Naitwa Ododi 35yrs Mkazi wa Kimara Korogwe. Nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 nimebahatika kupata mtoto 1 ambae anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa na kuja kwenye hii dunia yetu ukiachana na wengine 7 ambao wapo kwenye ulimwengu mwingine.
Ilipoanzia fungua kiungo
Sehemu ya kwanza
---------
Baada ya kutoka hospital tulirejea nyumbani, na maisha yetu yakaendelea kama kawaida, nikaendelea kupigwa matukio kila siku, nikayumba sana kiuchumi. Alikuja mzee mmoja wa kisukuma huwa na fahamiana nae kwa muda akaniambia niende nyumbani Niliko zaliwa kweli nilifanya hivyo.
Nikiwa nyumbani nilipelekwa sehem na uncle wangu, nikakaa pale kwa muda wa siku nne nikiwa naendelea na visomo, kuna Bibi alikuja nakunambia mitihani yote inatokana na upande wa mwanamke ubabani kwao wanamambo mazito kidogo, Basi mimi nilimpa taarifa muhusika nikaomba aongee na wazazi wake wajue namna yakumsaidia.
Nilipo rejea tena nyumbani hakukua na afadhali mwanamke bado aliendelea kukabwa daily, siku moja wife alikua anaumwa ni kawanae home tumekaa sebuleni nikaona kabadilika anajaa kama kapuliziwa upepo, akaanza kuongea huku akisaga meno, akanishika mkono kwa nguvu nakunambia kama mimi jeuri atanigongesha nyoka, akasisitiza huyu mwanamke ana kiti chake kuzimu ni muache ambebe. (Pepo linaongea)
Kiukweli sikuwahi pata hofu kama siku hiyo, nikaanza kutafuta msaada sasa, ni kawa nawaza nikigongeshewa nyoka itakuwaje si ndo napotea mimi, nilikimbilia kwa shekh mmoja Ilala nikafanyiwa visomo akanipa na dawa zakutumia siku kadhaa upepo ukatulia kidogo.
Mungu akafanya wepesi nikajishikisha sehem tena kazi baada ya kukaa bench sana, baada ya mwezi mmoja kazini nikapata dili nono life likachenj nikafukia fukia mabonde yote, kama unavyoelewa ukikaa mtaani bila kazi kwa muda sana na maisha yetu ya Dar, kama ni thamani zako utajikuta umeuza kama si kuweka bondi ili maisha yasogee.
Ghafla kuna siku nilikuta wife kaandika ujumbe kwenye karatasi na kachora kile kitu ambacho huwa anakiona, nilipiga picha nikamtumia mkwe kwa Whatsp! Wiki jana usiku ule ule na kusema inatakiwa binti yao afanyiwe visomo, nilipo mpatia mama mkwe lile karatasi alilochora mwanae ghafla niliona kabadilika anaunguruma kama mdudu akajitupa chini kama vile gorikipa anadaka mpira, akaanza kujigeuza ile style mamba akiuma kitu Alikua nikama anapigana na kitu tusichoona ikawa taflani pale ndani.
Basi nikatulia nashangaa kama movie, mpaka baadae kulivyo tulia, ndugu wa mwanmke wote wako pale na Baba mkwe akadai kuna sehem tunaweza saidiwa kama najiweza nimpeleke mke wangu. Nikaona sawa, siku inayofuata nika tengeneza mazingira yakutoka kazini Ijumaa mapema ili ni safiri na Jpili nirejee mzigoni.
Ijumaa imewadia niko mzigoni napambana nikaomba kumuona HR nikamueleza nina mgonjwa nyumbani na hakuna mtu wa kunisaidia nimepigiwa simu kazidiwa alinielewa na kusema nimuone mtu anishikie kipengele changu, nikachomoka ilikua saa sita mchana nikaenda home fasta nikampitia wife tukaruka mkoani.
Tulifika pale jioni tuka tafuta sehem yakulala asubuhi tukawa kwa mwalimu akanipa mazoezi yake akasema tatzo dogo ni Jini mahaba akadai atampatia dawa litatoka fasta na mimba ata shika vizuri na itakua. "Waswahili wanasema uongo wa mganga nafuu kwa mgonjwa" Ila sisi kwetu ilikua tofauti.
Ratiba yetu kisomo ilikua saa 8 mchana lakini wife ghafla akaanza ku bleed, na masheikh hawafanyii mtu hilo zoezi akiwa kwenye siku zake. Nikamuelekeza sheikh akanambia ni hilo dudu linavuruga tiba nimuachie yeye atajua nini chakufanya, Basi alipambana awezavyo Jpili tukarejea usiku Dar.
Inaendelea......
Kusoma kilichoendelea fungua kiungo
Sehemu ya tatu