Nawezaje kushikilia msimamo wangu bila kuwakwaza wazazi?!

Sawa mkuu Asante sana.
 
Tabia za mzee wako siyo tabia za mababa Kama angekua baba ingekua ameshakutimuaga hapo nyumbani siku nyingi sahivi unakula mlo mmoja kwa siku na maji mingi had msosi unaogelea tumboni ila dingi yako anatabia za Daddy hata ufikishe miaka 60 bado atakuona mtoto tu na atakupa kila kitu

Yani kwa kifupi si unamjua Le mutuz? Eeeh dingi yako anakuandaa kuwa Le mutuz katoboa miaka 60 ila bado mtoto yuko kwa baba
 
Ukimaliza iyoo kozi tafuta kazi alafu simamia ndoto zako Mimi Mzee alitaka nisome famasia Ila Mungu alinipa kazi mapema nikaachana na wazo lake alipiga kelele Ila ndyo nilishaamua cha Kwanza toka Kwanza mikononi mwake ujipangie ndoto zako bila kutegemea pesa yake
 
Vizuri sana mkuu Asante sana Kwa ushauri na Hamasa
 
Kwan kuwa na duka la dawa sio ujasiriamali? Mbona mzee kakushaur kitu kizur au kwako wewe biashara lazima iwe duka la nguo [emoji23][emoji23]
 
Kijana huhitaji kusomea Pharmacy ili uweze kufanya biashara ya Pharmacy, Ili uweze kufanya biashara ya Pharmacy unachohitaji ni hela tu, hapo Baba anataka kukupeleka mchomo, Komaa na msimamo wako mkuu Dunia ya sasa bila ya kukipigania unachokitaka au kukiamini utaishia pabaya sana. Mimi ni mhanga mkubwa wa hayo.
 
Issue ni kurudi Tena chuo miaka mingine mitatu kitu ambacho siko tayari kufanya.
Kwan kuwa na duka la dawa sio ujasiriamali? Mbona mzee kakushaur kitu kizur au kwako wewe biashara lazima iwe duka la nguo [emoji23][emoji23]
 
Pole sana mkuu.
Lakini Bado una nafasi ya kufanya kile unahitaji
 
Naoam
Naona mzazi anatka kutimiza ndoto zake kupitia kwako. Kuwa na msimamo itakuwa ujinga mkubwa utoke usome nursing hlf usome famacy. Mwambie Kama kumilik duka Unaweza bila kusomea... Mweleze usifikirie kutomuudhi. Mwache akasirike, we utumize ndoto zako. Atakuelewa baadaye.

Kama ni ufamasia somea ADDO, somea umiliki....biashara umeisha ndan ya mwezi.
 
Asante sana mkuu kwa mchango wako, uzuri tulishayamaliza na tukakubaliana hivi hivi kama ulivyoshauri.
Sema ndio hivyo sasahivi kozi yenyewe imesitishwa na hatuoni dalili zote kuwa itaanza upya lini




 
nikikumbuka vile mzee wangu alinambia nikasomee clinical officer baada ya kuhitimu kidato cha nne miaka ya 2000"s nikaleta ujuaji wangu leo niko job (sio serikalini) ila naishi kwa mashaka kama digidigi

maisha ni yako,ila biashara si lelemama mkuu alafu unaweza fanya biashara ukiwa na famasi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…