Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Kuna kanuni yangu moja nimeitunga ambayo naitumia maishani kwamba "I'd rather suffer my own consequences than someone's."
Yaani ni bora niumie kwa maaamuzi yangu mwenyewe kuliko kwa maamuzi ya mtu mwingine sababu nitaumia mara mbili na lawama juu.
Pili mzazi hatokuwepo milele sasa kama siku hayupo nani atakuamulia na nani utamlaumu mambo yakienda kushoto?

Mtoto wa kiume sio mtu wa kupangiwa itafikia hatua ni lazima ajifunze kuwa na misimamo na maamuzi binafsi na kama ukikosea basi utakula consequences zako mwenyewe na hakuna wa kumlaumu.

Sasa kama unataka misimamo basi tambua kamwe kwenye Misimamo hakuna Amani.
 
Nilisoma course ambayo baba yangu hakuitaka kabisa ndoto zake zilikuwa nisomee kitu kingine lakini nilishikilia msimamo ingawa ni mtoto wa kike nikasoma nilichokitaka. Wakati mwingine mtu mwingine hawezi kukuelewa lakini fuata unachokiamini.

Kwa upande mwingine wazo la mzee ni zuri sana anataka usome famasia uwe mjasiriamali kama unavyotaka. Kwanini hukusoma famasia moja kwa moja ukaachana na nursing?
 
Asante sana mkuu.
Tatizo ni kwamba hataki kuelewa.
Binafsi ninachotaka ni kusimamia malengo yangu.
Lakini Kila nikifikiria matokeo yake yatakavyokuwa inanipa wakati mgumu sana.
Ndio Maana nataka Kama Kuna mbinu ya kumwelewesha bila kumkwaza nifanye hivyo kwasababu mwisho wa siku nitafuata tu maamuzi yangu no matter what!

 
I couldn't have said it any better....

👏👏👏
 
Kwani ufamasia siyo Ujasiriamali ?? Ajira imewekwa reserve kwa ajili yako ili ukimaliza "ujishikize" ??
Mkuu nisichokubaliana nacho Mimi ni swala la kurudi Tena chuo kusoma diploma nyingine!
Sijakataa kama hata Pharmacy ni ujasiriamali.
Sitegemei urahisi au mteremko wowote katika kupata ajira.
 
Km utafanya km ulivyopanga kufanya ukimaliza io diploma kwa vyovyote vile mzee atakususa kwa io jiandae kusaikolojia mapema

I mean kuanzia kodi ya nyumba, mavazi na chakula ujitegemee maana mzee atakataa kukupa huduma yoyote kati ya hizo hpo juu

Kwa hiyo mdogo wangu jiongeze ukiwa hapo hapo chuo kwa kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ambazo zitakusaidia mzee akishakususa

Cha muhimu kuliko vyote we fanya unachoona muhimu kwako, kwa sasa mzee hawezi kukuelewa ila atakuja kukuelewa km utafanikiwa kwenye huo ujasiriamali wako.
 
Asante Kwa mchango wako mkuu.
Lakini kitukimoja ambacho hatujagusia hapa ambapo ni kwamba kama lengo la kurudi chuo ni Ili niwe na PHARMACY, it means inabidi niendelee Hadi degree which means I have to spend seven more years darasani, (three years diploma, four years degree!)
Na binafsi siko tayari kuendelea kukaa miaka yote hiyo darasani Tena!
Isitoshe si kitu ninachopenda
Msikilize mshua ana malengo mazuri kwako....!!

Huo ujasiriamali unaoutaka kuufanya utaufanya ndani ya afya!!(pharmacy)
 
Kweli kabisa mkuu maisha hayana formula
Ninachokiona hajapata taarifa sahihi kuhusu haya mambo.
Na Mimi mwisho wa siku nitafanya tu kile nilichoamua bila kujali chochote, ninachotafuta ni kujua kama ipo mbinu naweza kutumia ku make peace with him Ili hata nikija kufanya maamuzi iwe ni Kwa amani.
Ikishindikana sitakuwa na jinsi atanisamehe tu!
 
Mawazo yako umeyapata kwa wahamasishaji? Ukidhani biashara rahisi eeeh. Msikilize dingi maliza ukibahatisha ajira ajiriwa kusanya mtaji then fanya biashara ukiwa ajirani then ukiona unajiweza quit the job. Otherwise usidhani mtaani parahisi
Sitegemei urahisi wowote katika maisha ya mtaani nipo tayari kupambana na changamoto yoyote Ile itakayokuja mbele yangu Ili kutimiza malengo yangu.
Na pia sidhani kama Kuna ubaya katika kuhamasishwa Ili mradi isiwe nje na uhalisia wa maisha.
 
Asante sana Kwa ushauri mkuu
 
Moja ya vitu wazaz wanafeli ni kuforce usomee nn sijui wakat hawajui nn ni passion ya mtoto bro chochote utakachofanya ili ufanikiwe lazma uipende kutoka moyon
Kabisa mkuu Asante sana
 
Sitegemei urahisi wowote katika maisha ya mtaani nipo tayari kupambana na changamoto yoyote Ile itakayokuja mbele yangu Ili kutimiza malengo yangu.
Na pia sidhani kama Kuna ubaya katika kuhamasishwa Ili mradi isiwe nje na uhalisia wa maisha.
Kila la heri, ila usirudi namalalamiko nextime
 
Asante mkuu nimepata kitu kutoka kwako.
 
Hongera sana.
Mwanzo Hii kozi tuli apply lakini tulikosa nafasi nikapata Hii ya nursing.
Natumaini unavuna matunda ya kusimamia kile ulichoamini Kwa Sasa au Bado unapambania hongera sana!
 
Asante sana mkuu Kwa kuwa straightforward!
Ni ukweli usemayo Tena ukweli mchungu Sina budi kukubaliana nao.
Asante sana Kwa ushauri wako
nitaufanyia kazi.
 
Asante sana mkuu.
Samahani naomba kuuliza, ulikuwa unamaanisha duka la dawa muhimu au?
Pia hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…