Nawaza mateso waliopata watu kwa kutongozana kabla simu hazijaja

Nawaza mateso waliopata watu kwa kutongozana kabla simu hazijaja

Kipindi cha nyuma 1985-2000 simu zilikuwa nadra sana,

Lakin pamoja na uchache wa simu, watu walitia maneno mpaka wenza wao wakawaelewa,

Kwa wale wa juzi juzi mmerahisishiwa kazi sana,

Mtu kipindi hicho anakaa Tabata anamfuatilia msichana wa makumbusho bila hata simu, inabidi apande gari akashuke mwenge atembee mpaka bamaga kwakuwa anahisi msichana yule atapita maeneo yale kama siku alivyomuona akipita nyuma,

Na anamkosa, anaamua kurudi home, kesho yake anatia kambi tena lakin hafanikiwi, hii ilileta hamasa kwamba hata akimpata maneno ni hapo hapo,

Watu wameng'atwa sana na Mbu wakiwasubiri kina Mwajuma wapite njia fulani kisa wameona anapita asubuhi,

Watu wameshinda mtoni wakiwasubiri akina hilda ili wapate nafasi ya kutema yao

Watu wameteseka mno,

Siku hizi wanaume hata kutongoza imekuwa shida neno linalotangulia ni NAOMBA NAMBA YAKE HIYO DADA,

hawana uwezo tena wa kumface mwana mke kumtemea cheche live,

Siku hizi wamerahisishiwa sana , mwanamke akikunyima namba ya simu unamuomba basi anayotumia tigo pesa haha anaachia mara moja
Nimetembea sana kutafta madem
 
Shuleni tulikuwa tunaandika barua tunaiweka katikati ya daftari ya binti, wengi walipata misukosuko kwani baadhi ya mabinti waliozembea barua zilinaswa na walimu na wengine zilidondoka njiani bila wao kujua
Mi nimewai pewa adhabu ya kuchimbia kksima
 
Shuleni tulikuwa tunaandika barua tunaiweka katikati ya daftari ya binti, wengi walipata misukosuko kwani baadhi ya mabinti waliozembea barua zilinaswa na walimu na wengine zilidondoka njiani bila wao kujua
Hatari sana hiyo , high risk with high return
 
Siku hizi wanaume hakuna, wote tunajipanga nao foleni kununua chips mayai, wanaume wanasafisha kucha saloon doh, wanaume wanawekwa Heleni,
Thubutu upite mbele yangu nachanganya mpaka michezo ya amber ruti
 
Back
Top Bottom