Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
jina lako tu ni jiniNaitwa Ododi 35yrs Mkazi wa Kimara Korogwe. Nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 nimebahatika kupata mtoto 1 ambae anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa na kuja kwenye hii dunia yetu ukiachana na wengine 7 ambao wapo kwenye ulimwengu mwingine.
Najua unaweza usinielewe nikisema ulimwengu mwingine kuna watoto 7, ndio ninao si uongo ila hili sijambo nataka mnisaidie mawazo kwa leo.
Tuendelee na Mada tajwa.
Nia ya kuweka maandishi haya hapa chini ni vile nimekua nikipitia magumu mengi mimi pamoja na mke wangu na sasa naona mtoto pia anapitia shida nyingi, mke wangu amekua akiteswa sana na Kiumbe cha ajabu, amekua akikiona "fluently" Kikiwa na mapembe kama mbuzi kifupi ni kiumbe ambacho kina tisha sana, Ni kimekua kikimtesa, kumkaba, kumuingilia kivyovyote kikitaka, kinamfanya awe mgonjwa malanyingi, amekua hana nafasi ya kuwaza na kufikilia vyema.
Tatzo lilianza kabla ata sija funga nae ndoa, nakumbuka kuna siku nilimuacha nyumbani kwangu nikaenda kazini, ilipofika saa nane mchana alinipigia simu akilia sana, ikanibidi kurudi home. Nilipofika nilimkuta kalala chini hawezi ata kugeuka, alinambia kuna kiumbe cha ajabu kimemfata nakumbuluza nyumba nzima, amehangaika sana kuamka kashindwa lakini alikua macho anakiona na anasikia watu nje wakiongea nakupita ila pamoja na kupiga kelele hakuna alie sikia.
Mke wangu aliniita kwa majina yangu, na akasema alivyo kua akiona kipindi yule mdudu akimbuluza pale ndani ni kama amevunja vyombo vyote na TV, nikamjibu hakuna kitu chochote kilicho vunjika kila kitu kipo kama nilivyo acha asubuhi, Mke wangu aliinuka na kukaa kama dakika 20 bila kusema kitu, baadae akanambia anahisi maumivu makali sana kwenye mbavu, mgongoni, shingoni na mikononi.
Nilimvua nguo aliyo kuwa kaivaa juu kuangalia hizo sehemu anazopata maumivu, niliona mikwaluzo ya kucha alama za vidole, na zimevia damu sehem hizo zote, kiukweli sikuelewa nikamtafutia tu dawa za maumivu nikakaa kimya, ila cha ajabu usiku wake kile kiumbe kikaja tena, this time kilikua kinaongea ila mimi sikioni kikiniomba ni mpatie mwanamke wangu then chenyewe kinipe utajiri na mali nilikataa na nilisikia kikiondoka kinalia.
Ikapita muda maisha yakaendelea mpaka nikaja muoa huyu bibie, Safari ya ndoa haikua nyepesi nilipitia wakati mgumu sana kufanikisha zoezi la ndoa, matatizo ndo yakaanza mimba zinapotea juu kwa juu, Lile dudu likaanza mambo yake, mke akawa hawezi baki na nyumba itambidi akae nje mpaka nirudi na nikirudi hawezi enda kulala mpaka twende wote chumbani, nikama likawa linataka kumpa uchizi.
Siku moja kuna rafiki yangu akanipa wazo nijaribu kumtafutia Tiba kwa masheikh wa Pemba. Nikaomba likizo kazini ili niweze mtibia mke wangu, kazini nikapewa siku7 nikaona sawa, nikatafuta ndege mpaka Pemba mimi na mke wangu ili akafanyiwe visomo wamtoe huyo mdudu.. Mmh ndugu zangu ndo kama nikawa nimeenda kuwasha moto kwenye petrol station.
Visomo viliisha tuka rejea Dar es salam, Mambo yakawa mabaya zaidi, lile dudu ndo likaanza mkaba malanyingi kuliko mwanzo, sikukata tamaa nikaendelea kuhangaikia kwa mafundi mbali mbali ambao walidai wanaweza nisaidia mikoani huko bila mafanikio. Akiba yangu ikaanza kupungua kwa kasi sana sikumaliza mwezi kazini ni kapigwa chini.
Nikarejea sasa kukaa bila kazi hali ikawa mbaya sana, ilikua 2018 nilifedheeka sana kama mnavyoelewa maisha ya mjini ukiwa nacho alafu ghafla kikakata. Nikapata insomnia kwa muda maana nilikua silali usiku, mke wangu anaweza anza piga kelele anaona vitu mimi sioni usiku wamanane.
Usiku anapigakele za kuogopa vitu ambavyo mimi sioni, akidai amezungukwa na watu wa ajabu pale tulipo lala huku akijificha mgongoni kwangu, anadai kuna kitu wanamtoa tumboni anapiga kelele analia ni msaidie, imagine sioni chochote nabaki kama zuzu sielewi naanzia wapi, kuna muda alilia sana akasema wanamuuwa, alinistua sana kuangalia vizuri naona damu kitandani, nilipomwambia damu zina kutoka alipiga kelele moja na akazima.
Nilipata hofu nilipiga simu kwao nikawaelekeza juu ya yanayo endelea kwa mtoto wao, nilimkimbiza Botch Hospital alivyochekiwa Daktari akadai alikua na mimba inaonekana imeharibika.
ITAENDELEA
Kusoma muendelezo fungua kiungo
Mimi sio punguani na kama unaona ushauri wangu hauna mshiko basi toa ushauri mbadala.Wewe huyo Yesu alishawahi kukusaidia kukutoa majini au umekariri?
Mwenzako ana matatizo halafu wewe ulivyo punguani unamshauri mtu aende kwa matapeli kama Gwajiboy, Zumaridi..etc? Uko vizuri kichwani?
Pole sana japokuwa kuna watu watakubeza na kukataa baadhi ya mambo kwa upopoma wao wa kutokujua ulimwengu wa pili upoje lakini kulingana na maelezo yako huyo ni jini mahaba,na jini mahaba ni jini ambaye ana nguvu sana hasa akiwa ndani ya ukoo au uliyewekeana maagano nae..Kama ni jini mahaba wa vipengele hivyo viwili huyo hawezi kutoka mzee hata ufanye nini utadanganywa tu nenda kwa yesu mara kwa masheik atatulia tu baada ya muda atarudi na makali mara mbili yake trust me!! Ni heri umuache tu huyo mwanamke ana maagano aliyoyaweka huko nyuma tayari hawezi kuishi na mwanaume so sad!! Hili jambo limewahi kuntokea hata mimi lakini si kwa namna ya mateso unayopata wewe tulifika na mke wangu hadi kwa paroko lakin mwisho wa siku hakuna kilichofanyika ikabidi niachane tu na yule binti...
Rakims
Upo dini gani mkuu?
Huyo siyo mgalatia na hawezi kuja huko mnakotaka.Wew jamaa cjajua ni dini gani ila naona tu hapo visomo na mashehe.. sasa basi nakushauri tafuta huu mwamba wa uzima YESU KRISTO hakuna tatizo lililoshindikana hapo upate tu sehemu sahihi..kua na imani..hakuna jina lingine chini ya mbingu wala popote liwezalo kuokoa zaidi yake..
Unaishi huko nini mkuu?Mambo kama haya huwezi kuyasikia Oysterbay, Masaki, Upanga au Mbezi Beach🤣🤣🤣
Sasa huko si itabidi aweke imani kwa Yesu ndipo aweze kupokea uponyaji na yeye ni imani tofauti.Mtoa mada anaonekana ni muislamu na hataki kujaribu upande wa pili wa kanisa. Ni yeye n visomo na masheikh tu. So dump
Ila huwa mnarahisisha mambo sana wakuu.Mimi nacheka sana kazi ya nusu saa,unahangaika miaka 7?
Pole
Kama unapenda kuwa huru na mateso.
Piga kura za comment, ukipata kura nyingi nenda huko.
Kama utatumia ufahamu binafsi basi jiulize miaka yote ulienda wapi...
Basi toa walau mwezi mmoja uende kule ambako haukwenda.
Asipopona basi sikio la kufa.
Kisongo tena mkuuUkitulia tu, mwisho wako hautakuwa mzuri kama utaendelea kuishi na huyo mkeo.
Mpeleke kwenye maombi;- jaribu kwenda arusha umpeleke ngurumo ya upako, kwa sababu kuna wengine hutoka nje ya nchi na kwenda pale kwa msaada.
Mimi naona watu huko badala ya kwenda na kutatuliwa shida zao kwa haraka matokeo wanakuwa watu wa kwenda kila wiki kwa imani siku watapona shida zao kutokana na zile shuhuda wanazozisikia, sasa hapo si bora umuombe Mungu wako tu nyumbani kila siku hadi atakapo kubali maombi yako.Nenda kwa Mwamposa burudoza
Mkuu sicocell ni ugonjwa wa kichawi na kigangaShida ni binti na sio nyumba.
Binti aliweka maagano au kwao binti anatoka ukoo wa kichawi,kiganga,kitemi au kichief ni rahisi kufatiliwa na roho wa chafu.
Mfano ugonjwa wa sicocell,kifafa chanzo ni uzao ukoo wa kichawi au uganga au wa kimaagano ya kichawi.
Kama nyumba ndo Ina vitimbi basi hio nyumba imejengwa juu ya madhabau ya kichawi,au zamani eneo hilo ilikuwa ni kilinge cha mganga au ilikuwa ni eneo la matambiko au ni lango la kuzimu au mmiliki wa nyumba hio ni agent wa kuzimu au ni member wa freemason ikiwemo nyumba hio imejengwa kwa pesa za shetani.
Masheikh ndio wana uelewa na hivyo viumbe.Nmetafakari andiko lako kwa umakini...Hili tatizo niulize ni kwamba masheikh peke yao ndio wanaliweza? Wao wana uspesho gani au wanatumia nini ambacho hakimkufuru Mungu,? wana tofauti gani na waganga wa kweli ambao nao wamejaliwa karama za kutibu masuala ya kiroho kama hayo, wana tofauti gani na manabii na wachungaji wa kweli waliopewa karama kutibu na kuondoa kabisa masuala mazito ya kiroho kama hayo?
Huyo huwa anaongea tu anchojisikia.Mkuu sicocell ni ugonjwa wa kichawi na kiganga
Daah karne hii ya 21
Basi sawa
Fanya study wanaougua kama hawana historia ya mganga au mchawi kwenye ukoo waoMkuu sicocell ni ugonjwa wa kichawi na kiganga
Daah karne hii ya 21
Basi sawa
Mbona yaliwaingia nguruweTiba rahisi Sana ya jini Kula kitimoto alaf pale mlangoni au chumbani week mfupa was kitimoto Kama ni muislamu kuleni kwa dawa kidogo tu na mkeo ajipake mafuta yake majini hayapendi watu wachafu kitimoto kwa imani yenu ni uchafu alaf asipake perfum ya kunukia Sana Wala manukato nyumbani kwenu anzia hapo ulishindwa nipigie uje Lushoto