Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kwema Wakuu,
Semina Kwa Makarani wa Sensa imeanza Jana. Makarani wameshaanza mafunzo, na mdogo wangu ni mmoja wao akiwa anafanyia Mafunzo yake chuo cha Ustawi wa Jamii.
Sasa toka jana wanapigwa kalenda juu ya fedha zao za Mafunzo, Chakula na za Kujikimu. Hawajalipwa za Jana na za Leo pia.
Sasa cha pili wanaambiwa kua hata chakula hawatapewa hela ya chakula ambayo ni 10,000/- Kwa siku, bali wanalishwa chakula kisha wanakatwa hiyo hela.
Yaani kuna mtu hapo NBS amejipa tenda ya kuwapikia kisha yeye ndo achukue hizo 10,000/- kilazima. Chakula chenyewe anachowapikia hata Cha Mama Ntilie Cha Buku kina afadhali.
Hivi ni lazima kila kitu tuingize mambo ya dili? Kama hela zipo si muwape wajigharamie nauli za kuja huko kwenye semina? Hata chakula wapeni hela zao kisha pikeni hapo kwenye semina anaetaka kununua kwenu aje kununua kwa hiari yake Kwa bei ya Soko, sio kulazimishana kwa bei mnazozitaka nyinyi.
Hili ni zoezi muhimu sana, lakini mnaanza kuliharibu mapema tu sababu ya ulafi na uroho wenu wa hela za watu. Watu wanakuja kwenye semina huku wamenung'unika, mnadhan lengo la semina litafikiwa kweli hapo?