Nawaza mateso waliopata watu kwa kutongozana kabla simu hazijaja

Miaka hiyo, wasichana walikuwa na adabu kama unataka kuongea nae unamtuma mtoto wa jirani na kwao huku umempa kimemo ampelekee.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa nimeupitia nakumbuka mbali.sana
 
Kwahiyo ikaishia hapo?
 
Hahahaha
 
Mungu ni wa ajabu sana, sisi miaka hii ndiyo tumeivuruga nguvu ya uvutano ya mtu na mtu ya asili, zamani iliwezekana mtu kupata hisia kuwa kuna jambo linanihusu, anaondoka kwake kimatembezi tu na kufika mbele yanatokea unayoyasema hapo juu.

Baadaye ikaja matumizi ya barua na vishenga (vingi vilikuwa vitoto vya shule kwa maeneo ya mijini na vijijini) vilikuwa viadilifu kufikisha barua na kurudisha majibu bila kufungua (nahisi kwa leo hii vingefungua vinasoma na kuchukua nafasi)

Tuliokulia vijijini, tulikuwa tunaandika barua, tunavizia binti anapokwenda mtoni kuteka maji tunaitupa barua njiani tukiwa tumejificha kichakani, akipita ataiokota, ataisoma, ukiona ameondoka nayo basi kuna dalili njema za kujibiwa, ukiona ameitupa hapohapo basi application imefail.

Siku za mapumziko mkienda mtoni kufua, ziliweza kukupa majibu ya application, binti alikuwa anaweza, kuanika nguo maeneo ya karibu na unapofulia ili apate nafasi ya kukupa lake la moyoni kwa siri sana, na wala haikuwa inajulikana.
 
Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…