Nawezaje kupata Tsh. Milioni moja?

Athalia ukiipata hiyo milioni chonde usiiweke yote huko jikon..weka kam 300k! Anza kusoma mchezo tartibu...nunua vyombo vichache wateja wakizoea uongeze...sio upike ugali kilo 3 kwasiku hujasoma mchezo..nunua vichache hela nyingine kibindoni..kila la heri
 
Asante kwa ushauri, nikipata nitaufanyia kazi, barikiwa.
 
Nikirahisi saana. Sema kwa sasa kunachangamoto maana raw materials zkmefingwa kwa sabab ya Korona. Ukweli nikwamba inategemeana na imannyako juu ya michezo ya kinahatisha yaan Sports betting. Ningelkuwa ni mimi hapo mapema saana unalifuaya hilo jiko. Beti kunawatu walioko makin na smart haiishi wiki japo anaweza akapotezamo lakin lazma awapige tena huenda ikawa zaidi ya unayoitafta cha msingi uwe na kianzio....MCHANGO WANGI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh kubet hapana mkuu. Asante.
 
Mkuu ulifanyeje nami nina shida ya 3 milioni kabla ya june
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nimepita hapo ulipo, na kwa sababu ya passion niliyokuwa nayo nikaipata, watu ni wagumu sana hasa wanaposikia kwamba ni kwa ajili ya biashara, maana who knows kama itafanikiwa!

Mwombe Mungu, huku unaendelea kuwaza na somehow atatokeza na utafanikiwa kuupata huo Mtaji, ushauri wangu: Usilazimishe, na kuwaza oh jiko likienda ndo basi tena, au oh nikipata ndo maisha yamenyoka, ukilikosa pia mshukuru Mungu.

Kuna vitu nimewahi kulazimisha nikapata vikanipelekea kwenye uharibifu, kuna vitu nimewahi kukosa na nikapata vitu bora zaidi Baadae! Mungu akupe hekima na akupe vitu sahihi kwenye maisha yako!

Huu ni ushuhuda wa kweli, Nina shemeji yangu mmoja, wife wa rafiki yangu sana, Mme wake ali paralyse, sasa tulikuwa twaishi mikoa mbalimbali, so nilikuwa nawasiliana na shemeji yangu mara nyingi!

Kuna mpango wa cheti cha shemeji yangu alikuwa anasaiwa 1m hivi kupata ili aanze kazi, kweli baada ya mawasiliano nikamwambia nitakupa, ila ukianza pata mshahara urudishe: 20,000 kila mwezi.

Nikamtumia 1m - sikuongea na mme wake maana alikuwa kaparalyse, na hawezi ongea vizuri..... baada ya kumpa mawasiliano yakafa, ni kawa na wasiwasi na mshikaji wangu kapatwa na nini?

Nikapanda Bus kwenda muona, dah..... baada ya kumpa mwanamke hela, kamtelekeza jamaa, hakumwaga wala kumwambia mtu, then jamaa akafarariki........

Toka siku hiyo, kila wakati mtu akinambia hela, nakumbuka kaburi la mshkaji wangu na kwamba Siku pata hata fursa ya kuongea naye au kumwaga au kwenda kwenye mazishi.....

Sisemi wewe ni mtu mbaya, Hapana, nasema unaweza usipate msaada maana watu wamepitia mambo mengi, wewe mwamini Mungu, mwombe Mungu na Mungu ndiye atafanya usaidike kama wewe ni wa kusaidika
 
Asante mkuu nimekupata vyema, ubarikiwe kwa ushauri wako.
 
Umolewa? Umri wako? Mkoa uliopo? Hiyo Biashara una uzoefu nayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya chochote uwezacho ukutane na hawa viongozi wa kisiasa utasaidika
Jr[emoji769]
 

Mungu akubariki sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…