Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Baba yako ana reality yake katika maisha na wewe una reality yako pia. Kama baba yako ni mtu ambae hazikilizi kabisa maoni ya mtu basi mtaendelea kupambana nae mpaka uende njia anayotaka

Je una biashara tayari ambayo ina kipato kizuri? Kama ndio basi wazazi wengi huwdza kusapoti mawazo ya watoto kwa sababu hii kwa kuwa tayari wanaona kitu kinaendelea.

Kama hauna biashara yenye kipato basi ni muhimu kuwa mpole huku ukianza mchakato wa kujenga biashara yako. Baba yako anachoogopa ni kugharamikia kitu ambacho hakina future ila ukimuonesha tayari una uwezo wa kujenga kitu inakuwa rahisi zaidi kukusaidia.

Kumbuka path yoyote utayochukua haikuzuii wewe kutokuwa mfanyabiashara. Ni kuchukua hatua tu na utaweza kufika malengo yako kwa chochote utachosomea.

Mie mwenye baba kama wako niliamua kufanya maamuzi magumu ya kuacha shule kisha kutoa taarifa ila tayari nilikuwa na biashara na tayari nilikuwa na kipato kizuri tu. Ilikuwa msala mkubwa ila muda ulivyoenda na mshua kuona naishi vizuri hasira zikaisha bado nasonga mbele kitaa mpaka sasa. Usijaribu hili kama huna biashara, kipato kinachoeleweka na akiba ya kukutosha mwaka mzima kuishi mtaani bila kazi.
 
Habari zenu Wana Jamiiforums.
Mimi ni kijana ambaye umri wangu upo kwenye mid 20's.
Nipo chuo kimoja hapa nchini ambapo nasomea kozi ya uuguzi.
Nia na madhumuni ya kuleta Uzi huu ni kuomba ushauri kuhusu ni jinsi Gani ninaweza kushikilia msimamo wangu kuhusu Nini nataka kwenye maisha yangu bila kuwafanya wazazi wahisi kama nimewadharau.
Iko hivi...
Baba yangu ndiye anayenisomesha mpaka sasa, hivi karibuni nilipokuwa likizo ya kumaliza mwaka wa pili kuingia mwaka wa tatu wa masomo hapa chuoni Mzee wangu alinishauri kwamba nikimaliza kozi Hii ya nursing (diploma) nirudi Tena chuo kusomea Tena kozi ya pharmacy miaka mingine mitatu (diploma). Hoja yake ni kwamba nikifanya hivyo baadaye naweza kujiajiri Kwa kufungua pharmacy yangu Mimi mwenyewe na kwamba pharmacy ni biashara inayolipa vizuri sana.
Lakini Mimi binafsi Kwa upande wangu siko tayari kufanya hivyo kwasababu malengo niliyojiwekea Mimi ni kwamba baada ya kumaliza hii diploma ya nursing nitafute ajira inishikize Kwa miaka kadhaa huku nikiwa nafanya shughuli za ujasiriamali pembeni Kisha biashara zikiwa nzuri na nikiona Nina kipato Cha kueleweka niachane kabisa na ajira ya uuguzi nijikite Moja Kwa Moja katika biashara kwasababu moyoni mwangu nawiwa kuwa mjasiriamali mkubwa tu, Maana hata hii kozi ya uuguzi ninayosomea sasahivi sikuitaka kabisa, nilipomalixa kidato Cha nne nilitaka nikasome business administration au kozi za masuala ya entrepreneurship Ili baadaye niweze kujiajiri katika biashara na ujasiriamali kwani ndoto zangu ni kumiliki kampuni yangu binafsi. Lakini Mzee wangu alipinga vikali wazo hili akisisitiza kuwa kozi za biashara hazina tija na wapo wengi wanaozunguka mitaani na vyeti vyao bila ajira miaka nenda Rudi na Wana degree kabisa.
Nilijaribu sana kumwelewesha kwamba lengo langu si kutafuta ajira Bali ni kujiajiri mwenyewe kutokana na elimu nitakayopata lakini hakukubaliana kabisa na Mimi.
Baadaye akanitafutia vyuo vya afya na kufanikiwa kupata nafasi katika kozi Hii ya uuguzi chuo Fulani hapa nchini na Mimi Kwa kuepuka kumkwaza nikakubali kuja kusoma japo haikuwa passion yangu kabisa!
Sasa kinachofanya nije kuomba ushauri ni hiki...
Mzee wangu ni mtu ambaye anataka akiongea kitu basi ufanye kama alivyokwambia yeye, ukitaka kufanya tofauti anakuona kama mbishi, unampuuza au unamdharau!
Of course Baba yangu ni mtu mmoja mzuri sana kwasababu ana upendo wa ajabu Kwa wanae yupo tayari kufanya chochote na ku sacrifice Kila kitu Ili kutupatia kile ambacho yeye anaamini kuwa ni Bora katika maisha ni mtu mwenye upendo wa ajabu sana na familia yake na watoto wake na Kwa Hilo nimemfanya kuwa role model wangu. Shida yake ndio hiyo Moja hataki uende tofauti na anavyotaka yeye.
Mimi Kwa upande wangu siamini kama kusoma saaana ndio kufanikiwa na ninataka nikimaliza hii diploma nianze kupambana na maisha sasa lakini yeye anasisitiza kuwa diploma ni level ndogo sana Kwa maisha ya sasa. Of course inaweza kuwa kweli lakini Mimi naamini katika ndoto zangu na malengo Yangu na sitaki Tena kuendelea kupoteza muda kukaa darasani maana umri unazidi kwenda Mimi sio wa kuendelea kumtegemea mzazi Tena lakini nikimwambia hataki kabisa kuelewa.
Sasa wanajamvi shida yangu ninaomba mnisaidie nitumie mbinu Gani kumwelewesha na kumshawishi Mzee wangu akubali Mimi nifuate kile nilichojipangia katika maisha yangu lakini bila kumkwaza na kumfanya ahisi kama nampuuza au kumdharau?
Nawapenda sana wazazi Wangu sitaki kuwakwaza lakini pia sitaki kunyimwa opportunity ya kupambania malengo niliyojiwekea katika maisha na natamani pia wazazi wanipe Uhuru wa kujiamulia ninachotaka katika maisha yangu pia!
Nimepanga nikirudi home nikazungumze nae kuhusu hili lakini nashindwa kujua nitumie mbinu Gani kumuelewesha Maana najua nikishikilia uamuzi wangu tunaweza kuishia kupishana kauli kitu ambacho sitaki kitokee kwani pamoja na hayo sitaki kumkwaza.
Sasa naombeni ushauri wadau ni vipi naweza kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?
Asanteni nawasilisha.

Mtafute rafiki yake, mtu ambaye unaamini wameshibana, omba kukutana na huyo rafiki yake.

Kaa naye kwa ustaarabu na unyenyekevu mkubwa. Mpe hoja zako na malengo yako. Pia usisahau kuelezea namna unavyojisikia hususani kwamba hutaki kukorofishana na mzee, jinsi unavyomthamini na kuheshimu msaada na mawazo yake katika maisha yako.

Muombe akusaidie kuongea na rafiki yake (baba yako) kwa niaba yako. Mzee atakuita tu baadae au inawezekana asikuite ila atakuacha ufanye kinachokupa amani.

Pia muombe Mzee wako kupitia rafiki yake kwamba asimame na wewe katika jitihada zako za kutafuta maisha, asichukulie kama ukaidi bali ni njia yako ya kufikia malengo yako.

Wazazi ndivyo tulivyo, kuna wakati tunakuwa over protective na kutaka watoto waishi ndoto zetu.

Usisahau kunipa mrejesho.
 
Kama diploma tu ya pharmacy hujaifikia.. degree utaifikia lini maana bila degree huwezi kuruhusiwa "kuendesha pharmacy yako mwenyewe"
Utachukua muda sana.. bora usimsikilize mzee
 
Kama diploma tu ya pharmacy hujaifikia.. degree utaifikia lini maana bila degree huwezi kuruhusiwa "kuendesha pharmacy yako mwenyewe"
Utachukua muda sana.. bora usimsikilize mzee
Uliona wapi
 
Mkuu ubarikiwe mno! 🙏
Asante sana Kwa ushauri wako, so far wewe ndo umekuwa most relevant na nilichokuwa natarajia kutoka Kwa wadau!
Nitaufanyia kazi huu ushauri na panapo majaaliwa nitaleta mrejesho.
Asante sana.
 
Kama diploma tu ya pharmacy hujaifikia.. degree utaifikia lini maana bila degree huwezi kuruhusiwa "kuendesha pharmacy yako mwenyewe"
Utachukua muda sana.. bora usimsikilize mzee
Nadhani hatujaelewana mkuu!
Kinachofanya nisikubaliane na Mawazo yake ndio hicho kwamba kama lengo ni kumiliki pharmacy Maana yake Nina miaka mingine Saba ya kukaa darasani mitatu kutafuta diploma na Minne ya degree!
Na Mimi huo muda ninataka kuutumia kuanza kupambania malengo ambayo nimejiwekea sio Tena kukaa darasani!
 
Kwa hiyo mipango yako ya kutafuta ajira....then upate mtaji ujiajiri...inaweza chukua hata 4 years kwa upepo wa sasa ulivyo hususani ukizingatia soko la ajira lilivyo.

USHAURI WANGU.

Kama lengo lako uje kuwa mfanya biashara naona mzee wako naye analengo hilohilo. Chakufanya kaa chini na mzee wako mpe mikakati kwamba upo tayari kwenda kusoma phamarcy ili tu uje ufungue phamarcy yako na une udeal hiyo biashara. Sababu ya hilo mwambie nikimaliza tu chuo sifikirii kuajiriwa naomba uniandalie mtaji ili nkkihitimu tu nifungue hiyo phamarcy . Akikubali bila maelezo mengi bhasi nenda kasome but ukiona anasitasita endelea na mipango yako na hapa hawezi kukulaumu au kugombana na wewee sababu hajafikia terms zako.

Mwisho wa kunukuu
 
Msikilize baba yako maana yeye ndio kaanza kuliona jua kabla yako.

By the way, hakuna mzazi anayemtakia mabaya mwanae.

Huu ndo ujinga wetu wakiafrica

Ndo mana kila siku tunalalamikia sekta ya afya
 
Nimekuelewa Sana mkuu.
Asante Kwa Mawazo Yako nitayafanyia kazi bila shaka.
Najua mwanzo hatonielewa lakini atakuja kunielewa baadae hakika.
Pia hongera sana Kwa maamuzi uliyochukua na Mimi Niko nyuma Yako mkuu
Baba yako ana reality yake katika maisha na wewe una reality yako pia. Kama baba yako ni mtu ambae hazikilizi kabisa maoni ya mtu basi mtaendelea kupambana nae mpaka uende njia anayotaka

Je una biashara tayari ambayo ina kipato kizuri? Kama ndio basi wazazi wengi huwdza kusapoti mawazo ya watoto kwa sababu hii kwa kuwa tayari wanaona kitu kinaendelea.

Kama hauna biashara yenye kipato basi ni muhimu kuwa mpole huku ukianza mchakato wa kujenga biashara yako. Baba yako anachoogopa ni kugharamikia kitu ambacho hakina future ila ukimuonesha tayari una uwezo wa kujenga kitu inakuwa rahisi zaidi kukusaidia.

Kumbuka path yoyote utayochukua haikuzuii wewe kutokuwa mfanyabiashara. Ni kuchukua hatua tu na utaweza kufika malengo yako kwa chochote utachosomea.

Mie mwenye baba kama wako niliamua kufanya maamuzi magumu ya kuacha shule kisha kutoa taarifa ila tayari nilikuwa na biashara na tayari nilikuwa na kipato kizuri tu. Ilikuwa msala mkubwa ila muda ulivyoenda na mshua kuona naishi vizuri hasira zikaisha bado nasonga mbele kitaa mpaka sasa. Usijaribu hili kama huna biashara, kipato kinachoeleweka na akiba ya kukutosha mwaka mzima kuishi mtaani bila kazi.
 
Mkuu ubarikiwe mno! [emoji120]
Asante sana Kwa ushauri wako, so far wewe ndo umekuwa most relevant na nilichokuwa natarajia kutoka Kwa wadau!
Nitaufanyia kazi huu ushauri na panapo majaaliwa nitaleta mrejesho.
Asante sana.

Karibu
 
Kwa hiyo mipango yako ya kutafuta ajira....then upate mtaji ujiajiri...inaweza chukua hata 4 years kwa upepo wa sasa ulivyo hususani ukizingatia soko la ajira lilivyo.

USHAURI WANGU.

Kama lengo lako uje kuwa mfanya biashara naona mzee wako naye analengo hilohilo. Chakufanya kaa chini na mzee wako mpe mikakati kwamba upo tayari kwenda kusoma phamarcy ili tu uje ufungue phamarcy yako na une udeal hiyo biashara. Sababu ya hilo mwambie nikimaliza tu chuo sifikirii kuajiriwa naomba uniandalie mtaji ili nkkihitimu tu nifungue hiyo phamarcy . Akikubali bila maelezo mengi bhasi nenda kasome but ukiona anasitasita endelea na mipango yako na hapa hawezi kukulaumu au kugombana na wewee sababu hajafikia terms zako.

Mwisho wa kunukuu
Wazo zuri sana Hili mkuu Asante Kwa ushauri.
 
Nawapenda sana wazazi Wangu sitaki kuwakwaza lakini pia sitaki kunyimwa opportunity ya kupambania malengo niliyojiwekea katika maisha na natamani pia wazazi wanipe Uhuru wa kujiamulia ninachotaka katika maisha yangu pia!
Simple kama baba Yako analipa Ada na ku-provide vitu vyote wakati wa masomo yako, wewe Nenda Chuo halafu ukifika huko Tafuta Hizo ajira zako unazotaka, Ukifeli ni kumwambia Mzee kwamba nimefeli/disco etc itakuwa sababu Kuu, kuliko Ajira;
Hivyo usioneshe hali yoyote ya kuonesha kwamba una utaratibu wa mambo yako.
 
Naweza kufanya hivyo lakini sitaki apoteze pesa zaidi.
I do care about him too, kumwacha anilipie ada huku nikijua kabisa nitafeli sitapenda hilo.
Zaidi ya yote sitaki kabisa kwenda chuo kusomea hiyo kozi Kwa Sasa si kitu ninachopenda.
Lakini Asante Kwa wazo lako mkuu.
 
I do care about him too, kumwacha anilipie ada huku nikijua kabisa nitafeli sitapenda hilo.
Nimesema ukifeli sio ukijifelisha!! yaan nimechukulia kwamba utakuwa umejishikiza mahali, lakini pia una ujasiriamali wako unafanya hivyo balance ya mambo yote matatu impact inaweza kuwa kubwa kwenye Masomo kuliko hayo mambo mengine mawili.
hivyo kufeli ni incase isiwe nia yako.

Kwa maelezo yako ni kwamba mzee anapendz uje kujiajiri baada ya Kusoma phamarcy wewe unataka Kujiajiri kabla; Hivyo wewe na mzee wako mna common Interest isipokuwa kwa muda tofauti hivyo kumwin kwa kitu nilichokwambia ni rahisi sana.
 
Back
Top Bottom