Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.
Naona umri unakutupa mkono hadi kimuonekano hivyo tunategemea hvi karibuni utahitaji msaada katika utekelezaji wa majukumu yako.

Carer niko hapa mheshimiwa
20usd kwa lisaa 1.😅
 
Chukua hiyo
Uwe unachukua viaz vitamu unavipika na maganda yake alafu unakula na maziwa freshi ,kwenye kula unaruhusiwa kumenya yale maganda ukipenda muhimu upike na maganda yake tu kikiwa sehem ya chakula chako hutojuta
 
Unakunywa pombe? Unapiga shoo nyingi sana? Ulaji wa vyakula ni wa aina gani ya vyakula unakula? Muda wa kula mlo mmoja na mwingine ni muda gani? Unaufanyia mazoezi gani mwili wako? Kuna dawa zozote unazotumia kujitibu upatapo maradhi? Angalia sana hayo utagundua sababu kwa nini unazeeka haraka
 
Mkiambiwa muache mapunyeto huko ujanani mnakaza mafuvu. Madhara yake ndiyo haya sasa. Hakuna kitu kinachozeesha haraka kama mapunyeto...ukishavuka 35 tu hoi mgongo unakuuma, kumbukumbu hakuna, mwili legelege, uchovu 24/7, ngozi kukunguwaa, kukosa motivation, kulala lala hovyo; na matatizo mengine kibao.

Acha pono na punyeto...kula sana matunda na mboga, fanya mazoezi, maji kwa wingi....utakuwa OK.
 
Kwamba ni mcc[emoji3],

Mbona mzee wa msogo bado kama kijana wa jana[emoji3]
Mzee wa Msoga akisimama na baba Fredrick best ake inakuwa kama amesimama mtu na babu yake, maana mmoja nywele nyeupe kichwa kuzima na mwingine ni nyeusi kichwa kizima japo kiumri wapo sawa.

Mzee wa Msoga ni mtu wa kutumia hair superblack.
 
Dawa nzuri ya kupunguza speed ya kuzeeka,Anza Kula na kunywa supu ya kongoro angalau 500mls Kwa siku Fanya zoezi Hilo mwezi mzima njoo na mrejesho ikikufaa endelea nayo.
Yes , kongoro inaongeza kitu kinaitwa collagen sijui kwa kiswahili ni nini, hii inapunguza kasi ya kuzeeka. Tumia sana matunda na mbogamboga upate vitamin A na C za kutosha utaona unakuwa kijana
 
Back
Top Bottom