mtu anayepokea vitu vya burebure bila kulipia gharama lazima alaanike. Hawezi fika popote.

Huwezi taka ulipiwe nauli tuu burebure utegemee utakuwa mtu wa maana. Umejilaani mwenyewe.

Wanaojua siri hizi hawataki kusema ukweli wote.

Katika mafundisho ya Dini Kuna kitu kinaitwa Dhabihu, zaka na Sadaka.

Kikanuni, Mungu nimuweza wa yote. Anakila kitu lakini aliweka mfumo wa ukitaka kupokea sharti utoe kidogo. Unaitwa uwekezaji.

Ukipata kitu, unatoa sehemu ya kile kitu unamrudishia aliyekupatia. Hata kama sio siku hiyohiyo.

Ukienda ugenini. Inasemwa usiende mikono mitupu. Usikae burebure. Na mgeni akiondoka kwako asitoke mikono mitupu. Hizo ni kanuni za kustawi, kuneemeka na kufanikiwa. Najua haya mambo wengi hawajafundishwa na waliofundishwa wanapuuza.

Uliwahi kufika sehemu ukaona watu wanatunza?
Yaani umeenda labda kwenye tamasha fulani, kuna waimbaji au wasanii. Wanafanya burudani alafu ukaona baadhi ya watu wakitoka kuwatunza pesa. Wale sio wajinga.

Mtu akikufurahisha sana. Asikufurahishe bure. Kama una hata buku tano mpe. Utakuja kunishukuru.

Unaenda Kanisa au msikitini. Sheikhe au Mchungaji kaongea mambo ambayo umejifunza sana au yamekubariki. Usikubali kujifunza bure au kubarikiwa burebure. Hazitafanya kazi. Hutozifanyia chochote.

Hakunaga kitu cha bure ambacho utakifanyia jambo la maana. Zaidi kitakuletea matatizo.

Hapo ndipo umuhimu wa kushukuru unapojitokeza. Unashukuru kwa jambo la baraka na lililokufurahisha.

Pili, unatoa kidogo sehemu ya jasho(mali yako) kulipia kile kilichokubariki au kufurahisha. Hiyo ni kufanya baraka hizo ziwe na kibali bila vizuizi.

Nimemaliza. Hiyo ni kwa wenye ufahamu.

TaikonMaster
Kwa sasa Masaki, Dar es salaam
Naomba namba yako nitoe sadaka yangu
 
Lipieni hewa mnayovuta bure hapo ndio nitawaelewa, kila kitu kimewekwa bure, ni tamaa na kujilimbikizia mali kwa mwanadamu kulikopelekea wachache kuhodhi vingi mwishowe kuwaacha wengi kwenye scarcity. Mbona tunagawa bure migodi yetu, mbuga zetu, mashamba yetu kwa jina la uwekezaji na kuwaacha wakijichotea kila kitu na kutuacha patupu?. Makinikia yalikuwa yanatoka bure kabisa mpaka mwendazake akasimamia kimtindo, naamini kwa sasa wanajichukulia tu mabilionea wa Acacia.

Babu zetu waligawana mashamba bure kabisa, wamekuja matapeli wa maghalibi kutufundisha References zao kama hizo kwenye bible aMBAZO sio size yeTu, hao ni wayahudi na warumi huko, neno bure lina-exist KWA NINI? sababu bure ipo na ni fare tu, inapobidi. Hiyo ya kutoa sadaka mtakuja watoa mpaka watoto zenu kisa tama ya dunia hadaa.
We kiazi kweli! Haya ni mali ya nani tukalipie!
 
Ni kweli, japo ni vyema kutoa Sadaka sehemu sahihi

Sadaka huambatana na nia(kunuiza), kwamba unatoa Sadaka fulani ili kuomba jambo fulani

Mfano naomba kwa mizimu, mke wangu abebe mimba baada ya kusubiria miaka 10 ya ndoa, ombi langu linaambata na Sadaka ya Kondoo kwa mizimu

Baada ya miezi 3, mke anabeba mimba 🙏🙏
Alafu akishachinjwa analiwa na wewe au analiwa na sisimizi?
 
Sadaka ni muhimu sana, tena ukiitoa kwa nia ni lazima ufanikiwe

Habari za Sadaka za waabudu shetani si mnazisikia?

Unaambiwa mtoa Mtoto wako wa kidati Cha 6, ama mtoe mke wako n.k

Unatoa Sadaka inayokuuma kuitoa

Sahihi kabisa
 
NAWAPA SIRI NYINGINE; VITU VYA BURE VINA LAANA. UKITAKA KUPATA SHARTI UTOE KIDOGO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Huwezi ukafanikiwa kwa kitu ulichopewa bure au ulichokipata bure bila kukitolea jasho au sadaka au kitu chochote. Hii ni siri ambayo wengi hawaijui lakini walifundishwa wakiwa watoto kwa namna nyingi.

Angalia watu wanaopewa vitu vya burebure karibu wote wanalaana. Wanamaisha magumu. Ni maskini, tegemezi na watumwa.

Angalia wanawake wengi. Ni maskini, wanalaana na ngumu kufanikiwa kwa sababu wanapenda vitu vya bure na siku zote mtu anayepokea vitu vya burebure bila kulipia gharama lazima alaanike. Hawezi fika popote.

Huwezi taka ulipiwe nauli tuu burebure utegemee utakuwa mtu wa maana. Umejilaani mwenyewe.

Wanaojua siri hizi hawataki kusema ukweli wote.

Katika mafundisho ya Dini Kuna kitu kinaitwa Dhabihu, zaka na Sadaka.

Kikanuni, Mungu nimuweza wa yote. Anakila kitu lakini aliweka mfumo wa ukitaka kupokea sharti utoe kidogo. Unaitwa uwekezaji.

Ukipata kitu, unatoa sehemu ya kile kitu unamrudishia aliyekupatia. Hata kama sio siku hiyohiyo.

Ukienda ugenini. Inasemwa usiende mikono mitupu. Usikae burebure. Na mgeni akiondoka kwako asitoke mikono mitupu. Hizo ni kanuni za kustawi, kuneemeka na kufanikiwa. Najua haya mambo wengi hawajafundishwa na waliofundishwa wanapuuza.

Uliwahi kufika sehemu ukaona watu wanatunza?
Yaani umeenda labda kwenye tamasha fulani, kuna waimbaji au wasanii. Wanafanya burudani alafu ukaona baadhi ya watu wakitoka kuwatunza pesa. Wale sio wajinga.

Mtu akikufurahisha sana. Asikufurahishe bure. Kama una hata buku tano mpe. Utakuja kunishukuru.

Unaenda Kanisa au msikitini. Sheikhe au Mchungaji kaongea mambo ambayo umejifunza sana au yamekubariki. Usikubali kujifunza bure au kubarikiwa burebure. Hazitafanya kazi. Hutozifanyia chochote.

Hakunaga kitu cha bure ambacho utakifanyia jambo la maana. Zaidi kitakuletea matatizo.

Hapo ndipo umuhimu wa kushukuru unapojitokeza. Unashukuru kwa jambo la baraka na lililokufurahisha.

Pili, unatoa kidogo sehemu ya jasho(mali yako) kulipia kile kilichokubariki au kufurahisha. Hiyo ni kufanya baraka hizo ziwe na kibali bila vizuizi.

Nimemaliza. Hiyo ni kwa wenye ufahamu.

TaikonMaster
Kwa sasa Masaki, Dar es salaam
Taikon umenifundisha sana kwenye hili
 
Back
Top Bottom