Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Kuna kanuni yangu moja nimeitunga ambayo naitumia maishani kwamba "I'd rather suffer my own consequences than someone's."
Yaani ni bora niumie kwa maaamuzi yangu mwenyewe kuliko kwa maamuzi ya mtu mwingine sababu nitaumia mara mbili na lawama juu.
Pili mzazi hatokuwepo milele sasa kama siku hayupo nani atakuamulia na nani utamlaumu mambo yakienda kushoto?

Mtoto wa kiume sio mtu wa kupangiwa itafikia hatua ni lazima ajifunze kuwa na misimamo na maamuzi binafsi na kama ukikosea basi utakula consequences zako mwenyewe na hakuna wa kumlaumu.

Sasa kama unataka misimamo basi tambua kamwe kwenye Misimamo hakuna Amani.
 
Nilisoma course ambayo baba yangu hakuitaka kabisa ndoto zake zilikuwa nisomee kitu kingine lakini nilishikilia msimamo ingawa ni mtoto wa kike nikasoma nilichokitaka. Wakati mwingine mtu mwingine hawezi kukuelewa lakini fuata unachokiamini.

Kwa upande mwingine wazo la mzee ni zuri sana anataka usome famasia uwe mjasiriamali kama unavyotaka. Kwanini hukusoma famasia moja kwa moja ukaachana na nursing?
 
Asante sana mkuu.
Tatizo ni kwamba hataki kuelewa.
Binafsi ninachotaka ni kusimamia malengo yangu.
Lakini Kila nikifikiria matokeo yake yatakavyokuwa inanipa wakati mgumu sana.
Ndio Maana nataka Kama Kuna mbinu ya kumwelewesha bila kumkwaza nifanye hivyo kwasababu mwisho wa siku nitafuata tu maamuzi yangu no matter what!

yNini unahitaji kwenye maisha yako??kumfurahisha mzazi au kutimiza malengo yako???kwenda kosomea course ambayo hukutaka ulifanya kwaajili yake,ukimaliza nursing fanya Jambo kwaajili yako,wazazi wanatupenda Sana pia nao kama watu wengine Wana mtazamo tofauti kuhusu maisha ni Nini...atakua na maoni tofauti kuhusu mwanamke unaetaka kumuoa,ili kumfurahisha utafanya kila kitu???
 
Kuna kanuni yangu moja nimeitunga ambayo naitumia maishani kwamba "I'd rather suffer my own consequences than someone's."
Yaani ni bora niumie kwa maaamuzi yangu mwenyewe kuliko kwa maamuzi ya mtu mwingine sababu nitaumia mara mbili na lawama juu.
Pili mzazi hatokuwepo milele sasa kama siku hayupo nani atakuamulia na nani utamlaumu mambo yakienda kushoto?

Mtoto wa kiume sio mtu wa kupangiwa itafikia hatua ni lazima ajifunze kuwa na misimamo na maamuzi binafsi na kama ukikosea basi utakula consequences zako mwenyewe na hakuna wa kumlaumu.

Sasa kama unataka misimamo basi tambua kamwe kwenye Misimamo hakuna Amani.
I couldn't have said it any better....

👏👏👏
 
Kwani ufamasia siyo Ujasiriamali ?? Ajira imewekwa reserve kwa ajili yako ili ukimaliza "ujishikize" ??
Mkuu nisichokubaliana nacho Mimi ni swala la kurudi Tena chuo kusoma diploma nyingine!
Sijakataa kama hata Pharmacy ni ujasiriamali.
Sitegemei urahisi au mteremko wowote katika kupata ajira.
 
Km utafanya km ulivyopanga kufanya ukimaliza io diploma kwa vyovyote vile mzee atakususa kwa io jiandae kusaikolojia mapema

I mean kuanzia kodi ya nyumba, mavazi na chakula ujitegemee maana mzee atakataa kukupa huduma yoyote kati ya hizo hpo juu

Kwa hiyo mdogo wangu jiongeze ukiwa hapo hapo chuo kwa kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ambazo zitakusaidia mzee akishakususa

Cha muhimu kuliko vyote we fanya unachoona muhimu kwako, kwa sasa mzee hawezi kukuelewa ila atakuja kukuelewa km utafanikiwa kwenye huo ujasiriamali wako.
 
Asante Kwa mchango wako mkuu.
Lakini kitukimoja ambacho hatujagusia hapa ambapo ni kwamba kama lengo la kurudi chuo ni Ili niwe na PHARMACY, it means inabidi niendelee Hadi degree which means I have to spend seven more years darasani, (three years diploma, four years degree!)
Na binafsi siko tayari kuendelea kukaa miaka yote hiyo darasani Tena!
Isitoshe si kitu ninachopenda
Msikilize mshua ana malengo mazuri kwako....!!

Huo ujasiriamali unaoutaka kuufanya utaufanya ndani ya afya!!(pharmacy)
 
Kwanza pole sana kwa kuwa na wazazi wenye uelewa mdogo kuhusu uhuru wa mtoto kufata ndoto zake so long ni njia sahihi.. Pili baba yako alikosea toka Mwanzo kukutoa toka kwenye Njia ya masomo ya biashara na akakuforce usomee mambo ya science akiamini ndo kwenye Ajiraa pole sana lakini Ulifanya kosa kubwa sana maana kuajiriwa siku hizi haijalishi umesomea nini hakuna hajira isipokuwa hadi leo NIMESHUHUDIA washkaji zangu waliosoma masomo ya bisahara wakimaliza na Kuajiriwaaa faster hasa kama walikuwa wanaperfom vizuri darasani mfano mzuri ni Mdogo wangu kamaliza masomo ya biashara hama Miezi sita nyumbani Kashapata kazi tema serikalini... Tuliosoma masomo ya science hadi leo tupo private tunaunha unga so haya mambo sio ya Kukariri kabisa mdogo wetu alieonekana anapotea njia leo yupo serikalini mapema tu na huko ana nafasi ya kupanda cheo na kulipwa vizuei zaidi.

Tatu kosa ulilofanya mwanzo kufata ndoto za mzazi juu yako badala ya Ndoto zako Usilirudie tena sasa Huwezi soma diploma nursing leo umemaliza urudi ukasome Diploma ya pharmacy kisa tu eti famasi unaweza jiajiri Alokwambia kujiajiri famasi inahitaji Diploma nani??? Mtaji huna hata usome mpaka masters huwezi jiajiri kamwe... Labda kama baba yako atakupa mtaji wa kufungua famasi ukimaliza diploma na bado itakuwa haijakusaidia maana itabdi Umlipe mfamasia ili kuendesha famasi yako so Diploma haina msaada direct kwenye kupunguza Cost za kuendesha famasi.

Nne USIRUDI KUSOMA FAMASI. achana na mambo ya kuteseka kutimiza ndoto ya mazazi wako ushasoma nursing inatosha sasa Fata ndoto zako achana na Upuuzi wa kusikiliza ujinga anaokwambia mzee wako wakati hali halisi haipo Hivyo kabisaaa ukikaa vibaya Siku atakwambia usisome famasi soma Diploma ya Udaktari na wew utababaika.. Ur old enough kusimamia misimamo yako umri unaenda acha kuishi ndoto za mzazi wako akikasirika akasririke tu.

Mwisho pole sana ila KUWA NA MSIMAMO.
Kweli kabisa mkuu maisha hayana formula
Ninachokiona hajapata taarifa sahihi kuhusu haya mambo.
Na Mimi mwisho wa siku nitafanya tu kile nilichoamua bila kujali chochote, ninachotafuta ni kujua kama ipo mbinu naweza kutumia ku make peace with him Ili hata nikija kufanya maamuzi iwe ni Kwa amani.
Ikishindikana sitakuwa na jinsi atanisamehe tu!
 
Mawazo yako umeyapata kwa wahamasishaji? Ukidhani biashara rahisi eeeh. Msikilize dingi maliza ukibahatisha ajira ajiriwa kusanya mtaji then fanya biashara ukiwa ajirani then ukiona unajiweza quit the job. Otherwise usidhani mtaani parahisi
Sitegemei urahisi wowote katika maisha ya mtaani nipo tayari kupambana na changamoto yoyote Ile itakayokuja mbele yangu Ili kutimiza malengo yangu.
Na pia sidhani kama Kuna ubaya katika kuhamasishwa Ili mradi isiwe nje na uhalisia wa maisha.
 
Japo sijui kwa nini unaona kama ukiwaambia wazi wako juu ya malengo yako mtapishana kauli? Kwa sababu huwenda mzee wako anakuwekea mipango kwa sababu haoni unamipango gani.

Hivyo kwa kuwa bado hujamaliza kusoma hebu jaribu kumueleza mipango yako halafu uone muitiko wake, hilo mosi.

Pili kwa kuwa baada ya kumaliza kutakuwa na muda fulani wewe anza kuyaendea hayo unayoyaamini kwa vitendo, na kama utakuwa umeonyesha uelekeo itakuwa ni rahisi hata kuwashawishi wazazi, kuliko maneno tupu.
Asante sana Kwa ushauri mkuu
 
Sitegemei urahisi wowote katika maisha ya mtaani nipo tayari kupambana na changamoto yoyote Ile itakayokuja mbele yangu Ili kutimiza malengo yangu.
Na pia sidhani kama Kuna ubaya katika kuhamasishwa Ili mradi isiwe nje na uhalisia wa maisha.
Kila la heri, ila usirudi namalalamiko nextime
 
Kuna kanuni yangu moja nimeitunga ambayo naitumia maishani kwamba "I'd rather suffer my own consequences than someone's."
Yaani ni bora niumie kwa maaamuzi yangu mwenyewe kuliko kwa maamuzi ya mtu mwingine sababu nitaumia mara mbili na lawama juu.
Pili mzazi hatokuwepo milele sasa kama siku hayupo nani atakuamulia na nani utamlaumu mambo yakienda kushoto?

Mtoto wa kiume sio mtu wa kupangiwa itafikia hatua ni lazima ajifunze kuwa na misimamo na maamuzi binafsi na kama ukikosea basi utakula consequences zako mwenyewe na hakuna wa kumlaumu.
Sasa kama unataka misimamo basi tambua kamwe kwenye Misimamo hakuna Amani.
Asante mkuu nimepata kitu kutoka kwako.
 
Hongera sana.
Mwanzo Hii kozi tuli apply lakini tulikosa nafasi nikapata Hii ya nursing.
Natumaini unavuna matunda ya kusimamia kile ulichoamini Kwa Sasa au Bado unapambania hongera sana!
Nilisoma course ambayo baba yangu hakuitaka kabisa ndoto zake zikikuwa nisomee kitu kingine lakini nilishikilia msimamo ingawa ni mtoto wa kike nikasoma nilichokitaka. Wakati mwingine mtu mwingine hawezi kukuelewa lakini fuata unachokiamini.

Kwa upande mwingine wazo la mzee ni zuri sana anataka usome famasia uwe mjasiriamali kama unavyotaka. Kwanini hukusoma famasia moja kwa moja ukaachana na nursing?
 
Asante sana mkuu Kwa kuwa straightforward!
Ni ukweli usemayo Tena ukweli mchungu Sina budi kukubaliana nao.
Asante sana Kwa ushauri wako
nitaufanyia kazi.
Km utafanya km ulivyopanga kufanya ukimaliza io diploma kwa vyovyote vile mzee atakususa kwa io jiandae kusaikolojia mapema

I mean kuanzia kodi ya nyumba, mavazi na chakula ujitegemee maana mzee atakataa kukupa huduma yoyote kati ya hizo hpo juu

Kwa hiyo mdogo wangu jiongeze ukiwa hapo hapo chuo kwa kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ambazo zitakusaidia mzee akishakususa

Cha muhimu kuliko vyote we fanya unachoona muhimu kwako, kwa sasa mzee hawezi kukuelewa ila atakuja kukuelewa km utafanikiwa kwenye huo ujasiriamali wako.
 
Umalize diploma ya nursing halafu ukaanze tena diploma ya pharmacy? utapoteza muda bure kwa vitu visivyo na faida.
Mshauri mzee wako ukimaliza diploma ya nursing akufungulie tu pharmacy,Mimi ni medical officer nina pharmacy 3 na faida ninayopata kwa siku ni inakaribia mshaara wangu ninaolipwa.
Kwa wazo la mzee wako ni zuri sana coz ni wazazi wachache wanaowawezesha watoto wao punde wanapo maliza chuo.
Kaa chini na mzee umueleweshe vizuri pharmacy ni biashara inayolipa sana hasa ukipata location nzuri.
NB:si wote wenye pharmacy wamesomea hiyo fani
Asante sana mkuu.
Samahani naomba kuuliza, ulikuwa unamaanisha duka la dawa muhimu au?
Pia hongera sana
 
Back
Top Bottom