Nayaona Maisha ya Gamondi Yanga kuwa mafupi sana

Kote umeongelea pressing....kasoro mechi hizo mbili walizocheza na MAMELODI hujasema wamecheza mfumo upi mkuu....unahisi hawakucheza pressing pia??
Mpira unaulazimisha ila sio fani yako tafuta mchezo mwingine ushabkie. Mechi ya Yanga dhidi ya Mamelodi Yanga hakucheza mpira wao wa kukabia kwa juu, bali waliwaacha Mamelodi wacheze ila Yanga ikaziba njia huku wakitegemea mipira ya counter attacks. Jambo lililofanya Mamelodi wapige pasi nyingi golini kwao na katikati ila wakifika golini kwa Yanga mipira wana nyang'anywa au Mamelodi kupoteza mipira kwa kupiga pasi ovyo.
 
Kwahiyo uliposema kuhusu kocha wa Ken Gold kufungua njia kwa makocha wengine, hii mechi ya Ken Gold na Yanga ambayo ulioizungumzia kwenye uzi wako ilikuwani ya mwaka
Kafungua njia kwa kuwasoma Yanga kimfumo na namna ya kucheza nao shida Iko wapi.....kwanza nilichompendea katoka adharani kwenye press na kusema ili kuwakabili Yanga nicheze ABC na ndicho alichokifanya.....Sasa hata Kama ww ni Kocha mfano wa namungo/pamba au timu yoyote ambaye mechi ijayo inakutana na Yanga, ni lazima utatumia mechi hii Kama reference

Kwa aidha;
1...kurekebisha makosa ambayo ken Gold wamefanya kwa kutumia muundo huo huo

2....kuboresho muundo huo huo ili kupunguza makosa ya ken gold
 
Sawa nashukuru

Kukukumbusha nipo based na mambo tofauti kabisa na mpira.....Mimi ni mdau TU hata hivyo sio ushindani Kama tunatofautiana mitazamo na mawazo sio mbaya mpira haupo hivyo
 
Mwenzio huyu hapa alikuja na uzi baada ya kuona Yanga imeshinda kwa mbinde msimu uliopita lakini pamoja na kuweka hizo mbinu adharani lakini huyo huyo Gamondi kawa bingwa wa NBC na FA na CAF kacheza robo fainali. Sio kwamba msimu uliopita hakuna timu zilizocheza kama Ken Gold zipo nyingi na zilicheza hivyo na zikafungwa. Ndio maana nikakuuliza wewe mpira umeanza kufatilia leo? Maana unaleta utumbo

 
Kaka, unakuta baadae nae anajiita mchambuzi.
mchambuzi wa mchongo
 

Ila Sasa ni dhahiri makocha wengi wamemsoma na kuanzia kujua namna ya kucheza na mfumo huu ( watu hawalali wakuu )
 
Usisahau, mliropoka mineno ya kiubaya ubwela kama haya enzi za IHEFU..!! Na mliifanya Ihefu kuwa kichaka cha kujifichia. Wakaja kula KHAMSA BIN SUFURI pale Chamazi. Endeleeni tu na vichaka vyenu vipya kila kukicha, na sisi tutavifyeka kila mkivianzisha..!!
 
Wamesahau habari ya Ihefu
 
Imefikia hatua Yanga asipofunga goli kuanzia nne, inakua wachezaji wamechoka mara makocha wameusoma mfumo wa Gamond sababu kibao. Kwa hiyo braza mechi ijayo Yanga wakishinda 5 utatuambia nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…