Nawezaje kuishi na Mtu mwenye changamoto ya Afya ya akili?

Nawezaje kuishi na Mtu mwenye changamoto ya Afya ya akili?

Judithkaunda

Member
Joined
Aug 21, 2022
Posts
90
Reaction score
231
Habari Wana JF,

Naombeni ushauri ndugu zangu namna ya kuishi na mtu mwenye stress over.

Nimeshagundua rafiki yangu anatatizo la afya ya akili kwasababu.

Ni mtu mwenye hasira muda mwingi Hana furaha kwasababu mnaweza kukaa siku nzima usione anachekaa.
Muda mwingi analalamika hata likitokea jambo la kawaida atalamika tu.

Anamawazo ambayo hapati majibu na hakuna dalili za kupata majibu haraka.
Anamawazo hasi muda wote najitahidi kumshauri vitu vizuri.

Nafanikiwa kwa muda tu, lakini mkikutana Tena kesho hali ni Ile Ile najikuta namuonea huruma na hapo ndio naanza kujisikia vibaya kwakiasi ameanza kuniambukiza huzuni yake, Kila tukiwa pamoja najikuta Sina mzuka wa kazi, siwazi vitu vizuri najisikia kukata tamaa.

Natamani nikae na mtu mwenye mawazo yakufika mbali anipe hamasa lakini mazingira na kazi vinanilazimisha kuwa karibu nae na siwezi kumkwepa ni ndugu wa karibu na tunaishi pamoja. Natamani kumsaidia na wakati huo hali yake isiniathili.

Naombeni ushauri ndugu zangu
 
Ufahamu ndio unaomfanya mwanadamu kuwa kiumbe wa kipekee na matumizi sahihi ya ufahamu ndio vinakamilisha ubinadamu na kumtoa katika unyama wa mwituni.

Mwanadamu akijitoa katika matumizi sahihi ya fahamu zake anakuwa hana tofauti na mnyama wa porini.

Na matumizi sahihi ya ufahamu Kwa mwanadamu ni kumsaidia kuweza kukabiliana na kutatua changamoto au maswali yanayomzunguka kwenye mazingira yake na kuishi katika msawazo na wanadamu wenzake.

Mtu anapotokea udhibiti na matumizi ya fahamu zake anageuka kuwa kiumbe hatari kwani muda wowote anaweza kufanya lolote na katika mazingira yoyote bila kuwaza au kuhofia lolote.

Hivyo basi jambo la msingi ni kujiweka mbali au kupunguza ukaribu na watu wenye dalili hizo sio tu kwa kuwatenga bali Kwa faida yako huku tukiangalia namna ya kumsaidia kurudi katika hali ya kawaida.
 
Ilo asikusumbue,jioni mpige kvant ,atabaki akiimba na nakufurahi na atasahau machungu,inaonekana alipatwa na Jambo zito Sana,Sasa kulisahau utachukua muda
 
Umri wa 52 mtu bado anapagawa na ugumu wa maisha? Kwani ni kipi asichokijua.

Ninaamini katika umri huo unakuwa umepitia mengi na umeona mengi hakika unakuwa ni mshauri na mwalimu mzuri wa maisha.
 
Back
Top Bottom