Kiukweli hata kwangu kufungwa kwa GSW jana sikujisikia vibaya sana lakini kwa namna tofauti na wewe...kwako adui wa adui wako ni rafiki yako. Haijalishi nani kamfunga GSW,
Raimundo atafurahi tu...sawa bwana. Hata hivyo mimi nachukulia kufungwa kwa GSW kama changamoto kwa #Dubnation, kufungwa kunakomaza timu na ukizoea kufunga tu kama walivyozoea GSW, level of
concentration inapungua. Pamoja na hayo hongera nyingi ziwaendee OKC, good job!
Kufungwa kwa GSW pia kumewarudisha jamvini wenzetu waliopotea na idadi ya wachangiaji kuongezeka and so it was a blessing in other ways too...karibuni sana! Kwa Warriors ninaowafahamu, wanapojeruhiwa kama jana na OKC, wanakuwa wakali kama simba na hili nadhani wote tumeshuhudia. Ole wake atakayekaidi na kusimama mbele yake, kazi itakuwa ni kupiga tu kwani tumechoka, hatuna kingine bali kupiga tu...waulizeni CAVs na Spurs, makovu bado wanayo!