Naweza kuipata wapi dawa ya kunguni?

Naweza kuipata wapi dawa ya kunguni?

Nilihangaishwa na hawa wadudu kwa muda mrefu, nilituma kila dawa niliyoelekezwa za kienyeji na za kitaalamu bila mafanikio mpaka nilipokutana na mama mmoja anayeuza dawa ya asili ya kuua kunguni aisee! imebaki historia nililipa Tsh 1000 tu lakini kunguni waliisha Kabisa . Dawa ya huyu mama ni nzuri imeua soko la dawa za madukani mpaka wenye maduka ya kilimo hawampendi huyu mama.
Halafu hutaki kuitaja hiyo dawa wala anakopatikana huyo mama.
 
Ingia duka la dawa za Mifugo

ULIZIA DAWA INAITWA DIAZINONE

UPEWE HIO HIO NA SIO VINGINEVYO

kama uko Dar nitafute 0744033555 nikumalizie shughuli kwa elfu 15 tu

Mtaalam hii ndio komesha.
 
Huna akili, unaweza ukasafiri na bus ukawabeba kunguni mpaka nyumbani kwako, sasa wakishafika kuwaangamiza kwake siyo mziki wa kitoto.
Mkuu mwenye akili.
Unataka kuniambia toka 2020 bado hao wadudu wanakusumbua?
Maeneo ya kwenu Kuna watu wanaotanya fumigation? Au nenda duka la karibu ukaulizie ile dawa tunayo wa spray nguruwe. Kichupa kidogo Sana ukichanganya na maji inakua Kama chai ya maziwa I am forgetting the name. Hutaona sio kunguni tu ila kilaa mdudu atambaayye
 
Mzee mimi ni muhanga wa Hao wadudu kwa miaka karibu Mitatu! ni wadudu wa ajabu sana, Nilitumia Dawa zote za Kunguni bila mafanikio. Ila nilikuja kuwaangamiza kwa njia rahisi sana.

Kwanza unatakiwa kujua maeneo wanamojificha zaidi katika chumba.

Sehemu yao No 1 ni kwenye Foronya.
Sehemu yao ya 2 ni kwenye Kitanda hasa kikiwa cha mbao, Hujificha kwenye pembe na maungio ya kitanda. huzaliana humo kwa raha mustarehe wakipata food ya damu kila siku na kurudi kwenye makao yao salama ya kitanda.
Sehemu yao 3 ni kwenye sofa, hasa kama una sofa la kitambaa.
Sehemu yao ya 4 ni kwenye nguo unazazovaa.

TIBA YA UHAKIKA.

Kwa upande wangu Naamini Tiba kiboko ya kunguni ni MAJI YA MOTO

Hatua.

1. Chemsha maji kwenye sufuria yachemke na kutokota.
2. Weka maji hao kwenye Chombo
3.Tenganisha Dogoro na Kitanda.

Kama unaweza Fungua Kitanda kabisa Uweke chini

4.Mwagia Maji yaliyotoka kutokota kitanda na chaga vyote, Vilowe kwa maji ya moto hasa, Chukua Foronya Hilo Loweka kwenye maji ya Moto hasa Ulifue. Godolo litoe foronya na kama Godoro lina tundu lolote Hakikisha unamwagia hapo maji ya moto.

Ukimaliza Operation hiyo kwenye kitanda siku hiyo hiyo hakikisha unatoa nguo zako zote na kuzifua kwa maji ya moto.

Kama una sofa la kitambaa hakikisha unamwagia maji ya moto kwenye pembe zote, hapo uwe mwangalifu sana maana wale jamaa ni wahuni wanaweza kula kona.

Ukimaliza kumwagia maji ya moto kitanda, nguo, Godoro na sofa. Hakikisha mwisho na nguo ulizozivaa hapo Zinafuliwa kwa maji ya moto. Zoezi hilo lifanye mara mbili ndani ya mwezi mmoja.

Hao kunguni wote watapotea na katu hutawasikia ndani kwako.
Bila ya kufanya hivyo mzee jiandae kuishi nao hao jamaa maana huwa hawaishi. Unaweza kuwapoteza kwa mwezi mmoja baadae unakuta wameshafurika tena ndani.
 
Choma moto makazi yako anza upya maisha
 
kunguni ni dalili ya uchafu hakikisha mazingira yako yoote yako safi ni sawa sawa na mtu ambaye analalamikia chawa the same kuwa msafi hao watakua historia , maji ya moto sana tumia kumwaga kila mahali ikiwezekana kutwa mara tatu
 
Kunguni ni janga kubwa sana. Waliwahi kunipata miaka flani hapa , walinisumbua sana kwa kweli.

Dawa yao ambayo mm naweza kukushauri ambayo na mm ndio nilifanya nikafanikiwa..

Dawa yao ni kuhama kabisa bila kitu chochote. Oga, toka wewe mwenyewe, hama hiyo nyumba. Usibebe chochote. Narudia tena, usibebe chochote.

Kunguni nadhani wanahisiana na mambo ya shirki
 
Habari wana JamiiForums hope wote mpo poa ndugu yenu nina mabalaa apa ni mwez wa tatu huu cjalala kwa raha nimevamiwa na kungun hata cjui nifanyaje.

Balaa lilianza kama miezi mitatu iliopita nilikuwa nalala kwenye godoro ambalo halina foronya nikavamiwa na kungun nikawa silali vizuri nikaamua kununua foronya km zile za kwenye makoch ya magar ila kubwa enough kwa kufunika godoro hali ikaisha nikawa nalala raha mustarehe sasa sijui imekuwaje.

Kunguni wakajipanga sasa hivi foronya ipo lkn wanakuja juu sijui hata wanapita wapi nikawa najikuna usiku mzima nikaona isiwe kesi ngoja nikafue mashuka na foronya na godoro nikatoa nje lkn wapi hali ni ileile.

Nikasema ngoja nipige pas lakini mashuka bado jamaa wapo nikaenda kununua dawa moja hivi ya unga niliambiwa ni nzur nikamwaga unga kwenye godoro kitanda kizima kila kwenye tundu lakini hali bado tete nalala kwa shida yaan usiku imekuwa km series ya kujikuna kila siku niwaua kungun kwa kuwabinya watatoa harufu moja matata lkn wapi nimegundua kuna kungun wengine ni wadogo mno ivo ukifeel tu unawasha basi jua upo apo karibu utafeel anavyotembea.

Sasa naombeni mnisaidie nifanyaje
Halafu mtu kama huyu kesho anaandika uzi wa nilivuta mtoto gheto nikachakata mbususu mpaka saa nane usiku, halafu nikapitiwa na usingizi mzito hadi asubuhi!
[emoji23][emoji23][emoji23]
Natania tu!

Hivyo viumbe huwa vina mbinu tofauti! Usiombe ukavamiwa na jeshi la nchi kavu la hao viumbe! Utalia na kusaga meno!!
 
Kunguni ni janga kubwa sana. Waliwahi kunipata miaka flani hapa , walinisumbua sana kwa kweli.

Dawa yao ambayo mm naweza kukushauri ambayo na mm ndio nilifanya nikafanikiwa..

Dawa yao ni kuhama kabisa bila kitu chochote. Oga, toka wewe mwenyewe, hama hiyo nyumba. Usibebe chochote. Narudia tena, usibebe chochote.

Kunguni nadhani wanahisiana na mambo ya shirki
[emoji23] [emoji23]
 
Kama ni kitandani..hakikisha godoro liwe na kover kisha toa vitu vyote nje...

Wagia maji ya moto kila pahali uwalipojificha..narudia tena maji ya moto kila kona unayoamini wapo.

Vitu ambavyo haviwezi mwagiwa maji ya moto..vitupe na choma moto kabisa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bado huwajui kunguni ndugu yangu.

tena nyinyi mabishoo unakimbia nyumba unawaachia.
Hawajui kunguni,Wala haihusiani na uchafu Wala usafi!Yeye ajichanganye tu aegemee sehemu mayai yalipo halafu arudi home!Wakianza kufyatuliwa ndio atajua hajui!
 
Back
Top Bottom