Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Asipoamia haitakuja kamwe.Katiba mpya!
Hivi, upatikanaji wa katiba mpya nayo ni hisani ya Rais Samia [mimi simuiti Dokta kwa sababu hastahili kuitwa hivyo]?
Nimeona mara nyingi vya kutosha sasa watu wakisema:-
1. Samia atuletee katiba mpya.
2. Samia atupatie katiba mpya.
Sielewi kabisa. Kwani yeye huyo Samia ndo ana uamuzi wa mwisho kuhusu hiyo katiba mpya?
Ni hisani yake yeye huyo Samia, ambaye ni mtu mmoja tu, kutuletea Watanzania zaidi ya milioni 60, hiyo katiba mpya?
Kwa hiyo Samia akikataa kuleta hiyo katiba mpya, ndo basi tena?
Sisi Watanzania kuna kitu hakiko sawa kwenye psyche yetu.
Ccm ni watu wa hovyo sana