Nawaza mateso waliopata watu kwa kutongozana kabla simu hazijaja

Miaka hiyo, wasichana walikuwa na adabu kama unataka kuongea nae unamtuma mtoto wa jirani na kwao huku umempa kimemo ampelekee.
Kipindi cha nyuma 1985-2000 simu zilikuwa nadra sana,

Lakin pamoja na uchache wa simu, watu walitia maneno mpaka wenza wao wakawaelewa,

Kwa wale wa juzi juzi mmerahisishiwa kazi sana,

Mtu kipindi hicho anakaa Tabata anamfuatilia msichana wa makumbusho bila hata simu, inabidi apande gari akashuke mwenge atembee mpaka bamaga kwakuwa anahisi msichana yule atapita maeneo yale kama siku alivyomuona akipita nyuma,

Na anamkosa, anaamua kurudi home, kesho yake anatia kambi tena lakin hafanikiwi, hii ilileta hamasa kwamba hata akimpata maneno ni hapo hapo,

Watu wameng'atwa sana na Mbu wakiwasubiri kina Mwajuma wapite njia fulani kisa wameona anapita asubuhi,

Watu wameshinda mtoni wakiwasubiri akina hilda ili wapate nafasi ya kutema yao

Watu wameteseka mno,

Siku hizi wanaume hata kutongoza imekuwa shida neno linalotangulia ni NAOMBA NAMBA YAKE HIYO DADA,

hawana uwezo tena wa kumface mwana mke kumtemea cheche live,

Siku hizi wamerahisishiwa sana , mwanamke akikunyima namba ya simu unamuomba basi anayotumia tigo pesa haha anaachia mara moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu uzi ungepewa attention maalum kama ule wa wanywa pombe bhana. kukumbushwa those sweet days of ours...! wapi tena ningekumbuka haya mambo. watoto wa siku hizi hawakutani na heka heka za kukanyaga. miiba, vifutu, kukutana na fisi, mbwa mwitu au wazee wa kazi ukiwa umetoka. kufanya doria la kujitolea au tuote uwindaji wa kile nafsi imenuia ukipate.

mbaya zaidi umuwinde miezi 4 kisha akukate mchana kweupee, ebana eeeh.

ngoja smartphones zije wanamalizana whatsap, insta, sijui fb au text tu kwa gharama ya bando. za 500, saivi wangeishia kukamtwa uzururaji.
Kabisa nimeupitia nakumbuka mbali.sana
 
kuna mmoja aliitwa n...a alinitaka kwasababu nilikuwa mambo safi akaweka barua mi nikawa sijui, kumbe kuna mwingine anaitwa ja,,,k nilikuwa naonekana kama kutoka naye sasa alikuwa analalamika sana kwamba umuache huyo nimekuonesha hisia zangu hujaona, dah tukakusanya madaftari walimu si wakaona??>??? hatariii
Kwahiyo ikaishia hapo?
 
Kule vijijini tulikuwa tunaandika barua tunajificha kichakani tukisubiri binti anapokwenda au kutoka kuteka maji kisimani tunairusha barua njiani uso wa bahasha kwenye anuani yake ukiwa juu, akifika na kuiona anaichukua, ngoma ilikuwa kufuatilia majibu ya hiyo barua
Hahahaha
 
Kipindi cha nyuma 1985-2000 simu zilikuwa nadra sana,

Lakin pamoja na uchache wa simu, watu walitia maneno mpaka wenza wao wakawaelewa,

Kwa wale wa juzi juzi mmerahisishiwa kazi sana,

Mtu kipindi hicho anakaa Tabata anamfuatilia msichana wa makumbusho bila hata simu, inabidi apande gari akashuke mwenge atembee mpaka bamaga kwakuwa anahisi msichana yule atapita maeneo yale kama siku alivyomuona akipita nyuma,

Na anamkosa, anaamua kurudi home, kesho yake anatia kambi tena lakin hafanikiwi, hii ilileta hamasa kwamba hata akimpata maneno ni hapo hapo,

Watu wameng'atwa sana na Mbu wakiwasubiri kina Mwajuma wapite njia fulani kisa wameona anapita asubuhi,

Watu wameshinda mtoni wakiwasubiri akina hilda ili wapate nafasi ya kutema yao

Watu wameteseka mno,

Siku hizi wanaume hata kutongoza imekuwa shida neno linalotangulia ni NAOMBA NAMBA YAKE HIYO DADA,

hawana uwezo tena wa kumface mwana mke kumtemea cheche live,

Siku hizi wamerahisishiwa sana , mwanamke akikunyima namba ya simu unamuomba basi anayotumia tigo pesa haha anaachia mara moja
Mungu ni wa ajabu sana, sisi miaka hii ndiyo tumeivuruga nguvu ya uvutano ya mtu na mtu ya asili, zamani iliwezekana mtu kupata hisia kuwa kuna jambo linanihusu, anaondoka kwake kimatembezi tu na kufika mbele yanatokea unayoyasema hapo juu.

Baadaye ikaja matumizi ya barua na vishenga (vingi vilikuwa vitoto vya shule kwa maeneo ya mijini na vijijini) vilikuwa viadilifu kufikisha barua na kurudisha majibu bila kufungua (nahisi kwa leo hii vingefungua vinasoma na kuchukua nafasi)

Tuliokulia vijijini, tulikuwa tunaandika barua, tunavizia binti anapokwenda mtoni kuteka maji tunaitupa barua njiani tukiwa tumejificha kichakani, akipita ataiokota, ataisoma, ukiona ameondoka nayo basi kuna dalili njema za kujibiwa, ukiona ameitupa hapohapo basi application imefail.

Siku za mapumziko mkienda mtoni kufua, ziliweza kukupa majibu ya application, binti alikuwa anaweza, kuanika nguo maeneo ya karibu na unapofulia ili apate nafasi ya kukupa lake la moyoni kwa siri sana, na wala haikuwa inajulikana.
 
Kipindi cha nyuma 1985-2000 simu zilikuwa nadra sana,

Lakin pamoja na uchache wa simu, watu walitia maneno mpaka wenza wao wakawaelewa,

Kwa wale wa juzi juzi mmerahisishiwa kazi sana,

Mtu kipindi hicho anakaa Tabata anamfuatilia msichana wa makumbusho bila hata simu, inabidi apande gari akashuke mwenge atembee mpaka bamaga kwakuwa anahisi msichana yule atapita maeneo yale kama siku alivyomuona akipita nyuma,

Na anamkosa, anaamua kurudi home, kesho yake anatia kambi tena lakin hafanikiwi, hii ilileta hamasa kwamba hata akimpata maneno ni hapo hapo,

Watu wameng'atwa sana na Mbu wakiwasubiri kina Mwajuma wapite njia fulani kisa wameona anapita asubuhi,

Watu wameshinda mtoni wakiwasubiri akina hilda ili wapate nafasi ya kutema yao

Watu wameteseka mno,

Siku hizi wanaume hata kutongoza imekuwa shida neno linalotangulia ni NAOMBA NAMBA YAKE HIYO DADA,

hawana uwezo tena wa kumface mwana mke kumtemea cheche live,

Siku hizi wamerahisishiwa sana , mwanamke akikunyima namba ya simu unamuomba basi anayotumia tigo pesa haha anaachia mara moja
Hahaha
 
Back
Top Bottom