Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Baba yako ana reality yake katika maisha na wewe una reality yako pia. Kama baba yako ni mtu ambae hazikilizi kabisa maoni ya mtu basi mtaendelea kupambana nae mpaka uende njia anayotaka

Je una biashara tayari ambayo ina kipato kizuri? Kama ndio basi wazazi wengi huwdza kusapoti mawazo ya watoto kwa sababu hii kwa kuwa tayari wanaona kitu kinaendelea.

Kama hauna biashara yenye kipato basi ni muhimu kuwa mpole huku ukianza mchakato wa kujenga biashara yako. Baba yako anachoogopa ni kugharamikia kitu ambacho hakina future ila ukimuonesha tayari una uwezo wa kujenga kitu inakuwa rahisi zaidi kukusaidia.

Kumbuka path yoyote utayochukua haikuzuii wewe kutokuwa mfanyabiashara. Ni kuchukua hatua tu na utaweza kufika malengo yako kwa chochote utachosomea.

Mie mwenye baba kama wako niliamua kufanya maamuzi magumu ya kuacha shule kisha kutoa taarifa ila tayari nilikuwa na biashara na tayari nilikuwa na kipato kizuri tu. Ilikuwa msala mkubwa ila muda ulivyoenda na mshua kuona naishi vizuri hasira zikaisha bado nasonga mbele kitaa mpaka sasa. Usijaribu hili kama huna biashara, kipato kinachoeleweka na akiba ya kukutosha mwaka mzima kuishi mtaani bila kazi.
 


Mtafute rafiki yake, mtu ambaye unaamini wameshibana, omba kukutana na huyo rafiki yake.

Kaa naye kwa ustaarabu na unyenyekevu mkubwa. Mpe hoja zako na malengo yako. Pia usisahau kuelezea namna unavyojisikia hususani kwamba hutaki kukorofishana na mzee, jinsi unavyomthamini na kuheshimu msaada na mawazo yake katika maisha yako.

Muombe akusaidie kuongea na rafiki yake (baba yako) kwa niaba yako. Mzee atakuita tu baadae au inawezekana asikuite ila atakuacha ufanye kinachokupa amani.

Pia muombe Mzee wako kupitia rafiki yake kwamba asimame na wewe katika jitihada zako za kutafuta maisha, asichukulie kama ukaidi bali ni njia yako ya kufikia malengo yako.


Wazazi ndivyo tulivyo, kuna wakati tunakuwa over protective na kutaka watoto waishi ndoto zetu.

Usisahau kunipa mrejesho.
 
Kama diploma tu ya pharmacy hujaifikia.. degree utaifikia lini maana bila degree huwezi kuruhusiwa "kuendesha pharmacy yako mwenyewe"
Utachukua muda sana.. bora usimsikilize mzee
 
Kama diploma tu ya pharmacy hujaifikia.. degree utaifikia lini maana bila degree huwezi kuruhusiwa "kuendesha pharmacy yako mwenyewe"
Utachukua muda sana.. bora usimsikilize mzee
Uliona wapi
 
Mkuu ubarikiwe mno! 🙏
Asante sana Kwa ushauri wako, so far wewe ndo umekuwa most relevant na nilichokuwa natarajia kutoka Kwa wadau!
Nitaufanyia kazi huu ushauri na panapo majaaliwa nitaleta mrejesho.
Asante sana.
 
Kama diploma tu ya pharmacy hujaifikia.. degree utaifikia lini maana bila degree huwezi kuruhusiwa "kuendesha pharmacy yako mwenyewe"
Utachukua muda sana.. bora usimsikilize mzee
Nadhani hatujaelewana mkuu!
Kinachofanya nisikubaliane na Mawazo yake ndio hicho kwamba kama lengo ni kumiliki pharmacy Maana yake Nina miaka mingine Saba ya kukaa darasani mitatu kutafuta diploma na Minne ya degree!
Na Mimi huo muda ninataka kuutumia kuanza kupambania malengo ambayo nimejiwekea sio Tena kukaa darasani!
 
Kwa hiyo mipango yako ya kutafuta ajira....then upate mtaji ujiajiri...inaweza chukua hata 4 years kwa upepo wa sasa ulivyo hususani ukizingatia soko la ajira lilivyo.

USHAURI WANGU.

Kama lengo lako uje kuwa mfanya biashara naona mzee wako naye analengo hilohilo. Chakufanya kaa chini na mzee wako mpe mikakati kwamba upo tayari kwenda kusoma phamarcy ili tu uje ufungue phamarcy yako na une udeal hiyo biashara. Sababu ya hilo mwambie nikimaliza tu chuo sifikirii kuajiriwa naomba uniandalie mtaji ili nkkihitimu tu nifungue hiyo phamarcy . Akikubali bila maelezo mengi bhasi nenda kasome but ukiona anasitasita endelea na mipango yako na hapa hawezi kukulaumu au kugombana na wewee sababu hajafikia terms zako.

Mwisho wa kunukuu
 
Msikilize baba yako maana yeye ndio kaanza kuliona jua kabla yako.

By the way, hakuna mzazi anayemtakia mabaya mwanae.

Huu ndo ujinga wetu wakiafrica

Ndo mana kila siku tunalalamikia sekta ya afya
 
Nimekuelewa Sana mkuu.
Asante Kwa Mawazo Yako nitayafanyia kazi bila shaka.
Najua mwanzo hatonielewa lakini atakuja kunielewa baadae hakika.
Pia hongera sana Kwa maamuzi uliyochukua na Mimi Niko nyuma Yako mkuu
 
Mkuu ubarikiwe mno! [emoji120]
Asante sana Kwa ushauri wako, so far wewe ndo umekuwa most relevant na nilichokuwa natarajia kutoka Kwa wadau!
Nitaufanyia kazi huu ushauri na panapo majaaliwa nitaleta mrejesho.
Asante sana.

Karibu
 
Wazo zuri sana Hili mkuu Asante Kwa ushauri.
 
Nawapenda sana wazazi Wangu sitaki kuwakwaza lakini pia sitaki kunyimwa opportunity ya kupambania malengo niliyojiwekea katika maisha na natamani pia wazazi wanipe Uhuru wa kujiamulia ninachotaka katika maisha yangu pia!
Simple kama baba Yako analipa Ada na ku-provide vitu vyote wakati wa masomo yako, wewe Nenda Chuo halafu ukifika huko Tafuta Hizo ajira zako unazotaka, Ukifeli ni kumwambia Mzee kwamba nimefeli/disco etc itakuwa sababu Kuu, kuliko Ajira;
Hivyo usioneshe hali yoyote ya kuonesha kwamba una utaratibu wa mambo yako.
 
Naweza kufanya hivyo lakini sitaki apoteze pesa zaidi.
I do care about him too, kumwacha anilipie ada huku nikijua kabisa nitafeli sitapenda hilo.
Zaidi ya yote sitaki kabisa kwenda chuo kusomea hiyo kozi Kwa Sasa si kitu ninachopenda.
Lakini Asante Kwa wazo lako mkuu.
 
I do care about him too, kumwacha anilipie ada huku nikijua kabisa nitafeli sitapenda hilo.
Nimesema ukifeli sio ukijifelisha!! yaan nimechukulia kwamba utakuwa umejishikiza mahali, lakini pia una ujasiriamali wako unafanya hivyo balance ya mambo yote matatu impact inaweza kuwa kubwa kwenye Masomo kuliko hayo mambo mengine mawili.
hivyo kufeli ni incase isiwe nia yako.

Kwa maelezo yako ni kwamba mzee anapendz uje kujiajiri baada ya Kusoma phamarcy wewe unataka Kujiajiri kabla; Hivyo wewe na mzee wako mna common Interest isipokuwa kwa muda tofauti hivyo kumwin kwa kitu nilichokwambia ni rahisi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…