Naziona dalili zote kwamba Mbowe na wenzake wanatoka Gerezani

Wanalindana kuuibia wananchi,mmoja analindwa aibe kura mwingine analindwa ale rushwa
 
Bongo Raha.

Tuna amka asubuhi,

Tunakunywa chai,

Tunanunua bando,

Tumajadili mambo yale yale ya siku zote.

Tunakula mchana,

Tunaendelea kujadili

Tunakula usiku

Tunalala

Kesho tena tukiamka, ratiba inaendelea

Ogopa WASWAHILI 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Lete agenda mpya ndugu tujadili.
 
Lete agenda mpya ndugu tujadili.
Kutoka hatutakubali.

Mpaka hatutatoka Mwanza mpaka tufanye kongamano la katiba,

Tukaja vijana tuingie barabarani mpaka mwenyekiti aachiwe huru.

Sasa hivi tuko online tu, tunasubiria huruma kutoka kwa watu wale wale waliomkamata waamue kumwachia huru.

Wakikaza ndio imetoka hivyo.
 
Yes, unaweza kuwa karibu sana na ukweli....

CROSS EXAMINATION ya Jana tarehe 11/01/2022 toka kwa mawakili watatu wa utetezi (Nashon Nkungu, Malya & Kibatala) dhidi ya shahidi namba 08 Askari Polisi Jumanne Malangahe imefunua mambo mengi sana, moja kubwa ni udhaifu wa Jeshi la polisi ktk kusimamia sheria, kufanya kazi kwa mazoea na kutojua sheria ktk utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku...

Kikubwa zaidi ni kuwa, sasa inaendelea kuthibitika bila shaka yoyote kuwa kesi hii ni ya kubumba na watashangaa sana utetezi nao wakianza kuleta mashahidi wao kuja kuthibitisha "KOSA LA KUPANGA NJAMA ILI KUTENDA UGAIDI"

Nawahakikishia bila shaka yoyote na wala bila hata kupepesa macho kuwa, kuna baadhi ya mashahidi watakataa kuja kutoa ushahidi au la wataletwa kwa pingu kwa sababu kila kitu kimeshavurugika kwa sasa...

Kwa lugha rahisi ni kuwa, mpango mzima umshaharibika, hauendi kama walivyotarajia...!!

On the other hand, Mimi nawashangaa sana hawa Majaji wanaosikiliza kesi hii ya kijinga na kipumbavu kwa sababu hata kwa macho ya kawaida yasiyo ya kisheria, inaonekana wazi kabisa kuwa imetengenezwa na watu fulani waovu wachache huko serikalini, wenye nia na malengo maovu ili kuwaondoa katika picha (to take out of the picture) baadhi ya watu wanaowaona ni kikwazo kwa nia na malengo yao maovu kutimia...!

Kwa zaidi ya 100% Freeman Aikael Mbowe anaonewa tu. Hii ni mbaya sana na kwa kweli haiko sawa, ni balaa na laana kwa taifa na nchi yetu...!

Wameumizwa wengi sana kwa njia mtindo huu. Wenye majina na wasio na majina. Kumfikia Freeman Mbowe ndipo walipo crumble...

Wamefikia kwenye kilele cha OUVU wao na sasa it's KARMA TIME, IT'S PAYBACK TIME....
 
2025 fever
 
Kuwa mvumilivu ndugu...

Kila jambo lina wakati wake ndugu...

Na ukifika wakati wake, siyo kutenda tu bila kutumia akili, bali maarifa, busara na hekima ikiongozwa na akili njema ni muhimu sana kutumika...

Lililo HAKIKA KABISA ni hili, kuwa, siku zote WAOVU huwa hawadumu na hawashindi. Hata hawa hawatashinda. Wataondoka tu na kila tendo liwe BAYA au JEMA lililotwndwa na watawala hawa, lina hukumu yake sawia na ni hapa hapa ktk ardhi ya dunia hii...
 
Inasikitisha sana. Binadamu kumfanyia hivi binadamu mwenzako kwa sababu tu ya Tumbo.
 
Aiseee 🤣🤣🤣🤣

Anyway, ndio maana Mungu haonekani.

Maana hapa hatujui ni nani muovu kuliko mwenzake.

Possibly, ni waovu wawili kila mmoja na nguvu yake kwa wakati wake.
 
Mama na timi yake kabambe ya ushauri, wanalifanyia kazi hilo, tokea mama aingie madarakani.

Hi kesi ya mbowe, Hakubambikwa kesi Mbowe hata kidogo, aliyebambikwa kesi ni Mama. Mbowe ni chombo kilichotumika kumbambika kesi Mama. Juu ya hujumu zote alizofanyiwa mama, tukianza na walipoona Wameshindwa kusimamisha UAPIZWAJI wa mama kuwa Raisi, wakakimbilia kusomba pesa benki kuu, ili mama akose pesa za kuendeleza serekali na mengi mengine.

Na hii kesi ya Mbowe inawahusisha wengi hata kuna baadhi ya viongozi wa Chadema wanahusika na huu mkakati, tutakuja kuona ukweli ukitoka. Leo tunaiona kesi ikijumuisha matukio ya Lissu, Ben Saanane na wengineo, sijui inahusikaje na hii kesi, tena hilo limeletwa na wakili wa utetezi??????
 
Kazi yetu kubwa ni kuzidi kuomba MUNGU ili kesi hii ya michongo izidi kuwavua nguo wenye mamlaka
 
Kibatala alimchanachana Jumanne kiasi Cha kuonyesha wazi hakuna kesi. Maana vitu vyote vinavyowaunganisha watuhumiwa na kesi ya ugaidi imeonekana hakuna...hakuna rekodi ya maongezi, hakuna vilipuzi, hakuna ushahidi wowote! Wataenda kudhalilika vibaya
Hata mimi nilishangaa; nikahisi kuna mchezo unachezwa ili kumrahisishia jaji kazi ya kuandika hukumu.
 
Watakuja kukupinga,wale wale walioshangilia tulipoteswa sana ndio hao hao wanatushtaki na wanataka kutufunga jela kwa ushahidi na mashahidi wa michongo.Wale watetezi wa kweli wa HAKI,UHURU,UMOJA,DEMOKRASIA na MARIDHIANO ya kuiponya nchi kwa kuandika Katiba mpya!
Walinzi wa amani wanapogeuka watesi wa Raia Wema,lazima hali zetu zitakuwa dhoofu kiuchumi,kijamii na maendeleo yatakuwa ni ndoto.
Ndiyo maana Mh Mbowe yupo gerezani,lengo na dhumuni lake namba 1 ni Katiba kwa gharama ya Uhuru wake.
 
Adharani (hadharani); duha (dua) kweli wewe mhaya
 
Huwajui chadema wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…