Pesa ni ya nauli pia,Pesa huwez kupewa kabla ya kazi , wakijitahd Sana utalipwa after one week , ndo mana walisema wataprovide tea asubh na msosi wa mchana , na wakatoa Rai inabd ujipange kwenye malazi na chakula cha usiku wakat ambapo wanaandaa malipo , asa we sku mbili tuu unataka upewe mpunga wote , ukichora na kishikwambi cha watu ...!!
Ukijibana Zero cost na hela unayo huko ni kujitakia mwenyewe. Lakini heri upewe hela ukanunue chakula unachotaka, kuliko kupewa chakula cha buku kwa kukatwa 10,000/~Hivi unaonaje kwamba, watu wapewe hela ya chakula ili wanunue wao, hali itakuwaje wale wazee wa zero cost, yaani hanunui chakula ili ku-save hela, je, atasikiliza mafunzo vizuri?
Labda useme kwamba, hela ya chakula ni kubwa, kuliko kusema kila mtu anunue chakula chake. Itafika muda wa kula, wengine wamejikunyata tu, mwisho wa siku watapata vidonda vya tumbo na hawatasikiliza mafunzo.
Karani povu la nini sasa, wewe damka kesho uwahi semina na jioni mpigwe tena sound kuhusu malipoWewe bana nimekuambia sina mchezo wa kuwageuza wanaume wenzangu, au leo soko gumu unalazimisha kwangu?
Msikilize kwa makini Jenerali Anne Semamba Makinda aka bi kiroboto.... mmeambiwa muwe wazalendo na kazi ni yakujitolea.Kwema Wakuu,
Semina Kwa Makarani wa Sensa imeanza Jana. Makarani wameshaanza mafunzo, na mdogo wangu ni mmoja wao akiwa anafanyia Mafunzo yake chuo cha Ustawi wa Jamii.
Sasa toka jana wanapigwa kalenda juu ya fedha zao za Mafunzo, Chakula na za Kujikimu. Hawajalipwa za Jana na za Leo pia.
Sasa cha pili wanaambiwa kua hata chakula hawatapewa hela ya chakula ambayo ni 10,000/- Kwa siku, bali wanalishwa chakula kisha wanakatwa hiyo hela.
Yaani kuna mtu hapo NBS amejipa tenda ya kuwapikia kisha yeye ndo achukue hizo 10,000/- kilazima. Chakula chenyewe anachowapikia hata Cha Mama Ntilie Cha Buku kina afadhali.
Hivi ni lazima kila kitu tuingize mambo ya dili? Kama hela zipo si muwape wajigharamie nauli za kuja huko kwenye semina? Hata chakula wapeni hela zao kisha pikeni hapo kwenye semina anaetaka kununua kwenu aje kununua kwa hiari yake Kwa bei ya Soko, sio kulazimishana kwa bei mnazozitaka nyinyi.
Hili ni zoezi muhimu sana, lakini mnaanza kuliharibu mapema tu sababu ya ulafi na uroho wenu wa hela za watu. Watu wanakuja kwenye semina huku wamenung'unika, mnadhan lengo la semina litafikiwa kweli hapo?
Nawewe hujalipwa huko ipogolo Iringa?Inachekesha kidogo, Ila mwambie dogo awe mzalendo
Mwigulu aliyaona mapema
Mmeanza kelele. Next time Bora kuchukua walimu tu. nyie wanyoa viduku ujuaji mwingi.
19kwani semina ni siku ngapi?
Huu ni upimbi sasa jina ufanyie nini?Issue ya kulipa ni nyingine ila kiwango umedanganya. Leta jina maana kitakwimu hakuna longolongo bwashee
Kwa taarifa yako pesa ni 50 na chakula ujitegemeeKwa siku wanapata 40,000/=. Na Wanapewa chakula.
Hii nchi inavijana wa hovyo sana na mtabakia kulalamika hvyohvyo mpaka kiama. Hizo nafasi Bora wangepewa waalimu tu wanajua system ya serekali kwenye ulipaji coz kunakuchelewa lakini haki ya mtu ataipata.