Nawezaje kutoa hela kwenye laini ya mzazi aliyefariki

Nawezaje kutoa hela kwenye laini ya mzazi aliyefariki

Joined
Jan 26, 2019
Posts
87
Reaction score
113
Wakuu habari za wakati huu,

Samahani sana Nina jambo lakuwashilikisha hapa jamani. Mimi ni kijana nimefiwa na wazazi wangu wote kwa kufatana yaan alitangulia Baba ikapita wiki moja na Mama pia akafariki 😪😪😪. Dah!

Sasa suala langu so Hilo ila nilipenda ni rejee kidogo . SWALI:Je Nawezaje Kutoa Hela kwenye Akaunti ya Laini ya Marehemu Baba mzazi.
 
Taratibu za mirathi zikikamilika nenda na nyaraka zako kwenye ofisi za hio mitandao wata reset hizo accounts saiv chochote unachofanya kinaonekana ni uhalifu machoni pa sheria
 
Wakeup habar za wakati huu ,samahani sana Nina jambo lakuwashilikisha hapa jamani .Mimi ni kijana nimefiwa na wazazi wangu wote kwakufatana yaan alitangulia Baba ikapita wiki moja Na Mama pia akafariki 😪😪😪. Dah! Sasa swala langu so Hilo ila nilipenda ni rejee kidogo . SWALI:Je Nawezaje Kutoa Hela kwenye Akaunti ya Laini ya Marehemu Baba mzazi.
Pole sana mkuu kwa kufiwa na wazazi.
 
Msimamizi wa mirathi aliyeidhinishwa na mahakama ndiye mwenye mamlaka ya kukusanya na kuzigawa mali za marehemu.Hata kama ni mzazi wako kama hujaidhinishwa na mahakam huwezi kuzitoa, na kufanya hivyo ni uhalifu kama uhalifu mwingine.
 
Kama ni account ya bank nenda bank utapewa taratibu zote

Kama ni mtandao wa simu na upo dar es salaam nenda makao makuuu kama Voda nk
Ila cheti cha kifo lazima kiwepo wathibitishe kuwa amefariki
Pesa hizo zitatolewa tuu baada ya msimamizi wa mirathi kusimamia ugawaji wa hizo pesa na kuwe na muhtasari wa wanafamilia kuwa fulani atapata kiasi fulani cha fedha. Mahakama ndio itaandika cheki ya kuwalipa waliogawiwa.

Huo muhtasari utapitishwa na msimamizi wa mirathi na kupelekwa mahakamani

Kabla ya hapo msimamizi wa mirathi ataenda kujitambulisha kwa mtandao husika na hao wataandila cheki ya hela za maheremu kwenda mahakamani.

Nafikiri huu ndio utaratibu.
 
Hakikisha unapata cheti cha kifo kinapatikana RITA, hakikisha unapata barua rasmi ya kupewa mirathi ya familia hii kikao kikae na ndugu zako watie saini na muhuri wa mwanasheria baada ya hapo piga copy nenda kwenye mitandao.
 
kijana nimefiwa na wazazi wangu wote kwa kufatana yaan alitangulia Baba ikapita wiki moja na Mama pia akafariki 😪😪😪. Dah!

Sasa suala langu so Hilo ila nilipenda ni rejee kidogo . SWALI:Je Nawezaje Kutoa Hela kwenye Akaunti ya Laini ya Marehemu Baba mzazi.
Pole sana kwa msiba wa wazazi,zipo taratibu za kufuata kisheria utakapofungua/mtakapofungua mirathi kwa sasa muhimu kufanya ni kwenda office za mtandao aliokuwa anatumia baba au mama wape taarifa za kifo chake ili line wasiifunge.

Au jitahidi kila miezi mitatu unatia salio ili line iendelee kuwa active then wakati mirathi ikiendelea mahakama itaandikia barua mtandao husika ikikuthibitisha kama msimamizi wa mirathi but hii ita-depend kama wewe ndiye uliyeteuliwa otherwise mahakama itamtambulisha kwao msimamizi mliyemchagua nyie familia.

Kwa mara nyingine pole sana Mungu akufanyie wepesi unapoenda kutafuta haki zako.
 
Back
Top Bottom