NBS acheni dhuluma, walipeni Makarani hela zao

NBS acheni dhuluma, walipeni Makarani hela zao

Hivi unaonaje kwamba, watu wapewe hela ya chakula ili wanunue wao, hali itakuwaje wale wazee wa zero cost, yaani hanunui chakula ili ku-save hela, je, atasikiliza mafunzo vizuri?

Labda useme kwamba, hela ya chakula ni kubwa, kuliko kusema kila mtu anunue chakula chake. Itafika muda wa kula, wengine wamejikunyata tu, mwisho wa siku watapata vidonda vya tumbo na hawatasikiliza mafunzo.
 
Pesa huwez kupewa kabla ya kazi , wakijitahd Sana utalipwa after one week , ndo mana walisema wataprovide tea asubh na msosi wa mchana , na wakatoa Rai inabd ujipange kwenye malazi na chakula cha usiku wakat ambapo wanaandaa malipo , asa we sku mbili tuu unataka upewe mpunga wote , ukichora na kishikwambi cha watu ...!!
Pesa ni ya nauli pia,
Sasa usipotoa nauli unategemea nini?
 
Hivi unaonaje kwamba, watu wapewe hela ya chakula ili wanunue wao, hali itakuwaje wale wazee wa zero cost, yaani hanunui chakula ili ku-save hela, je, atasikiliza mafunzo vizuri?

Labda useme kwamba, hela ya chakula ni kubwa, kuliko kusema kila mtu anunue chakula chake. Itafika muda wa kula, wengine wamejikunyata tu, mwisho wa siku watapata vidonda vya tumbo na hawatasikiliza mafunzo.
Ukijibana Zero cost na hela unayo huko ni kujitakia mwenyewe. Lakini heri upewe hela ukanunue chakula unachotaka, kuliko kupewa chakula cha buku kwa kukatwa 10,000/~
 
Umeongea Fact Sana
Hii nchi ngumu

Chakula wanaweka mwiko mmoja na Andazi 1 na chai....huu ni unyanyasaji

Wanawa-wa- underrate makarani lakin they forget hawa ndo kitovu Cha sensa when you treat them wrong. In early stage what do you expect?
 
Kwema Wakuu,

Semina Kwa Makarani wa Sensa imeanza Jana. Makarani wameshaanza mafunzo, na mdogo wangu ni mmoja wao akiwa anafanyia Mafunzo yake chuo cha Ustawi wa Jamii.

Sasa toka jana wanapigwa kalenda juu ya fedha zao za Mafunzo, Chakula na za Kujikimu. Hawajalipwa za Jana na za Leo pia.

Sasa cha pili wanaambiwa kua hata chakula hawatapewa hela ya chakula ambayo ni 10,000/- Kwa siku, bali wanalishwa chakula kisha wanakatwa hiyo hela.

Yaani kuna mtu hapo NBS amejipa tenda ya kuwapikia kisha yeye ndo achukue hizo 10,000/- kilazima. Chakula chenyewe anachowapikia hata Cha Mama Ntilie Cha Buku kina afadhali.

Hivi ni lazima kila kitu tuingize mambo ya dili? Kama hela zipo si muwape wajigharamie nauli za kuja huko kwenye semina? Hata chakula wapeni hela zao kisha pikeni hapo kwenye semina anaetaka kununua kwenu aje kununua kwa hiari yake Kwa bei ya Soko, sio kulazimishana kwa bei mnazozitaka nyinyi.

Hili ni zoezi muhimu sana, lakini mnaanza kuliharibu mapema tu sababu ya ulafi na uroho wenu wa hela za watu. Watu wanakuja kwenye semina huku wamenung'unika, mnadhan lengo la semina litafikiwa kweli hapo?
Msikilize kwa makini Jenerali Anne Semamba Makinda aka bi kiroboto.... mmeambiwa muwe wazalendo na kazi ni yakujitolea.
 

Attachments

  • d55f41f9bad5b5084f747dc48ad332d5.mp4
    1.5 MB
20220801_222748.png
 
Mmeanza kelele. Next time Bora kuchukua walimu tu. nyie wanyoa viduku ujuaji mwingi.

Na wamewawezea kinoma. Kutwa kulalamika kwamb wamepokonywa simu kwny semina so hawawez kuangalia video za daimondi wkt wa semina
 
Hii nchi inavijana wa hovyo sana na mtabakia kulalamika hvyohvyo mpaka kiama. Hizo nafasi Bora wangepewa waalimu tu wanajua system ya serekali kwenye ulipaji coz kunakuchelewa lakini haki ya mtu ataipata.

Yani day two ya training mtu analia njaa, hii nchi hatari
 
kwaiyo apo ni elfu 40 mara siku 19 sio haba labda wanaandaa taratibu za malipo labda wataweka ktk akaunt za benki si unajua tena mambo ya tozo maana pesa ya serikal nayo kuipata sio poa.
 
Back
Top Bottom