miamiatz
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 505
- 941
Na ili umake it kwanza nikushauri usisome ma pdf achana nayo kabisa. Pdf lina page 400 eti linafundisha libraries mbili tu za python pandas na matlib ya kazi gani wakati python ni lugha ya vilaza unaiandikiaje page 400 [emoji3][emoji3][emoji3]. Na ninakwambia hivi sababu I'm a programmer ambae ni self taught.[emoji4][emoji120]
Nikwambie kitu programming is all about problems solving. The easier the solution the better.
Nitakupa mfano kuna jamaa tulikuwa tunajadili jinsi ya ku scrap data from various web sources kuzi clean na kuziweka kwenye database yetu. Then ku analyse hizo data na kuzitumia kutatua matatizo yanayokabili biashara za sekta flani as consultancy.
Tukabishania methods, moja ilikuwa ngumu moja simple. Yeye anataka ile ngumu sababu ni mtabe wa programming. Mimi nilikuwa nataka ile nyepesi sababu sio mtabe sana.
Tukachukua yake komaa komaa na wewe mwezi mzima nikamwambia haya time is over twende na yangu. Tukapiga wiki mkeka umekamilika. Unalala ukiamka unakutana na dashboards mpya zenye full analysis.
Jamaa mpaka leo hii hakubali tena kutumia njia ngumu kusolve issue kama kuna nyepesi.