Hii hali hunitokea once kila baada ya mwaka au miaka kadhaa na hamna kitu naweza kifanya kikaondoa stress zangu maana si tv,si kazini,si marafiki,si chochote kile na mara nyingi hujigundua nipo ktk hiyo state usiku wakati wa kulala.
nikifika kitandani usingizi hauji,nitajigeuza huku na kule ila wapi,kulala staki,kukaa staki,kusimama staki,naanza kutembea naenda sebleni,chumbani,narudi jikoni naenda chooni nazunguka nyumba nzima,hali naonaga inazidi tu kuwa mbaya.
ninachofanya huwa nafungua kabati natafuta nguo navaaa (kumbuka huo ni usiku inaweza kuwa saa 8 hata) nachukua viatu navaa,natoka nnje sichukui usafiri wowote wala sibebi simu.
naanza kutembea kufata barabara ya LAMI au barabara yyte ile iliyonyooka natembea natembea natembea (sijui niendapo) natembea naenda safari yangu itaishia pale miguu itakaposema imetosha yani imechoka,basi hapo hapo nikishachoka kuendelea naanza kurudi nyumbani kwa kutembea.
natembea narudi nyumbani taratibu mpaka nafika home nimechoka sana,nikiingia tu sebleni najilaza hapo hapo chini najinyoosha nalala usingizi unanichukua,nikija kuamka nikioga basi najikuta ile hali imepotea au kupungua.
kwa hyo njia pekee niliyo ithibitsha inayoweza ondoa hii hali ni kuuchosha mwili,najua huwezi fanya mazoezi kwa hali uliyonayo ila amka tembea tu,we tembea nenda huko fata barabara kama mtu aliepotea njia,mpk miguu ichoke nakuhakikishia ukrudi nyumbani kichwa itakua mpya na utaweza kuendelea na maisha tena.