Naweza kuoa mwanamke kutoka nyumba alipooa kaka yangu?

Naweza kuoa mwanamke kutoka nyumba alipooa kaka yangu?

Cachondo

Senior Member
Joined
May 6, 2019
Posts
144
Reaction score
139
Habari za muda huu wana JF!

Niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa kinavyojieleza hapo.

Nimempenda mdogo wake na mke wa kaka yangu. Je naweza kuoa?

Kimaadili imekaaje hii?

Msaada tafadhali.

1620802384304.png

 
Kimaadili inategemea na kabila lenu na la kwa huyo binti...ila sioni tatizo.

Muhimu...mkubaliane pande zote....(haswa kaka yako aliyetangulia kuoa huko...halafu yeye atakusaidia ukipeleka maombi ukweni)

Babu yangu alifanya hivi na kaka yake(babu mkubwa), miaka hiyo utaratibu wa kuoa mtu wa kijiji/mji... kimoja/mmoja ulionekana bora zaidi.

Kulikuwa hakuna kujichanganya kama sasa...
 
Inategemea na utamaduni wa jamii husika.

Kuna baadhi ya Koo na Makabila huruhusiwi kuoa shemeji yako na ni mwiko, maana yake ni kuwa Ndugu yako akishaoa mahali nyie wengine mnabaki kuwa familia tu na huruhusiwi kuoa.

Ila pia kuna baadhi ya Koo na Makabila mna ruhusiwa kuoa wake kutoka familia Moja Yani wewe , kaka yako na ndugu zako wengine mnaruhusiwa kuoa Sehemu Moja au familia Moja kama wapo wadada wa kutosha na mmependana kweli.

Cha Msingi fatilia au uliza KWA wazee kama inaruhusiwa then take action
All the best.
 
Habari za muda huu wana jf!

Niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa kinavyojieleza hapo.

Nimempenda mdogo wake na mke wa kaka yangu. Je naweza kuoa??

Kimaadili imekaaje hii?

Msaada tafadhali
Wewe inaonekana unaishi kwa kaka yako pamoja na huyo mdogo mtu na kwa sababu wewe ni domo zege na unapenda vya kunyonga ukaamua kuchekacheka na yeye akachekacheka mkajikuta mmeduuu, yaani hiyo inaitwa hakuna kutongoza... Toka nenda kaanze maisha ya kujitegemea utaona mali mpya sokoni acha kudowea hapo home kwa bro wako.
 
Naiona, nanunua, naonja, nakunywa.....
Utanifungiaje tu huko kwenye mfuko sijaiona, ukiniwekea whitedent badala ya soda!
Unajua hata Mussa aliiona nchi ya ahadi ila hakufika
 
Back
Top Bottom