Naweza Kudumu Kwenye Siasa Bila Rushwa? Maadili Yangu Yananizuia au Yatanisaidia?

Naweza Kudumu Kwenye Siasa Bila Rushwa? Maadili Yangu Yananizuia au Yatanisaidia?

ranchoboy

Member
Joined
Feb 22, 2022
Posts
46
Reaction score
49
Ndugu zangu,

Nimekua nikijiuliza jambo zito Je, mtu anayeishi kwa kusema ukweli, kuchukia rushwa, na kushikilia maadili anaweza kweli kusimama imara kwenye siasa zetu za sasa? Mimi ni mtu ninayethamini haki kuliko kitu chochote. Nachukia rushwa kwa nguvu zote, kiasi kwamba hata kama ningepewa nafasi ya kuchagua njia fupi na rahisi kufanikisha jambo fulani, nisingeikubali kama inaleta mwanya wa hila au udanganyifu. Napenda sana kwenda na njia ndefu ilimradi ni halali na ya haki.

Nitatoa mfano halisi wa maisha yangu nikiwa chuo. Mara nyingi darasani mwalimu akiacha nafasi kidogo ya udanganyifu (cheating), kwenye mtihani, test au quiz wenzangu wanachangamkia hiyo fursa. Lakini kwangu, hata kama nafasi ya kuibia iko wazi, siko tayari kufanya hivyo Yani Niko tayari kupata sifuri yakwangu kuliko mia ya mtu mwingine. Mara nyingi najikuta nakuwa tofauti na wenzangu ambao hunitazama kwa mshangao kwa kushikilia misingi hii.

Kwa muda sasa nimekuwa nikifikiria sana kuhusu kuingia kwenye siasa, lakini nashindwa kuelewa kama mtu kama mimi atashinda au kushindwa. Ukweli ni kwamba siasa zetu zimejaa rushwa, hila, na unafiki—je, kuna nafasi kwa mtu anayesema ukweli na anayeamini kwenye kufanya mambo sahihi kwa haki na uwazi? Mimi siyo mnafiki. Nikisema ndiyo, ni ndiyo. Na nikisema hapana, ni hapana. Lakini najiuliza, je, naweza kuishi na kufanikiwa kwenye mfumo wa kisiasa uliopo, au maadili yangu yatanikwamisha?

Sote tunafahamu kwamba siasa ni mchezo mgumu—lakini je, tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli bila kuacha maadili yetu? Je, Tanzania yetu inaweza kweli kupata viongozi wanaosimama kwa uadilifu bila kujihusisha na rushwa au unafiki? Kama inawezekana, ni jinsi gani tutafika huko? Au ni kweli kwamba ukiingia kwenye siasa ni lazima "uendane na mfumo"?

Ningependa kusikia maoni yenu. Je, inawezekana kubadili mchezo wa siasa na kuondoa mizizi ya rushwa? Ni changamoto gani tutakutana nazo kama tutaamua kusimama na ukweli? Au tumezama kwenye mfumo huu kiasi kwamba ni lazima tubadilike ili kuendana nao?

#UadilifuKwanza #SiasaSafiTanzania #RushwaNiAdui #MabadilikoYaKweli
 
Back
Top Bottom