Mkuu, nilishiriki zoezi la sensa mwaka 2012 kama karani, mwaka huo nikiwa ndiyo nimemaliza Chuo Kikuu, njaa kali mtaani.
Hapo kuna upigaji. Hata kipindi chetu budget ya chakula ilikuwepo. Pesa ambayo kama utaratibu ungefuatwa tulipaswa tupewe mkononi ili kila mtu ajitegemee maswala ya msosi, kilichotokea ni kwamba walilazimisha kumpa tender mtu wa catering! Sababu yao eti kila mtu akienda kula anapopajua kuna ambao watachelewa kurudi kuendelea na semina kwasababu wataenda kula mbali na muda wa lunch ulikuwa mchache (tulikuwa tunapewa an hour; ambayo kiuhalisia haukuwa muda mchache kwa mtu anayejua kujiratibu vizuri).
Ukweli ni kwamba kuna 10% yao kutoka kwa mtu anayepewa tender ya msosi. Na uzoefu unaonyesha kwamba chakula huwa hakilingani na thamani ya kiasi cha fedha kinachotolewa kwa sahani.
Halafu malipo yoyote huwa hayafanyiki kabla ya zoezi husika, hapo watafanya semina kwa siku kadhaa ndiyo walipwe kiasi, baadaye wataendelea na semina halafu watalipwa mkupuo mwingine wa mwisho.
Fedha inayolipwa kabla ni ile ya on-cite, kwa maana ya kwamba kabla ya kwenda kuhesabu watu ndiyo kila mtu atalipwa posho yake yote pamoja na kukabidhiwa vitendea kazi.
All in all mpe dogo pole (kama siyo wewe mwenyewe [emoji3]), mwambie awe/uwe mvumilivu.
Ikumbukwe kuwa Hayati Mwl Nyerere aliwahi kusema, "utumishi wa umma (likiwemo zoezi la sensa) ni kazi ya kujitolea, siyo kazi ya kulipwa mamilioni".
Asante.
Sent from my TECNO RC6 using
JamiiForums mobile app