Nawezaje kuwa na furaha na amani ya roho?

Nawezaje kuwa na furaha na amani ya roho?

Kitabu nimekisoma hichi.... Niwe mkweli kilinisogeza karibu na Mungu Wangu...Japo nichadini tofauti na Yangu...wamesisitiza Sana kusali..japo sikukimaliza
Vizuri sana...

Jaribu na hichi...how to use your hidden power of your subconscious mind,kizuri Sana kipo simple na kina pages 90 tu hakichoshi.

Ushauri wangu:-

1. Tafuta eneo lililotulia,muda ambao hakuna movement za vitu/watu...usiku au alfajir itakuwa vzur zaid.

2. Weka nia moyoni unataka kufanya jambo fulani.

3. Tia udhu, (tawadha kwa ajili ya kuswali).
4. Swali rakaa mbili za sunnah.

5. Leta nyiradi zako then omba chochote ulichokinuia kwa mola wako.
6. Kuwa na matumaini ktk kile ulicho kiomba.... feel as if u have already received that things.

7. Ukishamaliza fanya meditation as much as u can....
.......................

Jijengee tabia kila ukiamka asubuhi useme maneno mfano wa haya.

1. Alhamdulillah kwa kuamka salama mwenye afya,ninafuraha,nina mafanikio makubwa,ninaujasiri wa kufanya mambo yangu,nimetimiza ndoto zangu, n.k

Our greatest power is the power to choose... either happiness or sadness.
 
Tafuta movie/ drama za kikorea ambazo hazijatafisiliwa,hutojuta ushauri huu.

Mm nikitoka kazini fasta home, napita sokoni , napitia maziwa. Nikifika ni movie na kula, kunywa, kuchungulia jf.hayo ndo maisha yangu.

Hii ndo njia pekee ya kupunguza stress.kuna kipindi nilikuwa kama wewe sasa hivi nimezoea.

Wengine watakushauri utoke out. Ila najua sio rahisi utoke out kufanya nini?

Wengine watakwambia utoke na marafiki. Marafiki wapi? Wakati mmetoka kazini mkaenda home utoke kwa lipi? Mkifika huko mfanye nini wakati umeshiba?

Poole dia hiyo hali naijua huwa haielezeki.
Huenda "upweke wa kuwa peke yako"! Mungu akasema, si vyema huyu mtu kuwa peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae.

Nyie endeleeni tu kuwa peke yenu, cha moto mtakiona.
 
Sahau yote anza upya, Usiwabebe watu katika moyo, achia kila kitu, Chukua ufagio fagia duku duku lolote ndani ya nafsi yako, Jisamehee wewe mwenyewe kwa mahali uliposhindwa samehe na wote waliokukosea kwa moyo mkunjufu, hakika utaona mabadiliko katika moyo.
 
Wakukukaza unae??
Au ndio unashindia dildoo??[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapana! hata ivyo valium haina athari kama utatumia vyema na ushauri wa doctor utazingatiwa ipasavyo..
Basi ntaenda kwa doctor kuomba ushauri...Naona madoctor wakipa Stress kidogo wanajituliza na madawa...Sasa aijyi wafamasia
 
Pole sana. Hizo pia ni dalili za depression. Nishawai onja hicho kikombe.
 
Nishakuelewa ugonjwa wako.
Hata mimi nilikuwa na ugonjwa kama huo.
Huwa ugonjwa unasababishwa na loneliness/antisocial behaviour.
Inawezekana mazingira uliyolelewa ulikuwa hupati nafasi ya kujichanganya na watu ambayo hiyo hali imeendeleza upweke ambao ndio unakusumbua hadi leo.
Dawa ya huo ugonjwa ni kujichanganya na watu mbalimbali kwa mfano hata kama hunywi pombe sio mbaya mara moja moja kujichanganya na marafiki kwenda sehemu za kurelax inaweza kuwa beach au pub au kwenye mahotel.
Mimi hiyo hali huwa inaondoka nikitoka nyumbani na kujichanganya na watu pamoja na kusafiri sehemu mbalimbali.
Chukua hatua
This is Real
 
Pole bint,

Huwenda mm nikawa tofauti na wale wote, waliokushauli,

Kinachokusumbua ww umechoka kukaa home ukizingatia elim unayo na kazi hakuna , kuna muda unahisi huwenda ulipoteza muda kusoma na huwenda baadhi ya marafiki zak uliosoma nao hukoo na wao wakaishia njiani kwa sasa hivi wana kazi nzuli na wengine wameowa au kuolewa. Pole sana

Wakati bado unao tena mkubwa sana Fanya hivi

Mm binafsi huwa nasema ni bora kufanya kazi usiolipwa kuliko kukaa bila kazi kwnn nasema hivyo?

Ukifanya kazi kama haulipwi,kuna mambo unayatengeneza , unaongeza ujuzi ,watu wanakuona lkn pia kuna vishawishi vingi unapisha navyo ukiwa kazini,

Kama una rafiki ndugu jamaa au jirani ana kaofic kake nenda ukafanye kazi ukutane na mazingila tofauti yatakayokufanya utoke ktk hiyo hali, lkn pia hicho utakachofanya kitakuongezea ujuzi haijalishi ulisomea au ndio unajifunza
Kiufupi moyo wako ni mpweke lkn pia upo upo tu hicho ndio kinakufanya uwe ktk hali hiyoo,


KARIBU NYUMBANI RAFIKI MWEMA

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Umeongea kitu cha maana sana.. na kina ukweli asilimia [emoji817]
 
Nimesoma comment zote na hadi sasa bint CreditAnalyst ameshapatiwa ushauri mpana sana wa kuamua yey mwenyewe achague kipi..

Tatizo nnaloliona ni kwa bint hataki KUTUAMBIA ktk yaliyosemwa mengi kama Ushauri lipi hasa ni Tatizo lake ili asaidiwe

Wengine hapa ni Wanasaikolojia angeweka wazi angle ya tatizo lake basi tungempatia solition directly

Hauwezi msaidia mtu kama hujui chanzo cha tatizo, utabaki hisi ni hiki au kile
 
Hali hii imeakuanza lini? Ni mara yako ya kwanza au huwa inakutokea mara kwa mara? Je, kuna tukio lo lote baya (mf. kufiwa na mzazi au mpendwa wako) ambalo limetokea au lilitokea kipindi hiki? Afya yako ikoje? Umeongezeka (sana) uzito au kukonda ghafla? Kazini kuna misukosuko? Maisha yako kimapenzi yamekaaje? Kuna mabadiliko yo yote hasi kiuchumi? Ulikuwa mfuasi wa CHADEMA katika uchaguzi uliopita? Kiroho umesimama imara?

Majibu ya maswali hayo juu (na mengineyo) yaweza kutoa fununu lakini pia yawezekana ni msongo wa mawazo (depression) umekuanza. Kama ni hivyo utahitaji msaada wa kitaalamu kutoka kwa daktari wako au watoa nasaha. Au yawezekana ni mvurugano tu wa homoni na makemikali mwilini na hali hiyo yaweza kujirekebisha yenyewe tu.

Kwa sasa jaribu kuwa karibu na watu wakupendao. Kama kuna mmoja unayemwamini mwambie unavyojisikia. Unahitaji faraja na watu wanaojali. Kama ni muumini yawezekana pia ikawa ni vita vya kiroho. Mbali na wewe mwenyewe kupambana katika maombi, jaribu kumshirikisha kiongozi wako wa kiroho. Kama upo katika kikundi cha maombi au jumuia waombe wawashe moto wa maombi kwa ajili yako. Epuka kuwaza mawazo hasi na jitahidi sana kufanya mambo uyapendayo na hasa hasa kusaidia wenye shida. Badala tu ya kujifungia ndani, kama unaweza, nenda hata hospitalini huko ukasalimie wagonjwa siku za wikiendi au wakati wo wote unapokuwa na muda. Saidia watoto katika vituo vya mayatima huko na matendo mengine madogo madogo ya wema. Naamini baada ya muda msukosuko huu utapita, moyo wako utatanzuka na furaha yako itarejea.

Na kumbuka tu kwamba "you are fearfully and wonderfully made. Mungu Akubariki. [emoji1545][emoji1545][emoji1545]


View attachment 1624935
Ushauri bora
 
I don't know if what works for me will have same effect to you too.

For me to feel down/depressed means I have lost self appreciation /strength like I'm weak I can't handle my business. So the solution is to bring it back by working on my self.

Challenging my self to see new growth in three areas of my life is what I do. I work on my physical ,mental and spiritual growth .

Physical growth * I make sure I look my best by working out/exercising. Knowing I'm in control of my weight /body give me a lot of chill.

Mental growth * I spend a lot of free time seeking new knowledge that will provide solutions to my daily life.
It maybe a small knowledge like Doing DIY project for my home.Or new helpful knowledge to improve my performance at my job.

Spiritual growth * The last but important part. I make sure I have the best connection with my God.The feeling of having God close to me and my family brings so much joy to my heart.

For me happiness is bettering my self everyday. As for now i do all the above working out FIVE days per week, learning new things and improving the previous one (even this language I'm using is within my learning/improving program.

For sure every morning I work up feeling so energetic and exited about life because I have a lot to accomplish.
There is no correlation between the very first paragraphs and the last one.

I suspect something, you saying "(even this language I'm using is within my learning/improving program." And then followed by the use of wrong words in your last paragraph while you picked and used very right words in your previous paragraphs brings about suspicion.

Not to say much, but your English is much much much better than most of us.
 
hata mm nina hali kama hiyo natafta mchumba jaman nile tunda najua nitapona tu,
 
There is no correlation between the very first paragraphs and the last one.

I suspect something, you saying "(even this language I'm using is within my learning/improving program." And then followed by the use of wrong words in your last paragraph while you picked and used very right words in your previous paragraphs brings about suspicion.

Not to say much, but your English is much much much better than most of us.
Ooh thanks for correcting me. I didn't get time to proofread the thread i wrote.
I got tired writing that's why the last paragraph looks awful.
 
Hii hali mimi pia huwa inanitokea mara kwa mara. Najikuta nakosa furaha na naona bora kufa tu kuipumzisha nafsi yangu. Nakua sioni hata sababu maalumu ya kuishi hapa Duniani. Nimeajiriwa na ninafamilia ya watoto wawili.

Nilijaribu kumshirikisha wife hili jambo wiki kama mbili zilizopita lakini alihisi kama namtania maana jibu lake lilikua "achana na mawazo hayo, unataka kukimbia majukumu!?"

Sikutaka kuendelea kumsimulia kuhusu hiyo hali ila kwa sababu ulikua ni muda wa kulala tupo kitandani tayari, nilimalizia kwa kumsihi aliweke hilo jambo akilini na anikumbuke kwenye maombi yake ya mara kwa mara.

Ee Mungu tusaidie. Utusaidie kujua nini makusudio yako ya kutuleta hapa duniani..😭
 
Back
Top Bottom