Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Mkuu tatizo huwa hampendi kuwasikiliza watu wenye akili na UJINGA umekuwa ni sehemu ya maisha yetu, kitu ambacho hata Mwl J.K Nyerere alikibainisha kama ni adui wa maendeleo...

Tatizo namba moja linalosumbua Afrika, Tanzania ikiwemo ni UJINGA (ukosefu wa maarifa)...

Taifa lenye watu wajinga, lenye kukumbatia ujinga ni hakika litaangamia...

Biblia imeandika, watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, kwa kuwa pasipo maarifa hakuna hatua...

Hivyo basi, badala ya viongozi kusubiri waelezwe shida za wananchi, wanapaswa watafute namna ya kuondoa UJINGA...

Nitakupa mfano mmoja, mtaa ninaoishi una barabara nzuri kabisa imejengwa kwa kiwango cha zege, lakini hii barabara haipitiki nyakati za jioni kwa sababu nusu ya barabara inageuka kuwa parking ya bajaj, bodaboda na watu binafsi...

Mfano mwingine ni maeneo kama Mbezi Mwisho ambapo kuna barabara nzuri kabisa zilizojengwa kuondoa kero ya msongamano wa magari, lakini kwa sasa barabara zile zimemegwa nusu na wachuuzi kiasi kwamba ni sawa na kutokuwa na barabara...

Kuna mengi ya kueleza lakini itakuwa ni kazi bure kama hatutakubali kuachana na UJINGA...
 
Watanzania sijui nani katuroga hawa viongozi wakija humu ndio pakutemea shida zetu ambazo zilikua ngumu kufika kwao lakini leo hii akitokea kiongozi humu wale wale waliokua wanatokwa mapovu na mishipa ya shingo kusimama kama punda vihongwe ndio wanaanza ,


Za siku mjuu mimi John tulisoma wote igunda so what? Mara huyu nakukubali sana kiongozi, mara yule hakuna kama wewe gombea uraisi mkuu watu wanakupenda sanaa🤣🤣🤣

Mwingine utasikia mkuu ulivaa suti juzi ulitoka kali saaanaaa (rejea uzi wa waziri Gwajima)
Mwenzenu nilishawahi toa la moyoni hapa kesho yake tu nikaona mshike mshike kwenye ile ofisi nyie sifieni sifieniii tuuu au mmesomewa Kurjuaaaan eeenh
 
Karibu sana bwana Msigwa.

Sasa weye hapa usijitambulishe kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali jitambulishe tu kama Gerson Msigwa na cheo chako.

Pili, tuainishie hapa majukumu yako kiserikali na pia nini watarajia kutoka kwetu kama wauliza masuali kadhaa kuhusu serikali na nchi yetu.

Karibu sana hapa JF ila usikimbie masuali mazito na usikwazike na aina ya masuali maana masuali mazito na magumu yatakuweka sawa weye na hata sisi yatatuweka sawa na pia yatawasaidia viongozi wenzio huko serikalini.
 
Nchi imejaa machawa na kunguni, kujikomba komba tu inashangaza sana
 
Ila walimu bana
Kwanini mko hivyo MTU hata ajamaliza kuongea mnajieleza shida kibao
Tanawaheshimu Sana Ila na nyie muangalie na mahali sahihi na Wakati sahihi
 
Dada Yangu Doriss amewashtua nini kuwa huku ndio habari ya mjini!
Mlitutenga, naona mnakuja Kasi!
 
Karibu sana kiongozi hapa jukwaani kwa ma GREAT THINKERS ..jitahidi uwe na ngozi ngumu hapa kuna spana zilizoshiba kama za Makonda.
 
Nikukaribishe na swali!
Kuna taarifa kuhusu uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa kukarabatiwa kwa pesa nyingi zaidi ya zikizotumika kukarabati uwanja ule wa Zanzibar ila Uwanja wa Zanzibar umekarabatiwa kwa viwango zaidi ya huu wa kwetu!

Je kuna ukweli wowote?
 
Matu 12 online...

Gabon ukae ukijua Yanga ubingwa bye bye.... pelekeni michezo na makocha shuleni kuna vipaji.
Michezo ni ajira
 
Umesema vyema. Wape madini waondoe ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…