Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.

Fanya mazoezi mkuu
 
Kuka matunda na mboga mboga, epuka nyama wanyama kama mbuzi, kula sana samaki,maziwa soda yako iwe youghort,kunywa chai yenye limao, fanya mazoezi kidogo tafuta dam ya universal donor yani group O negative uwekewe punguza ngono
 
Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.
Ninaishi na wakulima wala hawazeeki kama watu wa maofisi na wamama wa nyumbani ila wanapauka tu. Watumishi wananawiri tu ila kuzeeka kuko pale pale.
Vitambi obesity, kisykari, presha vyote vinawazeesha white colar job.
 
Mkiambiwa muache mapunyeto huko ujanani mnakaza mafuvu. Madhara yake ndiyo haya sasa. Hakuna kitu kinachozeesha haraka kama mapunyeto...ukishavuka 35 tu hoi mgongo unakuuma, kumbukumbu hakuna, mwili legelege, uchovu 24/7, ngozi kukunguwaa, kukosa motivation, kulala lala hovyo; na matatizo mengine kibao.

Acha pono na punyeto...kula sana matunda na mboga, fanya mazoezi, maji kwa wingi....utakuwa OK.
Pono na punyeto vina zeeshaje mwili?

Je vipi mtu aliye na mke na wanasex kila mara?

Au mtu anaye fanya ngono kila mara?

Huyu ana utofauti upi na mpiga nyeto?

Maana wote wana toa protini ileile mwilini.
 
Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.

Fanya mazoezi, acha kula wali
 
Punguza vya kula vya wanga
Punguza nyama nyekundu
Punguza vitu vya sukari
Punguza kulala mchana
Acha pombe
Acha soda
Acha joice
Acha wali
Acha ngono
Acha kuchek movie au series kwa muda mrefu
Acha kucheza game muda mrefu
Pendelea fanya mazoezi kidogo
Pendelea mboga za majani
Pendelea bidhaa za bahari
Pendelea matunda
Pendelea vya nyuzi ( tende ,viazi vitamu nk
Pendelea kipaka mafuta ya nazi
Pendelea kula kabla ya saa mbili usiku
 
Back
Top Bottom